Sikuwahi kujua kama Mwingira wa Efatha kawekeza kijiji kizima namna hii!

Akili yako ni ya kulia na kuvaa, hivi hao watu 60 wanakaa hadi katikati ya uwanja? Lile kanisa ni kubwa taifa ndogo
Nawewe unakosea kudhania lile eneo la pitch katikati ya uwanja ni kubwa sana. Lile halizidi 160×120 sqm ukijumlisha na running tracks. Sasa katafute ule uwanja wote una sqm ngapi? Yale majukwaa yamejengwa kiufundi sana zile steps hivyo kupata eneo kubwa sana la kuketi watu. Bongo hakuna kanisa la watu milioni moja na wala hakuna kongamano wala makutano ya kidini linalifikia watu milioni moja ambalo liliwahi kufanyika au kutanisha watu kwa wakati mmoja sehemu moja. Nenda kawaongopee kondoo wenzio wanaovunwa sufu na nyama kwa huyo mchungaji wenu.

NYONGEZA......
Watu milioni moja sio mchezo hao, nikupe tu takwimu hizi kisha upime uhalisia:
Wakazi wa sehemu au nchi zifuatazo hadi sensa ya 2012
Zanzibar watu 1.304 Millions
Mauritius watu 1.256 Millions
Maldives watu 385,000
Unachosema ni kwamba uwazoe karibu wakazi wote wa zanzibar(Pemba na Unguja) namaanisha wanawake kwa wanaume na watoto wao uwapeleke Kibaha kwa Mathias ambapo kuna kijishamba kidogo cha Mwingira.
Je uliwahi kuhudhuria au kuona umati wa watu na vurugu inayotokea uwanja wa taifa na maeneo ya jirani kukiwa na mechi kubwa za Yanga na Simba au na Azam? Au mechi za kimataifa kama enzi zile za kocha Maximo? Nakuambia ni balaa la ajabu foleni njia zote. Umati ule ni wastani wa watu 70,000 tu ( 60,000 ndani, na 10,000 wapo nje kwa kukosa ticket au pesa au ni wafanyabiashara ndogo ndogo)
Utakuwa una kichaa wewe tena cha Dog.
 
Ni huko kibaha kwa mathias, upande wa kushoto unapotokea dar- 7km kuelekea kijiji kilipo ,Maelfu Kwa maelfu ya watu idadi (inakadiliwa ni kama Mara mbili au tatu ya ujazo Wa watu ambao huingia katika maonyesho ya siku yasabasaba) wamehudhuria kusanyiko katika kijiji kinachomilikiwa na mtume na nabii mwingila.
Nimefanikiwa kufika eneo hilo watu ni wengi sana na eneo ni kubwa sana takribani square mita 2,000,000sq na zaidi maarufu kama kijiji cha mwingila,
Huduma zilizomo ni Umeme, maji, network, bank hospital na sasa wanatarajia kuweka na hoter za kifahari,
Mkusanyiko huo umeleta watu kutoka kila mkoa na wengine kutoka nje ya nchi ambao kila kundi la watu wana mtaa wao Wa makusanyiko.
Mwenyeji mmoja kasema mkusanyiko huo hufanyika kila mwaka Kwa siku saba Kwa ajili ya waumini wake kupokea uponyaji,
Kushiriki mkutano huo, kila muumini huchangia Pesa Kwa ajili ya maradhi na Chakula,
Jumba ambapo mtume hupumzika hapatakiwi watu kukatiza ovyo.
Picha ya hapo chini ni kanisa lililopo huko lenye kubeba watu zaidi ya million moja
View attachment 605244
Kibaha ndo makao makuu ya Efatha mkuu.
 
watu 1M hzo ni ndoto tena za kiuwendawazimu ,huenda hadi unakufa hautakuja kushuhudia kusanyiko la hata nusu hyo uliyoitaja
Mkuu piga mahesabu Efatha kuna makanisa mangapi Tanzania ??sasa kila mwaka huwa kunasherehe waumini wote Tanzania wanakutana pale kibaha .pale kibaha ndo makao makuu.fika sikumoja uone palivo .mm nimefika sana kuna tenda fslan huwa nafanya nabank yanke .
 
Back
Top Bottom