Kijiji cha Materuni na utalii wa kahawa, Moshi Kilimanjaro

Funa the Great

Senior Member
Aug 1, 2022
160
271
Kahawa ni miongoni mwa zao la biashara linalolimwa ukanda wa Afrika Mashariki ikiwemo na Tanzania.

Mkoa wa Kilimanjaro ni miongoni mwa mikoa ambayo zao la kahawa linapatikana hususani kahawa aina ya ARABICA.

IMG_20231013_084247.jpg


Mnamo tarehe 16/10/2023 nilipata nafasi ya kuwapeleka watalii kijiji cha Materuni kilichopo wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro hakika nilijifunza mengi na kufurahi juu ya Utalii wa kahawa unavyofanyika ndani ya eneo ilo.

IMG_20231128_141051.png


Tulipata mwongozo wa namna ya kuandaa kahawa kutoka hatua ya mwanzo hadi mwisho huku tukisindikizwa na shangwe la nyimbo za asili kutoka kwa wenyeji wananaopatikana ndani ya kijiji icho.
Hutumika mashine maalumu kwa ajili ya kubandua maganda ya nje, baada ya hapo itawekwa kwenye sufuria na kukaangwa kwenye moto, ikiwa tayari itatolewa motoni na kupepetwa kwa kutumia ungo, itawekwa kwenye kinu kwa ajili ya kutwangwa wakati wa kutwanga watu hupokezana huku wakiwa wametengeneza duara kubwa na mtwangaji akiwa amezungukwa katikati huku akisindikizwa na nyimbo za asili, baada ya kutwangwa basi hatua ya mwisho inakuwa tayari kwa matumizi.

IMG_20231128_140236.png

IMG_20231128_141905.png

IMG_20231128_140205.png

IMG_20231128_140334.png


Ni eneo litakalo kufanya utamani kurudi tena kwa ajili ya kufanya utalii ndani ya kijiji icho sababu mwenyeji wake ni wakarimu na wamechangamka sana. Kijiji hupokea wageni tofauti kutoka mataifa mbalimbali.
IMG_20231128_124758.jpg


Haikuishia hapo tu wenyeji hawakutaka tunyimwe fahari ya macho tukafunga safari kuelekea kuyaona maporomoko ya maji yanayopatikana ndani ya kijiji icho maarufu kwa jina la MNAMBE WATERFALLS japo wengi huyafahamu kwa jina la MATERUNI WATERFALLS.

Hakika nilishikwa na butwaa kuona maporomoko marefu yanayotiririsha maji yake kutoka juu ya kilima kirefu hadi chini ya ardhi yenye maji baridi muda wote nikahisi nipo ndotoni naota na kujiuliza baadhi ya maswali "Hii ni Tanzania?. Hakika sikuweza kuzificha hisia zangu nilijawa na mshangao mkubwa na kujikuta naropoka "Sitaki mnirudishe nyumbani". Wenyeji wangu walicheka sana, basi baada ya hapo tukapata nafasi ya kuyagusa maji na kupiga picha. Baada ya shughuli zote kuisha siku yetu ikawa imeishia hapo na kuanza safari ya kuondoka huku nikiwa natazama macho nyuma kuendelea kufurahia uzuri wa eneo ilo.

IMG_20231128_124736.jpg


Baada ya hapo nikawaambia wenyeji wangu mwezi mwa kumi na mbili kuanzia tarehe 16-17 December 2023 kutakuwa na safari ya kutembelea hifadhi ya taifa Mikumi na maporomoko ya maji Choma.

KWA HUDUMA ZA SAFARI ZA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII CHEKI NAMI +255622174613

SAFARI ZA MARAFIKI, KIOFISI, COUPLES, VYUO/SHULE N.K.
Call/Whatsapp, +255622174613
 

Attachments

  • IMG_20231128_140334.png
    IMG_20231128_140334.png
    866.3 KB · Views: 2
  • IMG_20231128_140220.png
    IMG_20231128_140220.png
    739.1 KB · Views: 2
  • IMG_20231128_140236.png
    IMG_20231128_140236.png
    660.9 KB · Views: 2
  • IMG_20231128_140205.png
    IMG_20231128_140205.png
    619.3 KB · Views: 6
  • IMG_20231128_124715.png
    IMG_20231128_124715.png
    768.3 KB · Views: 4
Back
Top Bottom