Sikuwahi kujua kama Mwingira wa Efatha kawekeza kijiji kizima namna hii!

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Messages
5,084
Points
2,000

dmkali

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2014
5,084 2,000
Ni huko Kibaha kwa Mathias, upande wa kushoto unapotokea Dar- 7km kuelekea kijiji kilipo, maelfu Kwa maelfu ya watu idadi (inakadiriwa ni kama mara mbili au tatu ya ujazo wa watu ambao huingia katika maonyesho ya siku ya Sabasaba) wamehudhuria kusanyiko katika kijiji kinachomilikiwa na mtume na nabii Mwingira.

Nimefanikiwa kufika eneo hilo watu ni wengi sana na eneo ni kubwa sana takribani square mita 2,000,000sq na zaidi maarufu kama kijiji cha Mwingila. Huduma zilizomo ni Umeme, maji, network, bank hospital na sasa wanatarajia kuweka na hoteli za kifahari, mkusanyiko huo umeleta watu kutoka kila mkoa na wengine kutoka nje ya nchi ambao kila kundi la watu wana mtaa wao wa mkusanyiko.

Mwenyeji mmoja kasema mkusanyiko huo hufanyika kila mwaka Kwa siku saba Kwa ajili ya waumini wake kupokea uponyaji, kushiriki mkutano huo, kila muumini huchangia Pesa Kwa ajili ya malazi na Chakula. Jumba ambapo mtume hupumzika hapatakiwi watu kukatiza ovyo.

Picha ya hapo chini ni kanisa lililopo huko lenye kubeba watu zaidi ya million moja

IMG_20171008_192914.jpg
 

Forum statistics

Threads 1,344,387
Members 515,453
Posts 32,819,130
Top