Sikutegemea nitakuja kuwa single mother in my life

Sikutegemea nitakuja kuwa single mother in my life

Status
Not open for further replies.
Hadithi yako imenisikitisha sana...wakati mwingine maisha hayapo fea kabisa!!

Ni kweli kabisa Eli76 ,usawa kwenye maisha ya mahusiano wakati mwingine haupo ni kama bahati nasibu tu.
Samahani kwa kuchelewa kujibu.
 
Hongera kwa kupata mtoto. Badili mtindo wa maisha. What is single mother? Nothing exist as multiple mother. Hakuna mtoto aliyezaliwa katika matubo zaidi ya mama mmoja. Unaota kitu hakipo. Single mother ndio Mungu alivyotaka.
Kitu unachotamani ni Ushirika wa mwana ume ambalo sio jambo la msingi. Tambua unaye tayari, umeshirikiana naye kuzaa. Sasa unataka Ushirika gani tena zaidi huo?
Fahamu kuwa kuna wengine hata huyo mtoto hawana.
Badili mtizamo, uko normal kabisa kama ni maisha ndio yako hivyo.
Walio na shirika, hupoteza shirika zao ndani ya muda mfupi tu.
 
change your mind. kupata mwanamume bora kunaanzia kwenye MIND SET yako.....angalia huwa unataka mwanamume wa vigezo vipi? ukishakosea katika aina ya mwanamume unayemtaka basi utakasea pia mpaka katika MAZINGIRA ya kumpata huyo mwanaume.
kitu kingine badili fikra zako kuhusu KUOLEWA ndoa haitafutwi it comes automatic na hivyo hivyo mume HATAFUTWI atampata tu. unachotakiwa kufanya ni KUTULIA na KUJITUNZA. ukihangaika kuitafta ndoa au mwanamume utatahamaki una watoto wengine kibao na wote baba zao wamekimbia.
Rudi kwa Mola wako, ishi maisha ya kumpendeza Mungu na muombe Mungu atakuletea a dream man wako.
wanaume wako hivi: when it comes ishu ya kuoa wanakuwa makini sana kutafta mtu alietulia na anaejua maisha na mara nyingine hata kama uwe umeshazaa hawajali ilimradi uwe mtu uliejituliza na uko focused katika maisha.
wasichokijua wanawake wengi ni kule kudhani kuwa kuvaa kuvutia wanaume(sexy) au kuendana na fashen za kileo ndio njia bora ya kuwapata wanaume. hapo utapata wale wapita njia tu ila si serious man.
yote kwa yote lea mwanao na tengeneza maisha yako . you are in charge of your own life! jitunze jiheshimu na mheshimu mwanao pia, usiwe na papara ukawa kila siku unamtambulisha mwanao huyu anko X Mara huyo Anko Y ....Utamharibu pia na mtoto. pole kwa maswahibu ....dunia ndivyo ilivyo

Mkuu umemaliza kila kitu.
 
Ukipata helkopta niite tushirikiane . i have a better idea in mind.
Niwasalimu wote na pole mlotoka kazini, mlokuwa mmekaa home kizembe acheni mafanikio nikujituma , mnaoumwa poleni,

miaka kadhaa iliyopita nilikuwa binti mwenye nidham sana niliheshimu wanaume kwa wanawake, sikutarajia kufanya mapenzi kabla ya ndoa,

hata walokuwa wakinitongoza nikiwa kidato cha 4,5,6 niliwakataa kwakuwa walishindwa sharti lakusubir hadi nimalize masomo tufate utaratibu ,

nikaenda chuo nikawa na kijana mmoja hivi naye hivyo hivyo, alikuwepo kijana mmoja tulifahamiana pale ila alikuwa anatoka wilaya jirani akarusha ndoana nlivyomwambia no akatulia. Tukaendelea kuwasiliana kama washkaji tu kawaida na marafiki kwa alipotezea kama aliwahi nitongoza ila ndo haipiti week bila ' hi single mother'

2012 nikapata kazi ile naripoti tu nakutana naye ofisi hyohyo kaja naye kusain mkataba eeeh bwana urafiki ule ukawa tooo close ndo akanambia sahivi tuna kazi hebu tukubaliane nkaona isiwe tabu kila mti akaweka yake hadharan pale mi nlikuwa na mafupi tu kuwa nlishakuwa na x, y ila hawakuweza shart lakusubiri basii hatukuwa wapenzi

eeh bwana si mnajua tena mambo ya kuanza mapenz ukubwani tukaendelea hivyohivyo tukawa timekubaliana aende kwetu basi ili kuweka mambo vizur kaniunganisha na mamake, shangazi sometimes babake japo niwasalimu na akanambia nimwelekeze shangazi yake namna yakufika kwetu tukafanya hivyo,

ile kukaa pamoja mara kwa mara ikatokea tukavunja amri ya mungu mara 1,2,3 mimba duuu eee kimbembe kikaanza umezaa mno haraka na wakati kulingana na ugeni wa hayo mambo nlikuwa na kataa hadi nalia ila ndo unakuta umekuja kumsalimia kwake utapiga kelele ubakwa? haifai wangejiuliza uliingia kufata nini

basi akanambia japo tutaoana ika hyo mimba toa siitaki labda kama si yangu ila kama ni yangu toa ukizaa uajijua, basi ugomvi wakutoa mimba ndo ukaibua mazito kumbe kazalisha wanawake 3 na ndo hivyo wana maisha magumu kazi yake kuwadhihaki , kumbe ni mshirikina yeye na familia yake, tulivyogombana nkayajua hayo nkamwambia kwa style hii hatuwezani akawa anachart na babake mzazi eti watafute mtaalam anitengeneze sikuamin macho yangu,

mimba ile sikutoa maana hata naanzaje kuulizia mambo hayo basii nkazaa mtoto wangu nakumbuka mimba ilikuwa na complication kibao hadi nadondoka baranaran na mambo mengi ukimwambia anajibu kwa hiyo mi ni daktari au? ulivyokataa kutoa mimba ulitegemea nini?

basi nikakubaliana na hali nikalea mwanangu ana miaka 3 now, kuna kijana mmoja ananifwatilia siku nyingi nkaona si tabu hebu nijaribu tena ndo tunawasha moto wa mapenzi hata haujawaka vizur nadaka mesage za mkewe ni mme wa mtu nikajiona mwenye nyota ya bunndi

ni bora tu ningeanza mapenzi hata tangu zamani, nimemkosea nini mungu( ni huo uzinzi nlofanya nkabeba mimba?) nakosa suluhisho hili jambo linaniumiza sana moyoni japo wanaoniona nacheka hawawezi kujua, natamani nitumie helicopter nimwagie wanaume wote petrol angani niwalipue nawaona waatili sana hawana huruma,

nafikia mahali nawaza niwe na style gani ya maisha niwaepuke wanaume kama ebola.
 
anza hii ya kujiita single Mother, unazid kujilabel!

af pls pls hiyo petroli shosti usimmwagie mangi wangu!
this is to tell u, bado mapenzi yapo na ukiamua kuyafurahia unaweza! usiache jambo moja toka kwa wapuuzi flan ukaona dunia nzima haina watu!.
 
Karma is a bitch,haya maisha bana hayatabiliki....mimi ndio maana naishi kama kesho haipo na sina nnachojutia kuhusu maisha yangu ya nyuma.....pole Dada Mungu akutie nguvu
 
Wewe ni mmoja wa mifano mingi ya dada zetu. Wanakubali kuzalishwa bila kua na uhakika kama wataolewa na hao wanaume au vipi. Hii ni wazi kua jamaa amekutoa sokoni yaani hauuziki kabisaa na ukiangalia the market is very competitive.
Anyways jikubali, Fanya mambo yako na ujiamini. Chukulia ndoa ni option tu na sio lazima katika maisha yako.
 
Pole sana dada kwenye mapenzi Hakuna mzoefu siku zote tunajifunza kutokana na makosa
 
Dada najua umeumizwa na nivigumu kurudisha furaha yako ila kitu kimoja mnikwamba maisha yapo hivyo tafuta mtu mmoja uwenaye kimaisha mambo yataisha Mungu kaumba kusahau!
 
Umenifanya niwe na mtazamo chanya (positive) juu ya single moms.

pole sana
 
Mm sijawai kutendwa ila natenda. Kwa alichofanyiwa mdogo wangu nina machungu na hawa viumbe. Siku ukifanikisha petrol nijulishe na mm nitafute tindikali ili zoezi litimie. Helcopiter tutapata nitaongea na kamanda mmoja hivi.
Hebu weka sura yako tuione
 
Ni bora tu ningeanza mapenzi hata tangu zamani, nimemkosea nini Mungu (ni huo uzinzi nilofanya nikabeba mimba?) Nakosa suluhisho hili jambo linaniumiza sana moyoni japo wanaoniona nacheka hawawezi kujua, natamani nitumie helicopter nimwagie wanaume wote petrol angani niwalipue nawaona wakatili sana hawana huruma.

Nafikia mahali nawaza niwe na style gani ya maisha niwaepuke wanaume kama ebola.
Pole sana ..... Wadada wengi huwa mnajiachia mno ktk mapenzi au uchumba matokeo yake jamaa anakupa mimba alafu anakuacha ...haya yote yasingekuwepo unless mngejikinga mpaka mnakapokua mnazaa mkiwa ndani yandoa ....ndan yandoa ukiachwa wewe sio single mother Bali ni mwanamke alofiwa mumewe ...


Pole sana Dada ,,naona maumiv moyon mwako ..pole sana .
 
Ni bora tu ningeanza mapenzi hata tangu zamani, nimemkosea nini Mungu (ni huo uzinzi nilofanya nikabeba mimba?) Nakosa suluhisho hili jambo linaniumiza sana moyoni japo wanaoniona nacheka hawawezi kujua, natamani nitumie helicopter nimwagie wanaume wote petrol angani niwalipue nawaona wakatili sana hawana huruma.

Nafikia mahali nawaza niwe na style gani ya maisha niwaepuke wanaume kama ebola.
Mmwagie petrol huyo ulozaa naye acha kuwa na gubu na jifunze kupambana na hali yako!
 
Tatizo la binadamu hatuna shukran
HV do I think having a kid is a curse au blessing?
No iffence but Nyie ndo watu ambao mnajitafutia laana za bure wenzio wana ndoa miaka hata ishirini hawajabahatika kupata watoto wewe unajilaumu,what a shame?
Na aliyekuambia kila relationship lazima itunge ndoa ni nani?
Shukuru kwa kila jambo,kua kwenye ndoa haimaanishi utakua happy
Sikujui but am very disappointed with your mind is stupid and small minded!
Anyway be blessed

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom