Sikutegemea nitakuja kuwa single mother in my life

Sikutegemea nitakuja kuwa single mother in my life

Status
Not open for further replies.
Hata usijute.
Wengine wameolewa na ni single mothers huko ndoani.
 
Pole sana,mshukuru Mungu kwa yote! cha msingi jipe mapumziko ya muda katika mapenzi!anza na msamaha kwa waliokutenda halafuomba sana Mungu!ila nakushauri utakapoamua kuwa na mahusiano tafuta aliyekuzidi umri,mtu mzima anayejielewa na itapendeza akiwa mgane au single parent mwenzako!.shukuru Mungu una kazi yako,na ukae ukijua wewe sio wa kwanza kupatwa na majaribu kama hayo!
 
Duh pole sana ata mimi niliwatenda wengine huko nyuma, nikikumbuka uwa najilaumu sana, kwa kweli kidonda cha mahusiano ni kibaya sana.
 
Ukishatumwagia petrol,wanawake wenzio wanaotuhtaji watabaki na nani?
 
This world is dam crazy wakati mi nimelia na kusaga meno almost a month now sili vizuri, silali sifanyi shughuli zangu coz of rejection by a lady, somebody else somewhere analia ameachwa......who started love??



Mkuu haya mambo viceversa yani najionea tabu tu wengine wanalia baada ya kusomesha na kukimbiwa wengine tena ndio kama hivi
 
Cha ajabu unakuta mwanamke kama wewe ulitongozwa na wanaume smart kabisa wanaokupenda kwa dhati na wenye nia njema na wewe ukadengua.

Sometimes wanawake kinachowakuta huwa mmekitaka wenyewe, huwa mnajitakia matatizo.

Unajuaje kama hao wanaume wasingemletea mabalaa zaidi ya hilo alilonalo sasa?

Kosa la huyu Single mother ni kubadili gia angani, ajaweka kando msimamo wake aliokuwa nao mwanzo.
 
Last edited by a moderator:
Ur story isn't bad..by the way ur situation isn't ur fault wakulaumu ni hao majamaa ambayo hayakuona thaman yako..wat I can advice u z try to find happiness from within usiitafute kwa mtu yotote yule.u will b happy by by setting goals that u can archieve..second usinishushe chini raise ur standards back to normal usiwe cheap simply bcoz umezaa..penda mwanao lea mwanao n life goes on.Who knws what future brings???
 
yawezekana , ila kumbuka kila anayekutongoza anatumia nakupenda single mother blabla blaa hivyo ni ngumu kutambua moyo wa mtu, unakuta yule unayemkubalia kwa mara ya kwanza unakuwa mwaminifu kwake kumbe ndo hivyo

Wewe ulichokosea nj taratibu tu. Uliona ni bora umridhishe mwenzako kuliko kuridhika wewe! Ikiwa uliona kwamba ni vema kushiriki tendo la ndoa baada ya kufunga ndoa kwanini hukusimamia msimamo wako huo? Huoni kulegeza kamba kwa huyo mwanaume ni kuwanyima fursa waliokutokea kabla yake?

Matatizo uliyoyapata usiweke matumaini yoyote kwamba Mungu atakulipia au atamlipa huyo mwanaume sawasawa na aliyokufanyia wakati wote mlikiuka amri yake ya kutofanya zinaa/uasherati kabla ya ndoa. Kwahiyo umevuna ulichopanda; subiri fursa nyingine kama itakuwepo.

Ukipanda mahindi usitarajie kuvuna mpunga.
 
Pole sana, kama umeweza kumlea mwanao mpaka
kafikisha miaka 3 , basi maisha unaweza ukayaendesha,
usibabaishwe na mfumo dume. we komaa tu na mwanao.
 
change your mind. kupata mwanamume bora kunaanzia kwenye MIND SET yako.....angalia huwa unataka mwanamume wa vigezo vipi? ukishakosea katika aina ya mwanamume unayemtaka basi utakasea pia mpaka katika MAZINGIRA ya kumpata huyo mwanaume.
kitu kingine badili fikra zako kuhusu KUOLEWA ndoa haitafutwi it comes automatic na hivyo hivyo mume HATAFUTWI atampata tu. unachotakiwa kufanya ni KUTULIA na KUJITUNZA. ukihangaika kuitafta ndoa au mwanamume utatahamaki una watoto wengine kibao na wote baba zao wamekimbia.
Rudi kwa Mola wako, ishi maisha ya kumpendeza Mungu na muombe Mungu atakuletea a dream man wako.
wanaume wako hivi: when it comes ishu ya kuoa wanakuwa makini sana kutafta mtu alietulia na anaejua maisha na mara nyingine hata kama uwe umeshazaa hawajali ilimradi uwe mtu uliejituliza na uko focused katika maisha.
wasichokijua wanawake wengi ni kule kudhani kuwa kuvaa kuvutia wanaume(sexy) au kuendana na fashen za kileo ndio njia bora ya kuwapata wanaume. hapo utapata wale wapita njia tu ila si serious man.
yote kwa yote lea mwanao na tengeneza maisha yako . you are in charge of your own life! jitunze jiheshimu na mheshimu mwanao pia, usiwe na papara ukawa kila siku unamtambulisha mwanao huyu anko X Mara huyo Anko Y ....Utamharibu pia na mtoto. pole kwa maswahibu ....dunia ndivyo ilivyo
 
Tatizo wanawake wakishapata kazi tu basi wanabaki wanawaza kuolewa any guy akijitokeza mwenye kazi au pesa basi kakubaliwa but pole kwa yote bibie
 
Nimegundua NEW AGE mna ukosefu wa elimu ya mahusiano ambayo inapelekea pale mnakuja kuingia na kukutana na power of love unakuja kumuona mwenzako sawa na shetani.

//siyo maana yake hiyo//
Hebu tujiulize kwa wale mnaowaita old age waliishije ktk mahusiano pasi kuwepo kwenye NDOA?
 
Sijui kwanini wanawake mnaojidai kubanabana miguu kwa staili yako hii mnaishiaga kuwa na nyota ya bundi kwenye mapenzi
 
Kilichokuponza ni kufikiri mme bora utampata kwa kutokuhusiana nao... Wakati mwingine ni sawa ila inahitaji hekima na wasaidizi ambao watakusaidia kusoma tabia zao. Kimtazamo na kifikra au na jinsi ulivyoaminishwa kwamba mme bora ni yule asiye na mihemko ya mapenzi au mwenye kuvumilia hadi takwa lako litimie, na hiki ndicho kilichokufanya usijue tabia nyingine mbaya zaidi za mapendapenda sasa kila ukigusa ndio umetulizwa na pendapenda wa mitaala kibao.

Ushauri
Rudia nyuma na anza kujifunza tabia za wanaume na hapo utajue wakweli wanaongea vp na waongo wana swaga gani.... Pia kwa dunia ya sasa kigezo cha hadi ndoa wanakiweza baadhi ya wahindi na waarabu hivyo take time na mchuchu unayempata bila kujirahisisha kama mwenye mkato wa tamaa, amini kuwa mmeo anateseka gizani kukutafuta ila umekaa upande mwingine. Pia usichukie wanaume kwa sababu ya maisha uliyopitia kwa wanaume wapo wengi wazuri na wenye mapenzi/mahaba ya dhati sema ndio hujaangukia humo.

Mwisho usisahau kumshirikisha mungu hitaji lako na muda usio muda imani yako itatenda maajabu usiyoyawaza.
 
ni bora tu ningeanza mapenzi hata tangu zamani, nimemkosea nini mungu( ni huo uzinzi nlofanya nkabeba mimba?) nakosa suluhisho hili jambo linaniumiza sana moyoni japo wanaoniona nacheka hawawezi kujua, natamani nitumie helicopter nimwagie wanaume wote petrol angani niwalipue nawaona waatili sana hawana huruma,

nafikia mahali nawaza niwe na style gani ya maisha niwaepuke wanaume kama ebola.

Nakuonea huruma sana dah! But umekata tamaa too early. You still have time and with care u can always find someone. Wala usiregret kwa sababu having a child out of wed lock is confusing. It is wrong kwa namna nyingi tu contrary to ukimwangalia mwanao strugling to undestand life, so innocent and the love u feel (Jamani kuwa na mtoto ni raha).
Just focus on being a mum, ni jukumu kubwa na muhimu kwenye jamii. It is rewarding na hata mungu atakuona kuwa umekuwa mama muaminifu. While u are at it kuna atakayekuona na mwanao aseme I want a wife like that. Huyo atakuchunguza kwa mengi na hataconcentrate kwenye suala na wewe kulala naye.
 
Huna nyota ya bundi wala huna tatizo.... Tena Mungu anakupenda sana.... Ni vile hujui tuu.. Unafaham kama ungeoana na mshikaji ni nn kingetokea? In every situation God has something to say.... Mshukuru Mungu usimlaum.


Ushauri mzuri sana. Ktk kila hali bado Mungu anaweza kutoa majibu mazuri zaidi
 
pole sana dada yangu, na hongera kwa kujitahidi kulea mwanao,
hayo ni mapito tu ya dunia, una uwezo wa kufanya kazi jitume, kuwa busy na kazi zako lea mtoto wako,

ondoa hicho kisasi ulichikweka moyoni dhidi ya wanaume, si kweli kuwa wanaume wote wana matatizo nakuhakikishia wapo wengi tu wenye mapenzi ya dhati na uelewa tatizo ni muda tu.
wakati utafika utampata prince charming wako na utasahau kama uliwahi kuumizwa trust me.
have faith, jiamini na ujikubali wakati bado
mwombe mungu akupe mtu mwelewa, usiingie kwenye mahusiano ukiwa desperate, jipe muda na mwanaume anaekuja umwambie ukweli awe tayar kukupenda wewe na mwanao.

#bestrongbepatientneverloosehope# you will b e happy one day
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom