Sikutegemea nitakuja kuwa single mother in my life

Sikutegemea nitakuja kuwa single mother in my life

Status
Not open for further replies.
Acha chuki wanaume hatuna shida ila mara nyie mnawakubalia wapigaji kuliko waowaji kwa huna haja ya kumlaumu mtu
 
duuuh pole aisee,,,ndo utu uzima uo just embrace the experience
 
Dada usikate tamaa, japo dunia imejaa viatu na watu ni wachache, Muombe Mungu atakusaidia. Usituchukie wote, je na huyo mtoto wako angekuwa wa kiume naye ungetamani umumwagie petrol? Utakuja mpata mwanaume atakupa raha mpaka utakuja simulia humu JF. Kila la kheri, fungua madilisha kama mlango umefunga.
 

Usilie na kulalamika, wapo wengi wanaolia na kusumbuka katika maisha ya kimahusiano kuliko wewe.. Jipe mapumziko mafupi katika masuala ya mahusiano, angalia Wapi unapokosea kisha futa Vumbi simama imara Piga goti kwa Mungu kila kitu kitakuwa sawa Mama. Kwa Ushauri nicheki 0719846425
 
Last edited by a moderator:
Kwanza toa msamaha wa kweli kutoka moyoni kwako kwa watu wallkuumiza, pili
Mungu ni mwema sana, Fanya maombi kwa kufunga na kuomba toba akusamehe kisha , mpe nafasi katika maisha yako hakika atakutendea maajabu utashangaa.
 
Mi naamin hakuna mwanaume hata mmoja anaezidi ukatili kama firauni hapa duniani (sioni sababu ya kuwachukia )jipange omba toba, amin mungu anasikia na kuona ,naamin ipo siku utampata mwenza bora katika maisha yako, all the best dada
 
Mm sijawai kutendwa ila natenda. Kwa alichofanyiwa mdogo wangu nina machungu na hawa viumbe. Siku ukifanikisha petrol nijulishe na mm nitafute tindikali ili zoezi litimie. Helcopiter tutapata nitaongea na kamanda mmoja hivi.
 
A good man is hard to find.... Pole sana maisha hayatabiriki
 
Ulimwengu wotw ungekuwa Na fursa ya mwanaume kuwa Na wanawake wengi basi ungekuwa ushasitiriwa tatizo Ni wanawake hampendi kujua Kama mnashea mwanaume
 
Cha ajabu unakuta mwanamke kama wewe ulitongozwa na wanaume smart kabisa wanaokupenda kwa dhati na wenye nia njema na wewe ukadengua.

Sometimes wanawake kinachowakuta huwa mmekitaka wenyewe, huwa mnajitakia matatizo.
 
singleMother pole sana DD angu!

Naamini jibu lipo juu ya haja yako.

Kama upo dar, nakusihi fika kwa mtumishi huyu BONIFACE MWAMPOSA pale Vatican city sinza!!

Unahitaji msaada wa kiroho zaidi! kwa Mungu yote yanawezekana.

jnne na jtano ndyo ibada zake.

AMINI TUU.

Usimsikilize mwovu atakaebeza. Isikilize sauti ya Mungu UPUMZISHWE mzigo wako. AMINI TUU
 
Last edited by a moderator:
Dada yangu pole sana, nimepata picha ya yaliyokupata, najua ulivyoteseka kulea mimba. Sijawahi kulea mimba ila hukustahili mateso hayo yote. Ulistahili upendo wa mzazi mwenzako.
Natamani nikutafute niongee na wewe, ningekufariji na nina uhakika ukiondoka utakuwa umebadilika na utakuwa na fikra mpya , so sad haiwezekaniki.
Ila you have my prayers. Nimeumia sana kusoma bandiko lako. Lina hisia kali san na halihitaji kejeli.
Usikate tamaa. Na usinwombee mabaya aliyekufanyia ubaya,mwachie Mungu.
Pole sana dada yangu, sitasita kukuweka kwenye my prayers
Alamsiki!!
 
Samahani hiyo ya helikopta umenivunja mbavu.

Usijilaumu hayo yametokea labda ungeolewa nae baba mtoto ungekoma zaidi. Mshukuru Mungu amekupa mtoto na amekutoa kwa huyo mkaka.

Cha muhimu usiweke hasira moyoni jisamehe na kubali, ma weka fikra na imani kuwa muda wako utakuja aliokupangia Mungu.

Sali akuletee mtu anayejua mtaendana na kupendana na atampenda mwanao.
 
This world is dam crazy wakati mi nimelia na kusaga meno almost a month now sili vizuri, silali sifanyi shughuli zangu coz of rejection by a lady, somebody else somewhere analia ameachwa......who started love??
 
Aliyekwambia kuwa na mtoto ni ugonjwa ni nani???

Kuumizwa mapenzini ni kitu cha kawaida...jikung'ute songa mbele
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom