Sikutegemea nitakuja kuwa single mother in my life

Sikutegemea nitakuja kuwa single mother in my life

Status
Not open for further replies.

Single mother

Senior Member
Joined
Jun 10, 2015
Posts
158
Reaction score
57
Ni bora tu ningeanza mapenzi hata tangu zamani, nimemkosea nini Mungu (ni huo uzinzi nilofanya nikabeba mimba?) Nakosa suluhisho hili jambo linaniumiza sana moyoni japo wanaoniona nacheka hawawezi kujua, natamani nitumie helicopter nimwagie wanaume wote petrol angani niwalipue nawaona wakatili sana hawana huruma.

Nafikia mahali nawaza niwe na style gani ya maisha niwaepuke wanaume kama ebola.
 
Huna nyota ya bundi wala huna tatizo.... Tena Mungu anakupenda sana.... Ni vile hujui tuu.. Unafaham kama ungeoana na mshikaji ni nn kingetokea? In every situation God has something to say.... Mshukuru Mungu usimlaum.
 
Mbavu bhana, muda wote zinawaza kuwa nje ya mwili wake
 
  • Thanks
Reactions: DLS
Don't lose hope matatizo sehemu ya mwanadamu utampata mwingine atakaye kusahaulisha yote
 
Duh!
Naona kuna jambo umeshindwa kuliona hapo.
Ni kwamba MUNGU amekusaidia sana.
Inawezekana kwa kuwa hujaliona hilo na kumshukuru ndio maana huoni nini ufanye ili kusonga mbele.
 
Pole sana single mother, hauna mkosi sema umekutana na majambazi ya mapenzi, kuna watu wamepitia situations mzito kuliko zako na bado wanayafurahia maisha na wamewapata wenza wanaowapenda.

Ukimuona nyani mzee ujue kakwepa mishale mingi.
 
Single mother unataka kutumia chopa kutumwagia petrol wanaume wote kwa makosa ya wanaume wawili tu. sio kihivyo sasa
 
Last edited by a moderator:
Single mother nadhani hadi hapo umeshajifunza kwamba kupata mwanaume ni jambo gumu sana. Nadhani pia ikiwa ungeombwa kuwashauri kitu mabinti wa sasa ungewaambia kitu ambacho kwa hakika hawatakubalina nawe.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana kwa yote uliyopitia,naomba nikutie moyo kuwa kukosea ndio kujifunza.
Tulia na jipe mda wa kutafakari mapito yako.
Maisha ni zaidi ya mapenzi,shukuru Mungu una mtoto mlee na hakikisha anapata kile anochotakiwa kupewa kama haki yake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom