Pole Bebii kwa hao waliokukwaza.
Cha msingi ni kuwapotezea tu na maisha yaendelee, elewa tu hapa JF kuna members wenye mitazamo tofauti na tabia mbalimbali vilevile.
Uhuru wa kutoa maoni wakati mwingine unatumiwa vibaya na baadhi yetu, na hili linachangiwa sana na utaratibu wa kutokua na identity halisi ya baadhi ya members, na zaidi ya yote, hakuna interview au qualificatins za kuwa member bora ujue kusoma, kuandika (kidhungu kidogo), kutumia computer basi tunajiunga tu.
Mimi naamini kuendelea kuwepo JF bado kuna faida nyingi zaidi kuliko kuiacha kwasababu ya hao wachache wanaotumia vibaya uhuru ulopo.
Kuna members humu wana busara za ajabu hadi mtu unatamani ukutane nae ili muongee zaidi na wanasaidia sana kuonyesha umuhimu wa JF.
Usiondoke bwana, wengine tumepunguza sana kukaa vijiweni kwaajili ya breaking news pia tunajifunza mambo mengi sana hapa. Mwenzio ofisini naonekana bingwa wa latest news hadi wananishangaa coz siendi mtaani wala sina gazeti lakini nikishusha news wanapagawa kuona iko kwenye media baadae.
Pia kuna member mmoja alipatwa na msukosuko ktk safari yake siku moja akaingia JF kupata maoni na msaada, members waliungana nae kumuombea na akafika salama (somebody Elli). Kwahiyo JF bado ni nzuri ukiacha hao wachache wanao wakwaza wenzao.
Ohooo...nimeandika sana dada wewe, hebu nisikilize basi usiondoke sawa ''swetie''