Ushauri kwa Wazee wenzangu, Boko, Chama, Saidoo na wengineo

ANTDOTE

JF-Expert Member
Oct 14, 2023
217
605
Ni ushauri tu kwa Wazee wenzangu, Boko, Chama, Saidoo na wengine. Ni heri kuuwahi wakati kabla wakati haujakuwahi. Embu igeni ya Onyango. Alipoona Mwili unaanza kukataa akaomba mwenyewe thank you.

Mimi ni mwanamazoezi mzuri tu, tena wa muda mrefu. Ila nikitazama performance yangu mazoezini Leo na Miaka 2 iliyopita Kuna nguvu imeanza kupotea.

Wazee wenzangu ninyi mna record nzuri tu katika football, embu msisubiri record hizo zibadilike na zikabadisha wasifu wenu maana Kuna maisha after football age.

Mfano Hayati Mwalimu Nyerere, alipoona misuli yake ya kukabiliana na Siasa za Dunia zilizokuwa zinabadilika kwa Kasi, haiwezi kustahimili, aliamua kuachana na uongozi (king'atuka). Hili lilimfanya kulinda sana hadhi na thamani yake. Na ushauri kama huo aliwapa Wazee wenzake kina Kaunda na Mugabe, wao walikaidi Lakini mwisho wake walikutana mwisho wa fedheha.

Mzee mwenzangu Chama ni juzi tu nilikuona hata mbio uwanjani zinakukataa. Ukiwa Mbele ya mpinzani mita kadhaa aliweza Kutoka nyuma na kukupora Mpira na kukupita.

Sisemi wengine kama kina Miquisone, ambao sijui wamekutwa na Nini uarabuni.

Kwa ufupi niishie hapa, wakati nikiandaa ushauri mwingine kwa Mzee mwingine, Raisi wa Maisha (Kama Kamuzu Banda), Mzee Mo Dewj
 
Back
Top Bottom