Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,529
- 41,044
Unajua tusishabikie mambo bila kujua kwa sheria za kiislam hairuhusiwi mtu kuagwa, Pia maiti ikifa izikwe haraka, haya ndo mambo ya kuzingatia ila kwa nyie cdm mnaona ushindi kwa wanafamilia wamemtesa maiti wao na wamepata Laana kwa Mungu maana asipozikwa musilam kwa mafundisho MwenyeziMungu hushusha laana kwa waislam wa mji wote. Ndo maana kina sheikh shaabani kuogopa hilo walimfuata mzee naye alikataa kuogopa chadema kwa maneno yake
Hatuingilii mafundisho ya dini, cha msingi ni kwamba Mzazi wa marehemu hakushinikizwa na mtu yeyote wala CHADEMA kuupeleka mwili wa mwanawe uwanja wa NMC. Kama ametenda vema au vibaya kadiri ya imani yake, tumwachie mwenyezi Mungu ndiye mwenye haki ya kumhukumu. Tusijifanye kuwa sisi ni watu wenye haki sana mbele za Mungu, maana hekima ya Mungu siyo hekima ya mwanadamu. Sisi sote tulihuzunika kusikia kuwa CHADEMA ililazimisha mwili wa marehemu kupelekwa uwanjani, maana tunajua CHADEMA inaheshimu sana imani za watu. Tumefarijika kuwa mzazi wa marehemu, pamoja na kujua mahitaji ya imani yake, aliupeleka mwili wa mwanawe uwanjani kwa hiari yake na siyo kulazimishwa na CHADEMA kama ambavyo CCM/Serikali walivyotaka kutudanganya.