"Sikushinikizwa kumpeleka mwanangu uwanjani"- Baba mzazi wa Ismail | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Sikushinikizwa kumpeleka mwanangu uwanjani"- Baba mzazi wa Ismail

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alfu Lela Ulela, Jan 16, 2011.

 1. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Baba mzazi wa kijana Ismail aliyepigwa risasi na kuuawa na polisi huko Arusha, katika mapambano kati ya Jeshi la polisi na wafuasi wa CHADEMA amesema kuwa hakukuwa na shinikizo lolote kupeleka mwili wa mwanae viwanja vya NMC kwa ajili ya ibada ya kumuaga.

  Mzazi huyo amesema uamuzi wa kupeleka mwili huo viwanjani NMC ulikuwa ni uamuzi wa familia na hakukuwa na shinikizo lolote kutoka nje ya familia kama ilivyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari hapo awali.

  "Yalikuwa ni maamuzi ya familia kuwa mwili wa Ismail upelekwe viwanjani kuagwa na hakukuwa na shinikizo lolote kama inavyodaiwa." alisema mzazi huyo na kuongeza
  "Tuliamua kufanya hivyo ili kuuonesha ulimwengu ukiukwaji haki uliyofanywa na jeshh la polisi"

  Taarifa hii inakuja siku chacie baada ya kuenea uvumi kuwa wazazi wa Ismail walishinikizwa kupeleka mwili wa marehemu viwanja vya NMC kwa ajili ya ibada ya mazishi.

  Uvumi huo ulizidi kupaizwa na vyombo vya habari, na kukihusisha chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusika kuishinikiza familia kuileta maiti ya Ismail uwanjani NMC.

  Kwa maana hiyo taarifa ya mzazi wa Ismail inakisafisha chama cha CHADEMA kutokana na kupakaziwa na kuchafuliwa na taarifa za uvumi zilizotolewa awali.

  Vilevile taarifa hii inaonesha wazi namna baadhi ya watu wenye nia mbaya wanavyopika habari na kuzivumisha, huku wakichafua wengine kwa alili ya maslahi yao wenyewe.

  Pongezi kwa mzazi wa Ismail aliyeamua kueleza ukweli. Pongezi CHADEMA kwa kuruka kiunzi cha kutaka kuchafuliwa kwenye kazi njema mliyoianza.

  SOURCE:Radio One.
   
 2. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #2
  Jan 16, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  good, huo ndiyo uanaume mkuu, tufanyeni kazi huku tukijiandaa kumtoa kikwete na makamba, good redio one kwa kuonyesha ukweli wa mambo siyo gazeti la habari leo linalokurupuka tu,
   
 3. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #3
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duuu, nambari one imekuwa ziro.... sasa wanatafuta nyia nyingine!!!! Uzuri watanzania tushajua janja yao, aibu kubwa kwa habari leo!!!! :ban:
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  Jan 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  :Cry: CCM!!!!
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Jan 16, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,934
  Likes Received: 12,188
  Trophy Points: 280
  Kuna watu hapa walikuwa wanaongea hadi povu mdomoni kwa kujifanya kuijua dini kuliko mashehe walioswalisha tukawaambia watakuja kuwa wapole siku si nyingi sasa bado polisi nao watasema tu.
   
 6. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #6
  Jan 16, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  dah,kweli siasa ni mchezo mchafu sana
   
 7. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #7
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Walitupa karata ya udini sasa imewageukia
   
 8. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #8
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Walitupa karata ya udini sasa imewageukia, damu ya mtu haimwagiki bure lazima ije kula kwao
   
 9. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #9
  Jan 16, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Walitupa karata ya udini sasa imewageukia, damu ya mtu haimwagiki bure lazima ije kula kwao, mkwere, makamba & co tunawasubiria ni swala la mda tuu you are going down, you have no place to go except down
   
 10. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #10
  Jan 16, 2011
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naomba cdm wanunue muda kwenye main stream waonyeshe mkanda wa maandamano ili dunia ione uhalisia cio ile propaganda ya polisi eti cdm walitaka kuvamia kituo bila silaha
   
 11. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #11
  Jan 16, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwanini mkuu? Mi nadhani siasa si mchezo mchafu bali kuna wanasiasa wachafu, na wengi wao ni CCM. Wanapenda kutumia uongo kupotosha umma, ukweli unapobainika wanaumbuka. ShAME UPON THEIR FACES!!
   
 12. kitungi

  kitungi Senior Member

  #12
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hii habari itawasumbua sana sisi "M"!!
   
 13. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  [​IMG]


  Kitungi habari zako?
   
 14. kitungi

  kitungi Senior Member

  #14
  Jan 17, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Calm Down
  I Know What It Looks Like,
  But It's Just An Apple!!!!
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  My son I know, you know that, I know is a mighty apple!
   
 16. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Rev. Masanilo umekosa maadili.
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  My broda! Kwanini nimekosa tena hayo maadili?
   
 18. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Brother, sidhani kama ni busara kuattach that image the way you did.
   
 19. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nasikitika hukunielewa! Hiyo ni avatar ya mh Kitungi.
   
 20. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  dirty mind!
   
Loading...