Mimi tofauti na maoni ya wengi nakuwa na wasi wasi na msimamo wa wachangiaji wengi hapa. Inaonekana wazi kabisa kuwa si wote wamelisoma na kulielewa Azimio la Arusha na hivyo kutojua kwa nini swala lake linaanza kuibuka hivi sasa. Wanachojaribu ni kulitafsiri na kulihukumu kwa kuangalia wanachodhani yangestahili kuitwa mafanikio yake. Matokeo yake wanashindwa kuelewa malengo na sababu za kupitishwa kwa Azimio la Zanzibar na athari za kitendo hicho kwa Azimio la Arusha na mustakabali wa taifa kwa jumla. Nashauri watu watafute muda walisome kwanza kabla ya kuchangia ili wakwepe kukurupuka kama anavyokurupuka Mwinyi hivi sasa - ni ushauri tu.
Tuliokuwapo viwanja vya Mnazi Moja mwaka 1967 tuliziona sura nyingi zilizojaa matumaini na pia sura chache zilizofadhaika na kujaa woga. Tulijua vita vimetangazwa - vita iliyowaweka wananchi wenye moyo wa kujenga taifa lao upande moja na wenye meno ya kuila taifa upande wa pili. Ninachoweza kusema ni kuwa ilikuwa vita ngumu hasa kwa upande moja kwani pamoja na kuwa wengi, hawakuwa na nyenzo kama wenzao waliotumia nguvu ya pesa. Hivyo mwaka 1991 ushindi ulipatikana kwa upande moja huko Zanzibar na jemadari aliyeongoza hivyo vita ni Al Haj Ali Hasan Mwinyi. Leo hii anatokea na kudai hakushinda, sasa waliotangaza ushindi ni akina nani ?
Nakubaliana kabisa na wewe mkuu. Sasa hivi kuna vacuum ya vision yetu sisi kama Taifa. Hatuna Azimio la Arusha na hatuna ubepari. Tuna wizi wa mali ya umma.- Mkuu una maana vita ilitayarishwa bila ya kuhakikisha kuwepo kwa nyezo za kuvifanikisha in advance au?
- Mimi ningeshauri kwamba wa-Tanzania tuachane na mambo ya kale tuanze kutafuta ya kutupeleka mbele maana hayoya zamani simply yalishindwa na wote sisi wananchi na taifa zima ni wakulaumiwa, sasa tutafakari na tutafute mbinu za kutupeleka mbele.
FMEs!
My take
There is nothing wrong kumpenda na kumuheshimu Nyerere , bila matusi n.k
Tatizo ni pale tunapotaka kuamini it was the only solution ya kutatua matatizo yetu, tatizo na kutokubali kulikuwa na makosa na AD inataka kuwa dini na siyo reality, tatizo ni kutokuwa na watu shupavu wa kulisimamia kwa vitendo.,Kuhubiri na kushawishi watu, AD ni ushawishi zaidi,
Hali ya uchumi alipoingia Alhaj ilikuwa mbaya kweli, lakini unapotaka kufanya chochote kuna vitu vya msingi , na vingine ni vile vinavyo imarisha vitu vya msingi, na niliwahi kuongea na mtu moja ambaye ni swahiba/rafiki/ndugu wa alhaj ambaye ni mtu wa system mpaka leo, yeye alilalamika rukhsa ya mwinyi ambayo haikuwa na taratibu, yaani mambo yanajiendea holela holela.Nimeuliza swali hilo hakuna aliyejibu , mtu aje na tangible proof kuwa jamani ehe! wakati wa AD mafaniko yalikuwa haya, na wakati wa Mwinyi tulidorora kiasi hiki!
AD was talks, na Mwinyi amejibu hizo talks na kusema hakuliua! we are living in the world of no talks! action ambazo zinaendana na hali halisi ya natural behaviour ya binadamu!
Ujamaa na kujitegemea (if it make sense) ili uwe effect basi lazima kiongozi awe dictator, kama Nyerere hakuwa na dictator basi maana yake alianzisha siasa ambayo asingeweza kuitekeleza bila kuwa dictator! which is again is another failure!
Somethings just happens, kutafutana uchawi wakati hatuwezi kupima mafanikio ya Azimio hili ni kudanganyana! Laws and order are far superior than AD au whatever!
Makoko wa Uk , kama upo kwa malikia basi utaona hoja za mwalimu zilivyo fanikiwa , mfano ukitaka kupeleka maji kwa watu na ukapunguza gharama si utawashauri wakae sehemu moja ili uweze kuwapatia hiyo bidhaa iwe shule hospitali, maduka, barabara nk na hapo ulipo utaona watu wana kaa kwenye estate, na kuwezesha kujenga miji kutokana na kuwepo kwa watu.Comp,
Azimio la Arusha Lilizinduliwa 1967 mpaka hapo inapodaiwa kuwa lilifutwa, ni hatua ipi ya kujitegemea liliwafikisha Watanzania, kati ya hizo ulizotaja?
Nyerere alielewa alipokosea na hata alipotoka alisema Yeye hakuwa malaika, tatizo ni pale tunapoacha vitu vya msingi, nalo ni la kujithamini kama tunaweza. Nakumbuka Alipokuwa PM sokoinne kuna mambo aliyo fanya chini ya uongozi wa Mwl ilikupunguza adha kwa watu Mfano kuanzishwa kwa Dala Dala, hata kipindi cha Salim Ahmed Salim kuna vitu alifanya na Mwalimu alikubali.Wamzz,
Kuna tatizo moja ambalo tunashindwa kulizingatia Azimio la Arusha ilikuwa ni Sera na Mawazo ya Mtu mmoja. Nae alitaka ahakikishe Linakubalika Hatakama alikubaliki, Linatekelezwa Hatakama Halitekelezeki. Mwl Aliamini na Ameondoka Duniani akiamini Hivyo kuwa Fikra zake ni sahihi siku zote hivyo hakuhitaji mchango/msaada wa Mawazo toka popote.
Wakati tunagutishwa "Zidumu Fikra sahihi za Mwenyekiti", Washauri wake wanadai kuwa "Mzee Haambiliki".Sidhani sera inayokwenda mrama isipokubali ushauri na kufanyiwa marekebisho ingeweza kufika au kumfikisha yeyote alipokusudia.
Mag3 kumbe ulikuwepo Mnazi Mmoja 1967, basi labda tulipigana vikumbo au tukionana tunaweza kukumbukana sura zetu.
Waberoya,
Ukisoma maelezo hayo juu, hasa yenye bold, naanza kuelewa kuwa unafahamu nini sisi wengine tunalilia. Ila kwa makusudi kabisa, unatafuta makosa ya AD na kuyatumia kuonyesha kuwa AD ni balaa ya Tanzania.
Hakuna anayesema THIS WAS ONLY. Narudia kusema, unafahamu nini sisi tunataka kusema ila unaPINDISHA kwa makusudi kabisa maelezo yetu ili tu kuonyesha kuwa tunafanya makosa makubwa kabisa.
Labda niandike kwa ufupi. Kuanzishwa kwa AD kulikuwa kumejaa makosa au nisema kulisaidia kwa wakati ule ila kabla JKN hajaondoka na hasa akifahamu kuwa tunaelekea kwenye vyama vingi (hili alisaidia lianzishwe Tanzania) kuna baadhi ya mambo ya AD alitakiwa kuyaingiza kwenye katiba ya nchi na yasiyofaa basi ayaaondolee mbali na yeye mwenyewe ALIUWE rasmi Azimio la Arusha. Nasema hivyo kwa sababu AD ilikuwa chini ya chama na nchi ilikuwa ni ya chama kimoja.
Wakaja wajanja wakanja wakaona hili ni tatizo kwao. Wakitumia njia mbalimbali na nina imani hata hao IMF na World Bank, wakaanza kulihujumu kidogokidogo kwa miaka mingi. Mwisho ikaoenekana kwa watu wengi (soma maelezo ya FMes hapo nyuma) kuwa AD inatajirisha watu wachache na kuwazuia wao. Ndipo wakamuweka sawa Mzee Mwinyi.
Mwinyi bila kufahamu/kwa kufahamu akauvaa mkenge na kwenda Zanzibar na kuliuwa kabisa AD.
Baada ya kuuwa AD rasmi, yale mabaya yote na mazuri ya AD yakawa yamekufa. Katika mazuri machache ya AD ilikuwa MIIKO YA VIONGOZI. AD ilikuwa na hili swala muhimu. Viongozi dunia nzima wana matatizo yaleyale ya kutaka kujitajirisha. Nchi za wenzetu huwa wanakwama kufanya hivyo kwa sababu ya miiko ya viongozi na kuwepo vyombo maalumu ambavyo vipo tayari kuwashughulikia mara wanapovunja hiyo miiko.
Kinachoendelea kwa sasa Tanzania ni vacuum ya MIIKO YA VIONGOZI. Kama Mwinyi angelivunja AD na kuichukua miiko ya viongozi na kuiingiza kwenye katiba ya Tanzania, naamini kuwa leo hii angelikuwa anaheshimika zaidi ya JKN. Baada ya miiko ya viongozi kuondolewa, leo hii viongozi wa Tanzania wanajifanyia chochote wanachokitaka bila ya kuogopa kuchukuliwa hatua yoyote.
Wizi wa EPA, Richmond, Deepgreen nk ni mifano michache ya viongozi kujisikia wako juu ya sheria. Kitendo cha waziri kwenda kuweka sahihi mikataba nje ya Tanzania na tena kwenye caffee inatia kinyaa.
Kikwete na ubovu wake, kama akirudisha miiko ya viongozi na kuweka chombo kinachojitegemea cha kulinda hiyo miiko, basi atakuwa ni shujaa wangu mkubwa. Ila hata miiko ikiwekwa na kuwepo chombo kama TAKURURU ambacho kinashughulikia vidagaa, basi ni kupoteza tu pesa.
Ndiyo maana wengine tunaamini kuwa kwa Tanzania inabidi aje kichaa ambaye risasi mbili tatu zitatembea kwa wale wote watakaokuwa wanataka kumpinga kwa vitendo. JKN hawakumpinga kwa maneno ila vitendo, wakammaliza na AD yake.
Nilikuwapo ndugu yangu, ni siku ambayo ni vigumu kuisahau kama ulikuwapo lakini rahisi kuikebehi kama ulikuwa hujazaliwa. Hamasa, mwamko na mtumaini ya Watanzania na hasa vijana wakati huo yaliweza kuutikisa ulimwengu. Nakumbuka heshima aliyopewa Mtanzania nje ya mipaka yetu kwa aliyebahatika kusafiri wakati huo, ni kubwa. Hofu ilitanda si kwa majirani tu bali hata kwa mashirika ya kitaifa - kote walijiuliza itakuwaje hii kitu ikifaulu. Hapana, hali hii isiruhusiwe katu na vibaraka wakapatikana humu humu nchini na wakatumiwa ipasavyo kuihujumu.
Kama kuna watu wananipa kichefu chefu, ni huyu Mwinyi. Angekuwa mtu makini siku alipoombwa kugombea Uraisi angeweza kabisa akasema, thanks but no thanks, hivi viatu siviwezi - siwezi kuvuka huu mto kwani sijui kuogelea. Lakini Mwinyi being what he is, akatumbukia majini akiikokota nchi ya heshima - matokeo yake sasa tunayaona na kuyashuhudia. Okay, kabla yake tuliitwa masikini, sawa tulikubali na kukataa kuburuzwa, naam si masikini jeuri ? Na sasa tuko wapi ? Wezi wa kutupwa na tunamwibia nani ? Sisi, watoto wetu na wajukuu zetu. Mwinyi akae kimya, period.
Haya maneno nimeyakubali kamili kamili mkuu. Hakuna nchi isiyo na dira. Sisi lazima tukubali kuwa tunaenda enda tu kwa ujanja ujanja tena kwa hasara yetu wenyewe maana sijui ipi ni siasa tunayoifuata.Waberoya ndani ya Katiba yetu imetamkwa siasa ya nchi yetu ni ya Ujamaa na Kujitegemea ambao practical application yake ni kuchangiana harusi, misiba na kuomba omba wafadhili na wahisani. Aidha viongozi wakiiba tunawatetea wasinyongwe na wananchi na tunawalinda. Just look at our national character as a nation it evolves around kupenda vitu vya dezo na ujanja ujanja uliojikita kwenye ujinga.
Waberoya ndani ya Katiba yetu imetamkwa siasa ya nchi yetu ni ya Ujamaa na Kujitegemea ambao practical application yake ni kuchangiana harusi, misiba na kuomba omba wafadhili na wahisani. Aidha viongozi wakiiba tunawatetea wasinyongwe na wananchi na tunawalinda. Just look at our national character as a nation it evolves around kupenda vitu vya dezo na ujanja ujanja uliojikita kwenye ujinga.
Mzee Mag3, naomba unisaidie hasa sisi tulikokuwa hatupo kipindi hicho; maswali yangu siyaamini sana.............
Waberora,
Azimio la Arusha liliweka miiko. Ila kwa vipi lilikataza kuiba, hicho kitu hakipo duniani.
Hata leo Tanzania ukiuwa unaweza kunyongwa kikatiba, ila hiyo sheria haizuii watu kuuwa. Sasa unaponiuliza hilo, sijui uma maana gani. Isije kuwa yale ya kuuliza pua iko wapi wakati mdomo unauona.
Sasa hivi hiyo miiko tu haipo. Sasa hata Yona na Mramba kuwashitaki na kushinda ili jamaa waende jela hicho kitu hakipo. Walau zamani mtu anaweza kushtakiwa na akafungwa au kufukuzwa kazi. Lowassa pamoja na kuvunja miiko, bado WALIMUOMBA aangalie kipi cha maana akifanye. Yes, aangalie na si ashtakiwe na kufukuzwa kazi na mwisho kufungwa. Hii ndiyo hali mbaya ya vacuum iliyotokea baada ya kuvunjwa kwa AD.
Kukaa chini na kuangalia tabia zenu hilo ni kupoteza muda. tabia zetu pote duniani ziko sawa kabisa. Ila wenzetu wanafuatilia sana sheria. Kama JKN angelifahamu hili na kujenga kitu kama FBI, CIA na Sherrif/POLISI basi ninaimani leo hii watu kama Rostam Azzi, Lowassa na akina Mramba wangelikuwa wafanyakazi bora wa Tanzania huku wakiiletea Tanzania faida kubwa. Siwezi kushangaa kuwa hawa watu walikuwa na moyo sana ila wakakatizwa tamaa na wale wengine wa zamani. Kama Kikwete aliona wanavyoiba wengine, leo hii kawa juu unafikiri yeye ataacha? Ila kuna chombo chochote kinafanya ULINZI na USALAMA wa rasilimali zetu?
Haijalishi AD au katiba au chochote kile wewe utakaa na kusema tukifanye. Tanzania inabidi tuwe na chombo cha kuwalinda viongozi. Wabunge tumeshaona haliwezekani. Kama tukiwa na FBI yetu na hawa jamaa hawafanyi mchezo (kumfunga paka kengele) basi mchezo utakuwa umeisha. Miiko iwepo na chombo maalumu kisimamie. Huu ndiyo mzizi wa fitina.
Kama kuna kiongozi hafai, basi sidhani kama atakwenda juu. Leo hii tunasikia Mrema wa TANROAD kaajiliwa kwa mlango wa nyuma. Boss mpya wa NHC kaajiriwa kwa mlango wa nyuma. Pesa kibao zimetumia kumchagua CEO na watu wanakuja kuajiri kivyao na hakuna kitu kinatokea kwa hawa Mawaziri. Sasa unategemea huyu boss wa NHC atakuwa kweli makini? Kwanza ataambiwa achote pesa aipe CCM na hatapinga kwani wamemuajiri kwa kutumia penseli. Wanamtisha kuwa ukileta ya kuleta, form one utafutwa.
Makoko,Sk mkuu,
Miiko ipi hiyo mnayoizungumzia??? Wakati Sheria na Hukumu zipo toka Enzi za Torati: USIUE USIIBE USIZINI USIMTAMANI MKE WA JIRANI YAKO nk. Na Hukumu ya Mwizi na Akatwe mkono na Mzinzi apigwe Mawe Mwuwaji Auwawe nk, pamoja na kuzilainisha pia zimetushinda kuzifuata.
Sasa tunasingizia miiko miiko miiko miiko, miiko gani zaidi ya hiyo; Mkapa kaiba, Lowasa kaiba, Chenge, Mramba na wote wanaojulikana na ushahidi upo sasa Azimio la Arusha lingesaidiaje? linahitajika la nini? Kwa kesi kama hizi wakati Sheria zipo Jeshi la polisi lipo Ofisi/Idara ya Mwendesha Mashtaka ipo sasa habari za FBI nk zajia nini?