Raelish
JF-Expert Member
- Jul 17, 2013
- 489
- 162
Hakuna kitu ambacho kinaweza kukuachia shida na dhiki duniani kama kifo. Nyota yangu ilianza kung'aa nikawa darasa la nne baada ya kupata wastani wa A katika mtihani wangu, nikiwa sina hata ndala miguuni, kaptura ya shule iliyochanika, shati kubwa chafu, dunia ikiwa inanicheka huku nikipata faraja kutoka kwa baba yangu na mama yangu.
Ni wazazi wangu waliokua wamezaa watoto wanne wakiwa wanategemea kilimo cha jembe la mkono ili kuendesha maisha, silaha yao kubwa ikiwa ni upendo kwa watoto wao na kuwapa matumaini kuwa Mungu lazima atukumbuke siku moja.
Mwaka 2001, kaka yangu wa pili, baada ya kumaliza elimu ya msingi na kufanikiwa kuchaguliwa kidato cha Kwanza , alishindwa kwenda kwa sababu alikosa ada, ndipo alipoamua kuaga rasmi nyumbani na kuelekea mjini.
Nilikuwa mdogo kipindi kile lakini niliweza kuhisi maumivu makali ndani ya moyo wake, "mdogo wangu Mungu amekujalia akili lakini amekunyima uwezo, sijui kama utafika mbali katika elimu yako ila usiache shule wala usikate tamaa, maana hatujui kesho itakuwaje".
Mbele ya wazazi wapendwa, mimi nikiwepo, aliaga rasmi asubuhi yake akawa ameondoka huku akiniaminisha kuwa yupo tayari akafanye anavyoweza kuhakiksha nasoma ili nikomboe familia. Nakumbuka nilimsindikiza hadi stendi nikamwacha pale huku akinipa tsh mia. Maisha yaliendelea; baada ya miaka mitatu nilikuwa darasa la saba.
Kaka yangu akiwa mjini, alipata kazi ya kuuza mbao kwa tajiri mmoja pale mjini, alikuwa anapata chochote ambacho kilisaidia kuendesha maisha yake. Kumbe alikuwa anakumbuka ahadi yake kwangu akawa anatunza kiasi cha pesa.
Mwaka 2004 nikawa darasa la saba nikafanikiwa kufahulu katika shule ya sekondari Kibaha. Kaka yangu aliposikia alifurahi sana, akawa amenitumia Tsh 120,000 na wazazi wakaongeza Tsh 40,000 nikawa nimefanikiwa kwenda kuanza kidato cha kwanza, kipindi kile headmaster ni S. M Kayenga.
Shule ilinipokea na kila mtu aliweza kuona wazi hali yangu duni, kutokana na umri wangu mdogo nikawa nashindwa kuhimili ile hali, mara nyingi machozi ndio yalikuwa faraja yangu. Nilisoma kwa miaka minne bila kurudi nyumbani na nilikuwa nabaki shuleni.
Shule ilikuwa na utaratibu wa kuwalipa wale waliokuwa wanabaki kwa makubaliano ya kufanya usafi katika mazingira ya shule wakati wote wa likizo hivyo kupitia hilo nikaweza kulipa ada ambayo ilikuwa Tsh 70,000 kwa mwaka.
Nilihitimu kidato cha nne na kufanikiwa kufaulu vizuri combination ya CBG, nikaenda kujiunga kidato cha tano katika shule moja ya mission chini ya msaada wa kaka yangu ambaye sasa angalau alikuwa na maisha mazuri kwa sababu aliamua kwenda Msumbiji kwenye mgodi na huko alifanikiwa sana.
Sijui nini kilitokea nikiwa form six mawasiliano na kaka yakawa yamekata kabisa, kwa kuwa nilikuwa mkubwa niliweza kumudu maisha. Kidato cha sita nilimaliza na sikufanya vizuri sana,
Pale nilikuwa nadaiwa ada hivyo sikuweza kutoka na cheti. Ndipo nilipoingia rasmi mtaani kupambana na maisha, baada ya miaka kama miwili nikawa nafundisha shule moja private kama form six leaver. Nikapata simu kutoka Msumbiji, ilikuwa ni sauti ya dada iliniambia kuwa kaka ni mgonjwa sana hivyo niwahi mpakani Newala nikampokee maana amewekwa kwenye lori moja la mizigo.
Sikujiuliza sana, nikawa nimeenda kwa boss wangu, akanipa pesa nikaanza safari kuelekea Newala, nilipofika Newala nikapokea simu nyingine iliyoniambia kuwa ndugu yako alishushwa hapa mpakani ila tumemuwahisha hospitali hivyo njoo hospitalini.
Nilipofika pale sikuamini nilichokiona; alikuwa ni braza wangu mpenzi, macho ameyafunika, mwili wote umeisha, nilishindwa kujizuia kulia kwa sauti ya uchungu sana. Ndiyo, ni uchungu uliokuwa unatoka ndani kabisa ya moyo wangu.
Baada ya siku chache alifariki, nililia sana nikaona kabisa mimi nimezaliwa kwa bahati mbaya, umri wangu mdogo yanayonikuta makubwa.
Basi tulizika. Muda wa wiki nzima nikawa nashinda kwenye kaburi nikiamini huenda anaweza akatoka ili niwahi kumshika mkono nimrudishe nyumbani, nikirudi kwenye kibarua changu.
Bosi nilimwomba anisaidie kunisomesha elimu ya chuo akakubali, mwaka jana kupitia NACTE nikaomba nikapata diploma ya medicine, yaani clinical officer. Nikajiunga na chuo mwaka jana mwezi wa kumi. Juzi nimepigiwa simu na yule mfadhili wangu kuwa anatakiwa kurudi kwao Ulaya.
Nimechanganyikiwa sana, nawaza labda angekuwepo kaka yangu angenisaidia. Machozi yamerudi tena, moyo wangu unazimia ndio maana nasema "sikulaumu wewe kifo ila namwombea kaka yangu apumzike salama". Mapenzi yake ya dhati yamebaki kuwa kwangu, namiss uwepo wake.
Kwanini dunia, nani alikulazimisha unspoken?? Mbona unanitesa hivi? Kweli walimwengu watalia na mimi?? Nani atanifuta machozi yangu? Nani atashiriki Nami kikombe hiki?
Naomba msaada kwa yeyote ambaye anaweza kunisaidia kwa namna yoyote.
Natanguliza shukrani za dhati.
=============

Mkuu Raelish,
Pole sana na matatizo, Mwenyezi Mungu akuwekee wepesi na upate nafuu haraka na kwa amani.
Naomba nichukue nafasi hii kwa kuomba radhi kwa kuchelewa kujibu, hasa kwa wale ambao walikuwa wamenishtua nihusike kwa namna moja ama nyingine. Nimeshawasiliana na Raelish kwa kutuma PM, ili atimize baadhi ya vielelezo ili iwe rahisi kujua ni msaada aina gani anahitaji na wa kiasi gani itusaidie sisi kama wanajamvi kukusanya kwa nguvu hiyo.
Nawashukuru na wale wote walio onyesha nia ya kutaka sana kusaidia. Mara baada ya kumaliza mawasiliano na Raelish nitatoa mrejesho mara moja ili tuendelee na nia ya kuwa msaada kwa kiasi fulani katika maisha yake. Maelezo zaidi yatakuja baada ya kujibiwa na Raelish. Asanteni.
Pamoja Sana!
=======
TAARIFA:
Uongozi wa JamiiForums umejiridhisha na kuafiki kwamba matatizo ya Raelish ni genuine. Hivyo basi, utaratibu wa kuchangia utafanyika kama ifuatavyo;
Kwa wale walioahidi msaada wa kifedha, na hata wasioahidi ila wameguswa na wangependa kushiriki kwenye hili, wanaweza kufanya hivyo kwa kutuma kiasi cha pesa kupitia M-PESA, Namba ya Simu: 0757 525 366 (Jina litakalotokea ni OBEDI MNZAVA).
Tunatanguliza shukrani za dhati kwa nyote mlioshiriki na mnaoendelea kushiriki katika zoezi hili.
- Majina ya walioahidi kuchangia mpaka sasa ni;
Julius Malema Jr Nyalotsi Mokoyo miss chagga Idimulwa Alinda Kipilipili Billie CLEMENCY Kitulo Rugaijamu dagii MTUSIASA rosebud Freeland Deogratius n niester
Wengine pia mnakaribishwa.
Uongozi wa JF unalisimamia jambo hili kwa karibu na kwa umakini sana mpaka mwisho wake. Na litakapofikia, basi mrejesho utaletwa hapa.
Asante.