Sikukuu zimeisha, Rais Magufuli tunakuomba uanze ziara

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Naandika hivi ni kwa sababu Mh Rais unapokuwa katika ziara zako hapo ndipo kero za wananchi huibuliwa na kutatuliwa.

Maana wengi wa wasaidizi wako ni kama hawana msaada kwa wananchi. Misafara yako inaposimama kila mahali hapo ndipo akina mama na wazee walioonewa na kudhulumiwa huwa unawasaidia.

Mfano yule mama kule Kahama aliwatoa machozi watu mume wake aligongwa na trafiki lakini hakuna msaada aliokuwa ameupata mpaka msafara wako uliposimama.

Pia ulipofanya ziara Butimba prison ulimsaidia Kulwa aliyebambikiwa kesi ya mauaji. Sasa tunakuomba umalize likizo maana sikukuu zimeisha ili wananchi waje waibue kero zao kila utapopita.

Pia hata Mh Kassim naye amekuwa kimya kiasi cha wateule ambao wamejisahau kujisahau zaidi.

Hivyo tunakuomba urudi uwanjani ili usaidie wanyonge. Kwa ujumla watu wanaona ma-DC na ma-RC hawatatui kero za wananchi mpaka waone kuna ziara yako au ya Waziri Mkuu.
 
Mnamchosha na mtamzeesha Tanzania One wetu
Anaehisi hawezi kazi apishe
 
Hakuna mfumo bora wa uongozi zaidi ya drama za kusimamishana mabarabarani eti kutatua kero!
Nchi ya RAIA zaidi ya 50milion matatizo ya RAIA wake yanatatuliwa na Rais kwa njia ya kusimama na TV kisha mtu ananyoosha kidole kujieleza? That's Madness!
 
Nafikiri raisi anaweza kufanya kazi hata angekuwa kwenye ndege. Raisi wa nchi ana wawakilishi wake kila mahali.
 
Back
Top Bottom