Rais Samia ameongea ukweli na kushauri vyema kuhusu viongozi kutambua mipaka yao kiuongozi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,338
9,766
Ndugu zangu Jana October 3/2022 mh Rais Samia alikuwa anawaapisha viongozi aliowateua katika mabadiliko madogo aliyoyafanya katika Balaza la mawaziri, Ambayo siku zote hulenga katika kuboresha utendaji na kuleta ufanisi kazini utakaokuwa na tija katika kuwatumikia na kuwahudumia wananchi.

Pili lazima ifahamike kuwa suala Hilo la kufanya mabadiliko madogo Ni Jambo la kawaida na siyo Mara ya kwanza kutokea na halitakuwa la mwisho kufanyika hapa nchini, lakini pia lazima ifahamike pia mtu kuondolewa katika uwaziri siyo kuwa amefanya jinai au ameharibu Sana au amefanya uhaini, Ndio maana mtu anaweza akatenguliwa Leo katika wizara hii halafu baada ya muda akaibukia na kurudishwa katika Wizara fulani, Ambayo mh Rais anaweza akaona kuwa mtu huyu atapaweza na kumudu vyema majukumu ya Wizara husika kutokana na taaluma yake au uzoefu wake,

Hivyo kuenguliwa katika uwaziri au uongozi mwingine wowote Ni Jambo la kawaida katika masuala ya kisiasa na kiuongozi, lakini pia lazima sote Tufahamu ya kuwa mh Rais Ni kiongozi anayepokea, kupata na kuwa na Taarifa zote za wateule wake ambazo zingine sisi wananchi wa kawaida hatuwezi kuzifahamu, hivyo tumuachie na Tumwamini Rais wetu katika suala Hilo la uteuzi na utenguzi na tubaki kutoa mawazo na ushauri tu hasa pale tumapomwona mtu fulani kutokana na Elimu yake na uzoefu wake anaweza akafanya vyema Sana na kutusaidia ikiwa atapata uteuzi katika nafasi fulani au kuhamishiwa eneo fulani kutoka mahali alipo, na hapa tukumbuke kuwa ushauri siyo lazima uchukuliwe na kufanyiwa kazi maana ushauri siyo shuruti au lazima

Katika hotuba yake Rais Samia amewashauri na kuwasihi viongozi kuzingatia urefu wao yaani mipaka yao ya kimamlaka, jambo ambalo nakubaliana nalo kabisa, Kama jambo hili lingekuwa linazingatiwa na viongozi wote naamini hata migogoro na mikwaruzano isingekuwa inajitokeza maofisini, kazi zingekuwa zinafanyika vyema kabisa.

Tusingekuwa tunasikia mivutano au migogoro ya Ma DED na Ma DC, au mawaziri na manaibu mawaziri, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu, Ma RC na ma DC, wakurugenzi wa halmashauri na madiwani, mawaziri na makatibu wakuu wao na wengine wengi tu, kazi zingefanyika kwa amani na upendo Sana, kusingekuwa na kutunishiana misuri, kusingekuwa na habari za kutambiana kuwa Mimi ni mteule wa Rais kwa hiyo huna Cha kuniambia, kusingekuwa na habari za Mimi naripoti kwa Rais pekee, maana kila mtu angefahamu na kujuwa kuwa mipaka yake inaishia mahali fulani na inapoishia ndipo mamlaka ya mwingine yanapoanzia

Kila kiongozi angepaswa kufahamu kuwa wote wapo kwa ajili ya kuwatumikia na kuwahudumia watanzania, kuwatatulia kero watanzania, kuwafuta machozi wanao Lia, kuwapa faraja na matumaini waliokata tamaa, kutoa haki kwa waliozulumiwa na kusikiliza wenye shida, Kama viongozi wote wangeshirikiana vizuri pengine hata mabango ya malalamiko yasingekuwa yanaonekana Rais au makamu wa Rais au Waziri mkuu akifanya ziara mahali fulani

Sasa Leo unakuta mtu Ni Waziri lakini anaanza kujiona na kujifananisha na Rais wakati hata kwenye kura za maoni tu za ubunge ilikuwa Ni shida tupu, unakuta mtu Ni mwandishi wa Hotuba za Rais lakini anaanza kuhisi Naye Ni Rais na anataka watu wajuwe kuwa naye Ni Rais mdogo, unakuta mtu katumwa kumwakilisha Rais mahali fulani akirudi anaanza kupandisha mabega kuhisi kuwa anaweza kuwa Rais kwa kuwa tu alishangiliwa na kupigiwa makofi Sana bila kujuwa kuwa ni kwa kuwa tu alikuwa amemuwakilisha Rais na yupo pale kwa niaba ya Rais wa nchi na siyo yeye aliye vaa suti,

Viongozi lazima wajifunze kuheshimiana, kuheshimu mamlaka iliyo juu yao, kuheshimu viongozi wenzao, kuzingatia mipaka yao, waache kuhujumiana na kuhujumu juhudi za wenzao

Lakini pia viongozi lazima wajuwe kuwa uongozi unatoka kwa Mwenyezi Mungu, hivyo Kama unatamani nafasi fulani huwezi ukaipata kwa kumhujumu mtu, maana unaweza ukafanya hujuma na fitina na usiipate wewe hiyo nafasi akaja akaipata na kuitwaa mtu mwingine kabisaaa ambaye hata akilini mwako hakuwepo kabisa, maana MUngu Humuinua mja wake yoyote yule kwa hiyo unaweza ukajikuta kwa Tamaa zako za uongozi wewe siyo mmoja wake uliye katika list yake

Viongozi Fanyeni Sana kazi kwa kujituma na maarifa kutuhudumia hasa sisi vijana tunao pambana huku mitaani, Tambueni huo uongozi mmepewa na Mungu, jiulizeni Ni wangapi wenye sifa na hawajapata bahati ya kuwa kwenye Nafasi mlizo nazo? Jiulizeni mlisoma na wangapi lakini Hadi leo wanahangaika huku na kule na maisha? Jiulizeni wangapi wapo tayari kufanya kazi hata kwa kukesha lakini hawajapata nafasi? Jiulizeni Kuna vijana wangapi mitaani wanaoweza kufanya kazi hata kwa kulipwa posho ya elfu mbili kwa siku lakini bado hawapati?

Heshimuni na kuridhika na nafasi mlizopewa na mwenyezi Mungu, Toshekeni na vipato vyenu, Fanyeni kazi ndizo ziwapandishe vyeo na siyo majungu, majungu yanaweza kuwapandisha Ila hayaweza kuwaacha juu, utendaji kazi uliotukuka ndio pekee unaoweza wafanya mkawa kileleni muda wote,Mtangulizeni mwenyezi Mungu kwa kila Jambo na kwa kila maamuzi mfanyayo kwa maslahi ya Taifa letu

Kwa niaba ya vijana wenzangu Nawaombeni mfanye kazi Sana kwa ajili yetu sisi ambao Ni kundi kubwa Sana tuliopo hapa nchini, Msituone Ni wazembe Bali mjuwe tu kuwa kupata Ni Majaliwa ya Mwenyezi Mungu, Aliyekupa wewe ndiye kaninyima hicho ulichonaacho au kunisubilisha mimi na yule, Mungu ametuumba kwa makusudi maalumu, Tumieni nafasi zenu kutimiza makusudi ya Mungu kututumikia,

Kazi iendeleee ,mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Hakuna pointi za maana katika gazeti hili!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom