Madame S
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 17,190
- 34,526
RIWAYA: SIKUJUA UNGENISALITI MPENZI (1)
MTUNZI: JOSEPH SHALUWA
SIMU: 0762 458590
EMAIL: joeshaluwa@gmail.com
FACEBOOK: Joseph Shaluwa
INSTAGRAM: josephshaluwa
*****
HALI ya hewa ilikuwa ya baridi sana asubuhi hiyo, mvua za rasharasha ziliendelea kunyesha na hapakuwa na dalili ya kukatika! Kwa mji wa kibiashara kama Dar es Salaam, mvua hizo zilikuwa kero kubwa sana kwa wakazi wake.
Ziliharibu kila kitu, wengi walisikika wakilaumu kwanini ilinyesha mjini badala ya Bagamoyo! Ni mvua ambayo ilikesha usiku kucha ikinyesha hadi asubuhi hiyo bila kukoma. Mavazi makuu sasa yakabadilika, yakawa ni makoti, masweta na majaketi!
Mvua ilikuwa kero!
Lakini kwa wenye nazo, haikuwa kero kubwa sana, kwani waliamua kupumzika majumbani mwao wakifurahia fedha na mali walizonazo. Lakini kuna ambao walizidishiwa zaidi maumivu na mvua hizo; wagonjwa waliolazwa katika hospitali mbalimbali.
Ndani ya wodi ya majeruhi, katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam, hali haikuwa shwari kwa kijana huyu! Kwa mwonekano wake, alikuwa anavutia sana. Ana macho makubwa meupe, yenye mboni nyeusi. Mpangilio wa nyusi zake ndiyo unaowachanganya wanawake wengi. Kifua chake cha mazoezi ni kati ya vitu vinavyozidisha mwonekano wake wa kimahaba.
Hakuna nguo ambayo anaitia mwilini inamkataa. Kila anachovaa anapendeza sana, huyu ni Bruno. Utanashati wake, mvuto wake wa kimahaba, uchangamfu na kila kitu, vyote vimepotea! Sasa Bruno amekuwa mpya! Amebadilika kwa kila kitu.
Hana tabasamu tena!
Hana furaha tena!
Maisha yake sasa yametawaliwa na huzuni na hofu tupu. Amelala kitandani akionekana kuwa na mawazo na kukata tamaa kabisa. Hana tumaini tena, kila kitu kimeshaharibika. Macho yake yamezingirwa na machozi, anaonekana hana amani wala matumaini ya kuishi muda mrefu baada ya pale.
“Mimi ni mzoga tu,” alijikuta akitamka kwa sauti huku mvua ya machozi ikianza kunyesha machoni mwake.
Msichana mrembo aliyekuwa akipita jirani yake, aliumizwa sana na machozi yake; akajua lazima alikuwa na jambo zito lililokuwa likimtatiza. Akapiga hatua za taratibu, macho yake yakiwa yanamwangalia sawia Bruno.
“Pole!” Akatamka msichana huyo kwa sauti ya chini, lakini kwa haraka kidogo.
“Nashukuru sana!”
“Pole utapona tu!”
“Ahsante sana.”
“Naitwa dada Vanessa, sijui wewe!”
“Bruno.”
“Pole sana Bruno, Mungu atakupa afya njema. Jipe moyo!”
“Ahsante sana!”
“Umepatwa na nini?”
“Ajali, nimepoteza mguu mmoja dada yangu!”
“Masikini pole sana.”
“Nashukuru.”
“Mimi pia nina mgonjwa wangu, mjomba wangu amelazwa hapa. Ndiyo nimetoka kumwangalia!” Akasema Vanessa.
“Pole sana, anaendeleaje sasa?”
“Ana nafuu kidogo, anaweza kuruhusiwa kesho kama siyo kesho kutwa.”
“Pole sana dada yangu!”
“Usijali, wewe ndiyo unatakiwa kupewa pole nyingi zaidi kutokana na matatizo uliyoyapata.”
“Nashukuru kwa wema wako.”
“Usijali...samahani, kuna jambo nataka kukuuliza...sijui utaniruhusu?”
“Uliza tu!”
“Kuna mtu anayekuja kukuangalia hapa hospitalini?”
“Unamaanisha nini?” Bruno akauliza angali macho yake ameyakaza usoni mwa Vanessa.
“Namaanisha mtu wa kukuletea huduma muhimu, mathalani chakula na mambo mengine!”
Lilikuwa swali baya kwa Bruno, swali lililotibua mambo yaliyojificha ndani ya moyo wake! Vanessa akashindwa kuelewa kwamba swali lile lilikuwa sawa na mwiba wa samaki ndani ya moyo wake!
Ghafla, macho ya Bruno yakalowana!
Mvua nyingine ya machozi ikaanza kumwagika machoni mwake, yakafunika kope zake...aliumia sana moyoni. Hakupenda kabisa lile swali.
Vanessa hakuyapenda machozi ya Bruno, kwa kumtizama tu, akafahamu kwamba, lazima alikuwa na kitu kingine kinachomwumiza zaidi. Bruno akazidi kulia, Vanessa akaketi kitandani kisha akatoa leso yake na kumfuta machozi.
“Samahani sana Bruno kama nimekukosea...” Vanessa akamwambia Bruno kwa sauti tulivu sana.
“Hapana dada, hakuna kitu!”
“Lakini umeanza kulia baada ya kukuliza kama kuna mtu anayekuja kukuangalia...samahani sana kama nimekukosea, siyo dhamira yangu!”
Bruno akazidi kulia.
“Nyamaza tafadhali, wewe ni mwanaume, hakuna tatizo kubwa kwa mwanaume, jikaze na utulize moyo wako.”
“Sawa, nimekuelewa...” Bruno akasema akijitajidi kunyamaza.
“Yaani Tunu?!!!” Hatimaye neno hilo likamtoka Bruno kinywani mwake.
“Tunu? Ndiyo nani?”
“Ni habari ndefu sana dada’ngu, siwezi kuzungumza kitu kwasasa, lakini fahamu hakuna mapenzi ya kweli duniani!” Bruno akamwambia Vanessa ambaye alionekana kushtuka sana.
“Hakuna mapenzi ya kweli, kivipi Bruno?”
“Fahamu tu, kwamba hakuna mapenzi ya kweli duniani!” Bruno akasema akianza kulia tena.
“Kwani hayo mapenzi yana uhusiano wowote na hii hali uliyonayo sasa?”
“Tena kwa asilimia mia moja!”
“Kivipi?”
“Siwezi kuongea chochote sasa hivi, sitaki kujiumiza zaidi ya hapa, nahitaji muda wa kupumzika zaidi, samahani kama nimekuudhi, lakini siku tukionana kwa majaliwa ya Mungu, nitakusimulia kisa kizima!”
“Sawa. Sasa unaweza kujibu swali langu?”
“Uliuliza nini vile?”
“Kama kuna mtu anayekuja kukuangalia na kukupa mahitaji yote ya muhimu?!”
“Kifupi hakuna!” Bruno akajibu baada ya kujikaza sana.
“Pole sana, kama hutajali, naomba kuanzia sasa nianze kukuangalia, sijui utaniruhusu?” Macho ya Vanessa yalikuwa ya huruma sana wakati akizungumza maneno hayo.
Bruno hakujibu!
Alibaki akimwangalia Vanessa.
“Tafadhali naomba unikubalie, usikatae Bruno nakuomba sana.”
Bado hakujibu!
Ghafla matone ya machozi yakaanza kumiminika tena machoni mwake. Ikawa machozi ni kitu cha kawaida kwa kijana huyu mtanashati. Kila kitu analia! Kila swali analoulizwa jibu lake ni machozi!
Machozi!
Machozi!
Machozi!
Vanessa akaogopa sana, akashindwa kuelewa ni kwanini kila anapomwambia kitu lazima alie! Akilini mwake kukajengeka kwamba lazima alikuwa na matatizo makubwa sana.
Ni kweli siku zote alikuwa mtu wa kusaidia watu, moyo wake ulikuwa wa huruma sana, hakupenda kumwona mtu akiwa katika hali ya shida na matatizo halafu amwache, kama anaweza kumsaidia alifanya hivyo.
Kwa kijana huyu aliyelala hoi kitandani, akionekana kukosa faraja kabisa, akionekana kukata tamaa ya maisha kabisa. Akionekana kupoteza hamu ya kuishi.
Aliyepoteza dira!
Ambaye havutii kwa chochote!
Hatamaniki kwa lolote!
Mlemavu!
Moyo wake ulikuwa na zaidi ya huruma, alishawishika kwa kiasi kikubwa sana kumsaidia, alishindwa kuelewa ni kwanini alijikuta akihisi hali hiyo, lakini moyo wake ulishaamua na alikuwa tayari kumsaidia kwa namna yoyote na kwa gharama yoyote.
“Tulia Bruno, lazima ujikubali kwanza jinsi ulivyo. Najua una mawazo mengi sana lakini unatakiwa kujitahidi uyaondoe, kwani hayatakusaidia kitu.
“Nahisi unavyoumia, naona unavyoteseka. Najua...nafahamu utakuwa na maumivu mengi sana kwa wakati mmoja. Nahisi unavyoungua na moto, lakini hayo yote ni sehemu ya maisha.
“Kumbuka matatizo hayakimbiwi Bruno, matatizo yanakabiliwa. Yanatatuliwa. Hayakimbiwi. Kwanza huwezi kuyakimbia. Utakimbia mpaka wapi? Utajificha wapi? Utalia mpaka lini? Nyamaza tafadhali...” sauti ya Vanessa ilikuwa ya kusihi kuliko kawaida.
Ilikuwa sawa na msumari wa moto ambao uliingia moyoni mwa Bruno kabla haujapoa vyema. Maumivu juu ya maumivu. Vanessa hakujua kinachomliza Bruno. Hakulia kwa sababu ya maumivu na mateso pekee.
Hakulia kwasababu sasa alishakuwa mlemavu. Alilia kwa sababu nyingine zaidi. Sababu kubwa kuliko kawaida, kubwa ingawa kwa mtu mwingine ingeweza kuonekana ndogo!
Mapenzi...
Hiyo ndiyo sababu kubwa iliyomfanya kila wakati awe analia. Akajuta kuyafahamu mapenzi, akajuta kumfahamu mpenzi wake aliyesababisha awe katika hali ile.