Siku za Shibuda ndani ya CHADEMA zahesabika

Siku za Shibuda ndani ya CHADEMA zahesabika

attachment.php


Huyu nae anamuwakilisha nani?

Wananchi wa jimbo la Hai
 
Kifo kinapomfika mja ujanja wote hupotea na kuwa zebwe,halikadhalika mbwa aki sense harufu ya Chatu hujipeleka mwenyewe kutafunwa,kwa mantiki hiyo basi kifo cha CCM haitaji elimu ya chuo kikuu kubaini.Na kwa kuwa Shibuda ni mamlukuki na hajawahi ku declare kuwa ameacha kazi yake ndani ya serikali inabidi tumuelewe na tumuogope kama ukoma ila kwa kuwa CDM ni mtu kichwa hawana muda wa kupambana na adui ambaye udhaifu wake na silaha zake haziwezi kumdhuru hata inzi




Ule ni mkutano wa moja ya chama kikongwe na kikubwa barani Afrika; walikuwepo wanadiplomasia kutoka nchi kadhaa; Dr Slaa hawezi mikutano kama ile amezoea kusimama kwenye majukwaa kusema uzushi na uwongo; game ya Kizota kubwa ni wachezaji mahiri wenye viwango vya kina Lionel Messi; cristiano Leornado, Ibrahimovic tu wenye uwezo wa kusimama kwenye mikutano ile na kusema maneno ya hekim; Dr. Slaa kiwango chake ni Mrisho Ngassa hapawezi!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Wanasheria wa chadema wako katika hatua ya mwisho kabisa kuandaa document za kumfukuza uanachama shibuda cdm, wakati wowote kuanzia leo na jumatatu atakuwa tayari amefukuzwa cdm,

kinachomwondoa cdm kwa uhakika zaidi ni ile ya kujialika kwenye mkutano mkuu wa wa nane wa ccm na matamko aliyotoa ambayo yamekera kambi zima ya upinzania


kamati kuu ya cdm itakutana wkato wowote kuhakikisha kuwa inamfukuza huyu msaliti. Kiti cha ubunge kitakuwa wazi na cdm wako tayari kwa lolote kuliko kuwa na mtu kama huyu.

Source: Wanasheria makini wa cdm
 
Ni bora wangeendelea kumdharau kama walivyofanya siku za nyuma!
 
Hivi kwa nini unamtaja sana Messi na kuacha kumtaja ULIYEMDHAMIRIA? Huu ni ujinga DHAHIRI, Messi na mchezaji soka na Shibuda ni mwanasiasa vitu viwili TOFAUTI KABISA.
Kuna ubaya jirani kupewa sifa anazostahili? Hebu funguka alichosema Messi wapi kakosea?Uliishasikia Messi akichezea Real Madrid japo kwa mazoezi???????????????

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Hivi kwa nini unamtaja sana Messi na kuacha kumtaja ULIYEMDHAMIRIA? Huu ni ujinga DHAHIRI, Messi na mchezaji soka na Shibuda ni mwanasiasa vitu viwili TOFAUTI KABISA.

Jacobus

Jibu hoja kinachosemwa umekielewa; John Shibuda aka Messi amekosea wapi?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hii thread iliwekwa jana hapa lakini imepotea. Wanasheria wa chadema wako hatua za mwisho za kuandaa makabrasha ya kumtimua rasmi shibuda toka cdm, hii imechochewa hasa na yeye kuvamia mkutano wa 8 wa ccm akijifanya kuiwakilisha cdm, bila cdm kumtuma. Hotuba aliyotoa shibuda ndo haswaa imemfukuza kwenye chama, vyama vyote vya upinzani vimechukizwa mno na matamshi ya shibuda kuwa ccm ni dawa ya wapinzani, na kuwataka ccm kujibu mapigo y aupinzani.
 
shibuda ni ndumilakuwili,wacha afukuzwe akatafute mahali pengine pa kujiegesha..pu..mb..av zake.
 
ni kweli inahitajika busara kidogo tu kummaliza huku kukiwa na matayarisho mbadala jimboni kwake, cdm wasisubiri 2015 bali wanachotakiwa ni kuanza kumpekecha taratiiiibu kote alikoshika ili akidondoka basi asinyanyuke tena, ccm kwenyewe hawamtaki kwani wanamjua alivyo kinyonga ndumila kuwili, mwanzoni shibuda alivyokuwa anahangaika akiwa ndani ya ccm kugombea nafasi mbalimbali na kuzikosa mie nilikuwa namhurumia sana kumbe ilikuwa haki yake,

shibunda hana faida na chama wala wapiga kura wake bali yeye huwaza ntakunywa pombe na nani ndani ya chama au ntakunywa pombe na mpiga kura yupi na sio kuwazia matatizo ya wapiga kura wake na ndio maana akakomalia posho bungeni utafikiri kitu posho ni mama yake.
mfukuzie mbali huyu mtu,ni dhahiri kuwa athari za kuwa naye ni kubwa mno kuliko athari za kumtoa,afukuzwe mapema ili aanze kuwasaidia magamba katika propoganda,2015 ni mbali sana ,mkimtoa mapema utakuwepo muda wa kutosha kurekebisha madhara yatakayojitokeza maswa na ku-identify potential candidate,pia itawapa muda wa kutosha kupima na kutathmini propoganda zake dhidi ya upinzani na kujipanga kupangua hoja na mashairi yake kabla ya 2015.mbowe na slaa ,please act fast and remove this rubbish
 
Ni afadhari uwe na jeshi lenye watu watano kuliko unakuwa na jeshi la watu kumi alf wanakuwa na akili za shibuda ni kupoteza mda na mwisho wa siku ni kushindwa vibaya kwa jeshi lako hapa dawa ni kufukuza tu huyu mzee wa mipasho
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kimechoshwa na kauli tata za Shibuda na siku zake zinahesabika ndani ya chama.

Hayo yanesemwa kwa nyakati tofauti katika mikutano ya chama chao mikoani walipoulizwa na wanananchi. Kati ya walionyeshwa kuchoshwa na kauli za Shibuda ni Tundu Lissu na Mbowe

Source: Mtanzania


Shibuda ni jembe la chadema ni kama messi wa cdm, hana mpinzani uwanjani na anafanya atakalo na hakuna wakumzuia, hili twaliita jembe
 
Thubutuu...

Juzi alinguruma Dodoma, hili ni jembe kweli kweli hata likienda TPP Maendeleo linapata ubunge.
 
Back
Top Bottom