Siku za Shibuda ndani ya CHADEMA zahesabika

Siku za Shibuda ndani ya CHADEMA zahesabika

Habari,,,
shukrani za pekee ziende kwa yule anaetupa pumzi na uzima hadi muda huu,,

Humu ndani wengi wetu tunajificha nyuma ya id's na kuzungumza yaliyo mema,na wengne kwa makusudi yao wanayazungumza yaliyo mabaya,,

Mimi nazungumza yaliyo mema hasa kwa watu wenzangu wema ninaojifunza mema kutoka kwao kwa kila siku ya uwepo wangu humu jamvini (JF - home of great thinkers),,

Shibuda kama ninaongea uongo njoo ukanushe ndugu yangu,,

ilikua namna kama ifuatavyo,,

Shibuda vs viongozi wa CHADEMA

Shiduda vs Mbowe

Mh. Mbowe najua wewe unae mtu wako uliempgia chapuo na ni girlfriend wako hadi akapata ubunge wa viti maalum,,hilo tumeliona na tumeliridhia,,

Shibuda vs Slaa,,

Mh. Slaa wewe tunafahamu ya kwamba unae mkeo humu ndani ya chama ambae kwa sasa mmetalikiana,ila ulihakikisha na kupigana kidete hadi mkeo akafanikiwa kupata ubunge wa viti maalum,tumeliona na tumelikubali hilo kwa maslahi ya chama,,

Shibuda vs Lissu

Mh Tundu Lissu,,wewe humu ndani una ndugu yako,tena wa damu,katika harakati za kujenga na kuimarisha chama ulihakikisha unapigana usiku na mchana kuhakikisha ndugu yako anapata nafasi ya uongozi na uwakilishi ili kupeleka gurudumu la chama hiki mbele,tumeliona na kuliafiki hilo kwa maslahi ya chama na umma

Shibuda vs Ndesamburo

Mh. Ndesa, wewe humu ndani tunajua una damu yako pia,ambayo kwa udi na uvumba ulipigana kuhakikisha nayeye anaambulia chochote katika cake hii iliyo Mbele yetu,,anaitwa Lucy Owenya,na ni mbunge wa viti maalum,tumeliona na kulikubali hilo kwa maslahi ya chama.

Shibuda vs Mzee Mtei

mzee Mtei,tunajua na tunafaham mahusiano ya kishemeji yaliyopo baina yako na Mh Mbowe,,

Hatuna wasi wasi na uchapakazi na weledi bora kuiongozi wa Mh Mbowe
na hii ilitokana nawewe kumpa nafas na imani kubwa juu yake had leo tunanufaika na maamuzi yako yaliyotukuka katika hilo mzee wetu,,

Sasa mimi kama Shibuda, ambae ni mwanachama na mbunge wa chama hiki,niliethubutu kuwahama mafisadi wa CCM,wafanyaji magendo wa CCM,waua tembo CCM,wahujum uchumi CCM,wafichaji wakuu wa pesa zetu Uswiss,,ninaethubutu kuwa mstari wa mbele wa kuiweka CHADEMA madarakani 2015.Mimi kama Shibuda na mimi leo nataka,namimi leo kama Shibuda nataka,,

mimi shibuda nina dada yangu nataka kama vile mlivofanya nyinyi namimi pia nataka apewe ubunge wa viti maalumu kupitia kule maswa,,sasa naleta rasmi ombi langu ndani ya chama dada yangu yule ni material na anafaa kuwa mbunge wa viti maalum,naomba afikiriwe kupewa nafasi hiyo kama walivopewa kipaombele wengine katika chama hiki,,

naomba kwa heshima na taadhima apewe,,na sipewe kwanini??au kwa kuwa yeye si mchaga??

Naomba dada yangu na mimi apewe nafasi hiyo kwa maslahi ya chama na umma kwa ujumla,,

ombi langu lisipofanyiwa kazi na kupewa kipaombele mtamjua Shibuda ni nani...!!

Shibuda kama unalo la kukanusha katika hilo tokezea uje ukanushe,,lakini haya ndiyo hasa yanayojiri ndani kwa ndani,,na hadi kuyapata inakubidi uwe mtu wa sampuli ya kipekee kidogo,,

sasa hadi lini viongozi wa CHADEMA mtaendelea kumvumilia ndugu John Shibuda ambae mimi namchukila kama ni pandikzi la CCM? ni hadi lini mtaendelea kumkumbatia wakati anakiharibu chama?

2015 iko karibu sana,tunahitaji kujenga chama,watu kama Shibuda hawatufai,,

siku njema.
 
Viti maalumu ni janga kitaifa nasema tena si upinzani wala ccm inabidi vifutwe vimekaa kubeba watu haviangalii vigezo vya uongozi na utendaji bora.

Hivi kwanini kuna wabunge wa viti maalumu kwa vipindi vitatu bado wako bungeni kama viti maalumu hawawezi gombea majimbo kwa wenzao kina mdee,kilango na wakimama wengine wao ni kupitia kapu la viti maalamu.

Ndo matatizo tunayo yaona leo watu watakuja na madata hapa viti maalumu mchakato ulienda wazi hakuna chochote hivi viti maalumu ni janga kwa kweli.

Namaliza kusema viti maalumu vifutwe tuunde mfumo wa kuwatengea kina mama majimbo yao ambao watapambana wenyewe kwa wenyewe sio huu upuuzi.
 
hili galasa Shibuda wiki iliyopita nililiona pale nbc posta limewakusanya washikaji kama watano linabwabwaja,nikaamua kupita kimya kimya...he knows his position come 2015,.

Katika aliyoongea kuna mengine yana ukweli lakini ameharibu hapo anaposema au kwa vile dada yangu sio mchaga?

Hivi chanzo cha habari ni kipi?
 
hili galasa shibuda wiki iliyopita nililiona pale nbc posta limewakusanya washikaji kama watano linabwabwaja,nikaamua kupita kimya kimya...he knows his position come 2015,.katika aliyoongea kuna mengine yana ukweli lakini ameharibu hapo anaposema au kwa vile dada yangu sio mchaga?hvi chanzo cha habari ni kipi?



ulikosea hapo ulipomkukuta anabwabwaja ungesimama tuh na kumsikiliza mbunge wako,,

katika watu watano,hukumuona mmoja kati yao ni mweupe kavaa shati la blue na trouser jeusi na mawani??

Kama utakua na kumbu kumbu that man is big show himself..
 
Tatizo letu watanzania ni zaidi ya vyama vya siasa.tatizo letu ni kukosekana kwa uadilifu na kutotumia akili ipasavyo.tatizo letu ni kila mtu kufikiri katika upeo wa kujinufaisha yeye na ndugu zake badala ya kujenga taifa kwa ujumla.lakni kwa kuwa tunataka tuonekane wema;kila mtu anadai mimi nataka niwasaidie watanzania,chama changu ndo bora zaidi ya vingine na kadhalika kumbe hana lolote bali ni msaka tonge tu.kwa kuwa viongozi wa chadema wana akili na wanayaona haya na hawachukui hatua lazma wana sababu ya msingi ya kumlinda shibuda.nani anayeweza kuijua?
 
ulikosea hapo ulipomkukuta anabwabwaja ungesimama tuh na kumsikiliza mbunge wako,,

katika watu watano,hukumuona mmoja kati yao ni mweupe kavaa shati la blue na trouser jeusi na mawani??

Kama utakua na kumbu kumbu that man is big show himself..

kumbe mkuu ulikuwepo pale?nina aleji na galasa lile!!!natumai ulilipa za uso..infact nilikuwa na haraka zangu angekuwa mnyika ningesimama na kupata madini
 
Ndani ya CDM ningempata mtu aliyebebwa hata akawa kwenye hivyo wanavyoita special seat ningefurahi sana, i mean kama kuna mtu anaonekana kabisa hakustahili butu yupo huko, ningefurahi sana cause kama kumbukumbu zangu zitakua sahihi, ni CDM pekee waliotoa sifa za atakae chaguliwa kwenye hivi viti na watu pekee waliotoa majibu mara baada ya malalamiko, sikusikia CUF, magamba n.k (sisemi nao hawakutoa tathimini na sifa, nimesema, sikusikia)
 
ndani ya cdm ningempata mtu aliyebebwa hata akawa kwenye hivyo wanavyoita special seat ningefurahi sana, i mean kama kuna mtu anaonekana kabisa hakustahili butu yupo huko, ningefurahi sana cause kama kumbukumbu zangu zitakua sahihi, ni cdm pekee waliotoa sifa za atakae chaguliwa kwenye hivi viti na watu pekee waliotoa majibu mara baada ya malalamiko, sikusikia cuf, magamba n.k (sisemi nao hawakutoa tathimini na sifa, nimesema, sikusikia)


uko sahihi,kila mtu kwenye nafasi iliyopo yupo smart,sasa malalamiko ya shibuda yana msingi gani?
Je viongozi wa cdm wanatambua athari yake kwa watu wanaomeza taarifa zenye utata kama hizi kama zilivo pasi na kuzipima??
 
Shibuda ni sawa na tone la maji ndani ya Bahari, siku zake zinahesabika
 
Chadema walidandia lori kwa mbele, lori hilo linawakaanga sasa..! Pambana Shibuda mpaka umalize kazi uliyotumwa na JK
 
kumbe jeikei ndie aliemtuma eeeh??

Sasa salam zitarud kwa mtumaji
Vita ni vita mura..! Unakuja mujini na jembe unataka kurima rami? Mujini watu wanakuja na vyeti..! Hata lile jembe la Mwanza, yaani mstahiki meya ndugu Matata ni kazi ya JK na bado list ni ndefu. lengo ni kuifanya chadema ifanane na cuf by 2015
 
Vita ni vita mura..! Unakuja mujini na jembe unataka kurima rami? Mujini watu wanakuja na vyeti..! Hata lile jembe la Mwanza, yaani mstahiki meya ndugu Matata ni kazi ya JK na bado list ni ndefu. lengo ni kuifanya chadema ifanane na cuf by 2015


NIGHTMARE HIZI,POLE SANA
:blah::blah::blah:
 
Back
Top Bottom