Siku za Hussein Bashe ndani ya CCM zinahesabika!

Siku za Hussein Bashe ndani ya CCM zinahesabika!

Usichokijua ni kwamba wabunge wote vijana wakiwemo kina nape ni vigumu kushinda uchaguzi ujao kama watabaki ccm ila wakihama wanao uhakika wa kushinda.Muda utaongea ntakwambia kwa nin
 
Kwa umri wake Bashe ni aibu kubwa sana kuwa mwanachama wa ccm
 
Ukweli ni jambo zuri sana kulisema, lakini uzalendo ni kitu bora zaidi kuliko kitu chochote kile.

Hussein Bashe wewe uko ndani ya CCM na ajabu wewe unaongoza kwa kuiponda CCM kuliko hata ambavyo unaviponda vyama vya upinzani. Katika siasa tabia kama hii haikubaliki hata kidogo.

Wana CCM tumekuwa tukikufuatilia kwa karibu sana, na matamko yako, yanaonesha wazi kabisa wewe siyo mzalendo kwa chama chako kilichokulea mpaka kukufikisha hapo ulipofika.

Inawezekana madai yako yakawa na ukweli ama la; lakini namna unavyoyawasilisha na mahali unapoyawasilisha siyo sahihi hata kidogo. Sidhani kama Mwenyekiti ataendelea kukuvumilia. Mimi nikiwa kama mwanachama wa CCM nimekerwa sana na matamshi yako unayoyatoa bungeni. Acha kutafuta cheap publicity!

Bashe wewe ni msaliti, tena inaonekana unatumiwa na CHADEMA sababu ulikuwa swahiba wa Lowassa. You are a traitor! You are a mole and you have to be removed!

Nakushauri Mwenyekiti wangu mpendwa na Rais wetu, ndugu John Pombe Magufuli, muondoe haraka sana huyu kijana ndani ya chama chetu sababu sasa ameshaota MAPEMBE. Bashe ni hatari sana kwa mustakabali wa chama chetu (CCM).

Hakuna chama chochote kile cha siasa hapa Tanzania ambacho kingemvumilia mwanachama kama BASHE! Mifano ipo mingi sana.

Mbaya zaidi anayoyaongea Bashe bungeni hayana faida yoyote ile kwa wananchi wa jimbo lake! Kazi yako Bashe ni kuwawakilisha wapiga kura wa NZEGA na siyo kupigana na CCM na serikali yake!

Mheshimiwa Rais; naomba uunde kamati maalumu ndani ya CCM kwa ajili ya kumchunguza huyu bwana mdogo. Anakoelekea siko kabisa na hatufai tena ndani ya chama chetu.

Mimi nina uhakika wa 90% hata kama tukimfukuza uanachama huyu msaliti BASHE, jimbo la NZEGA bado tutalichukua. Wakati ni sasa!

By Son of Gamba.
This is Stupid....
 
Bashe,ni kama mesi anaweza kucheza timu yoyote,na akachukua kikombe
 
Shida yangu ni Bashe anajipendekeza kwa wapinzani na kukidhoofisha chama chetu. Bashe ni msaliti wa chama.
hio ccm itabaki na wasukuma tu msipoangalia....na bashite...Nyerere alitabiri upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm yenyewe hivyo wakati umefika wa utabiri ccm inakatika vipande vipande .....na upinzani kuanza rasmi
 
hio ccm itabaki na wasukuma tu msipoangalia....na bashite...Nyerere alitabiri upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm yenyewe hivyo wakati umefika wa utabiri ccm inakatika vipande vipande .....na upinzani kuanza rasmi
Sijamwona mtu hapo. Hapo kila mmoja anatetea maslahi yake binafsi.
 
Chama kitu gani wewe kwa hiyo watu waendelee kutaharuki na nchi iangamie kwa kushindwa kusimamia haki kwanza anakiokoa kama uelewi chama kikichukua hatua na kubadilika nani atakiweza chama kikongwe kama ccm acha unazi nyie ndiona dhamira mbaya kwani hata raisi anahitaji washauri siyo mamangi meza!
 
Kama "BABA MUNGU" ni mjomba wako, basi itakuwa hivyo.

Lakini kama BABA MUNGU ni wetu sote, basi nasema, "USHINDWE KWA JINA LA YESU KRISTO!

Huyo yesu wako lazima ndo yule anayeliliwa na Bashite kwenye mahekalu ya dini za kila aina hadi freemason
 
Huenda ukawa unamuona si mfia chama, lkn sie tunamuona ni mzalendo kwa nchi yake.
Duh, hivi wazalendo wamekwisha hapa nchini hadi kumuorodhesha Bashe! Waulize akina Kubenea, Ndimara na Absolom Kibanda, hata ndugu wa marehemu Dan Mwakiteleko (Apumzike kwa Amani) watakwambia Bashe ni nani kwao na kwa Rostam Aziz.
 
Tatizo CHAMA CHA MAJAMBAZI A.K.A CCM Mtu akis3ma ukwel mnamuona muovu kwenu hiv mkoje mbn hambadilk kuna miwatu adi leo bado wana utawala wa kidicteta kwenye hii nchi , mm nashauri bashe piga kazi wakikutema usiogope r chama sio ki1 kwan raia tunataka mtu chapa kazi anayesimamia kwel na haki ata ukienda TLP tutakuchagu baba
 
Hivi kila anayetamka maneno yake kutokana na hisia zake binafsi tayari anakuwa mshauri, tena wa kiwango cha kumshauri Mkuu wa Nchi na Serikali (dola)? haya ni mkubwa. Ukishauri ukaona umekuwa ignored basi tambua kuwa hujafikia hadhi hiyo.
 
Nimekusoma vizuri sana ila ushauri kuwa Bashe afukuzwe chamani naona hujui unachotaka kufanya. Hakika, Bashe hana haja ya kujiunga CDM ili achukue jimbo. Naona unataka kuwasaidia TLP ya Mrema ipate kiti bungeni. Akiingia kwa TLP hata Mrema asipoenda kumkampenia, atalichukua jimbo asubuhi. Amekosa nini Bashe?? Unadhani Watanzania wa leo hawajui kweli na uongo?? Ngoja Ngosha aufuate ushauri wako ukione kiti cha Nzega kikienda upinzani asubuhi. Labda mbadilishe mbinu zenu kwa kukanyaga na kusigina katiba
 
Wewe usiejielewa ndo unapata shida na bashe, katika maslahi ya taifa chama huwa kinakaa pembeni, kama chama kitakuwa na watu wa namna ya kwako, itakuwa ni rahisi sana kuunga fikra za mwenyekiti hata kama si sawa
 
Mumfukuze na Nape kwani naye hana uzalendo na chama
Ijapokuwa ni mkweli
 
Hafukuzwi Mtu hapa wote wataendelea. Ujanja wa kutafuta kick hakikubaliwi.
 
Back
Top Bottom