Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,720
- 6,952
Ukweli ni jambo zuri sana kulisema, lakini uzalendo ni kitu bora zaidi kuliko kitu chochote kile.
Hussein Bashe wewe uko ndani ya CCM na ajabu wewe unaongoza kwa kuiponda CCM kuliko hata ambavyo unaviponda vyama vya upinzani. Katika siasa tabia kama hii haikubaliki hata kidogo.
Wana CCM tumekuwa tukikufuatilia kwa karibu sana, na matamko yako, yanaonesha wazi kabisa wewe siyo mzalendo kwa chama chako kilichokulea mpaka kukufikisha hapo ulipofika.
Inawezekana madai yako yakawa na ukweli ama la; lakini namna unavyoyawasilisha na mahali unapoyawasilisha siyo sahihi hata kidogo. Sidhani kama Mwenyekiti ataendelea kukuvumilia. Mimi nikiwa kama mwanachama wa CCM nimekerwa sana na matamshi yako unayoyatoa bungeni. Acha kutafuta cheap publicity!
Bashe wewe ni msaliti, tena inaonekana unatumiwa na CHADEMA sababu ulikuwa swahiba wa Lowassa. You are a traitor! You are a mole and you have to be removed!
Nakushauri Mwenyekiti wangu mpendwa na Rais wetu, ndugu John Pombe Magufuli, muondoe haraka sana huyu kijana ndani ya chama chetu sababu sasa ameshaota MAPEMBE. Bashe ni hatari sana kwa mustakabali wa chama chetu (CCM).
Hakuna chama chochote kile cha siasa hapa Tanzania ambacho kingemvumilia mwanachama kama BASHE! Mifano ipo mingi sana.
Mbaya zaidi anayoyaongea Bashe bungeni hayana faida yoyote ile kwa wananchi wa jimbo lake! Kazi yako Bashe ni kuwawakilisha wapiga kura wa NZEGA na siyo kupigana na CCM na serikali yake!
Mheshimiwa Rais; naomba uunde kamati maalumu ndani ya CCM kwa ajili ya kumchunguza huyu bwana mdogo. Anakoelekea siko kabisa na hatufai tena ndani ya chama chetu.
Mimi nina uhakika wa 90% hata kama tukimfukuza uanachama huyu msaliti BASHE, jimbo la NZEGA bado tutalichukua. Wakati ni sasa!
By Son of Gamba.