Siku za Hussein Bashe ndani ya CCM zinahesabika!

Siku za Hussein Bashe ndani ya CCM zinahesabika!

uzalendo siyo kuponda upinzani, ni kusema ukweli kutetea taifa.
Bashe amesema aliteakwa na usalama wa taifa. Je ulitaka akae kimya?
Siasa zilizo asisiwa ba mwalimu nyerere za kupinga ukosoaji wa utawala wake ndiyo unawafanya ccm kuona kuponda upinzani ni uzalendo kwani mwali jk aluwatimua wakina duarado, kolimba, jumbe kwa kupinga utaratibu wake. Ccm mnapaswa kuelewa siasa c vita na mjifunze kujenga hoja.
Ni kweli ktk siasa kuna kukosoana na kutofautiana kwa hoja kati ya wanachama. Je huyu Bashe anafanya hayo kwa manufaa ya chama chake au anajitafutia kuonekana ktk chama yeye ndio genius na wote chamani wana mawazo mgando?
Ikifikia hapo ni lazima mmoja ambae hakubaliani na wenzake awapishe ili wale wengine waendelee na lengo lao la pamoja.
Mmoja maana yake hata likitoka kundi la wana CCM 30 kwa kutofautiana mitazamo hiyo ni sawa na hapo mimi naona ndio mabadiliko makubwa ya uendeshaji wa chama na serikali yatakuwa yameleta Matunda yake chanya. Business as usual itoke.
 
uzalendo siyo kuponda upinzani, ni kusema ukweli kutetea taifa.
Bashe amesema aliteakwa na usalama wa taifa. Je ulitaka akae kimya?
Siasa zilizo asisiwa ba mwalimu nyerere za kupinga ukosoaji wa utawala wake ndiyo unawafanya ccm kuona kuponda upinzani ni uzalendo kwani mwali jk aluwatimua wakina duarado, kolimba, jumbe kwa kupinga utaratibu wake. Ccm mnapaswa kuelewa siasa c vita na mjifunze kujenga hoja.
Kama alitaka kutekwa kwanini hakutoa taarifa polisi? Kulikuwa na haja gani ya kuropoka bungeni wakati taratibu anazijua. Kwanini basi hakukaa na waziri wa mambo ya ndani kumwambia hili swala? Huyo dogo siyo mzalendo, huyu ni msaliti kwa chama chetu.
 
Mlitaka akae kimya mumteke pambafu nyie madikteta uchwara[emoji57][emoji57]
 
Bashe si msifia maovu, bashe simpiga makofi, bashe si msema ndiyo , bashe anatumia akili na fikra zake na si za chama wala mtu, maana amesha ona chama kitadumaza uwezo wake wa fikra kama walivyo dumaa wengine kiakili.
Kama anaona chama kinamdumaza kwanini asiondoke aende zake huko kwa MASWAHIBA wake CHADEMA?
 
Huyu ni UVCCM kabisa, huwa wana mawazo ya kijinga jinga, nipo CCM yaani hawa Vijana ukionekana unashauri haki wanaanzishs fitina. Macho yote yamewatoka kusubiri KUTEULIWA kuwa DED, DC na RC. Waoneeni huruma watz. Tz siyo ya CCM, BALI NI YA WATZ.... MImi nipo CCM LAKINI UJINGA WA HAWA WATU HUWA SIUVUMILII HATA KIDOGO
Ukatae, ukubali, Bashe ni msaliti wa chama chetu, na tutaungana kuhakikisha anang'olewa kwenye uanachama.
 
Ukweli ni jambo zuri sana kulisema, lakini uzalendo ni kitu bora zaidi kuliko kitu chochote kile.

Hussein Bashe wewe uko ndani ya CCM na ajabu wewe unaongoza kwa kuiponda CCM kuliko hata ambavyo unaviponda vyama vya upinzani. Katika siasa tabia kama hii haikubaliki hata kidogo.

Wana CCM tumekuwa tukikufuatilia kwa karibu sana, na matamko yako, yanaonesha wazi kabisa wewe siyo mzalendo kwa chama chako kilichokulea mpaka kukufikisha hapo ulipofika.

Inawezekana madai yako yakawa na ukweli ama la; lakini namna unavyoyawasilisha na mahali unapoyawasilisha siyo sahihi hata kidogo. Sidhani kama Mwenyekiti ataendelea kukuvumilia. Mimi nikiwa kama mwanachama wa CCM nimekerwa sana na matamshi yako unayoyatoa bungeni. Acha kutafuta cheap publicity!

Bashe wewe ni msaliti, tena inaonekana unatumiwa na CHADEMA sababu ulikuwa swahiba wa Lowassa. You are a traitor! You are a mole and you have to be removed!

Nakushauri Mwenyekiti wangu mpendwa na Rais wetu, ndugu John Pombe Magufuli, muondoe haraka sana huyu kijana ndani ya chama chetu sababu sasa ameshaota MAPEMBE. Bashe ni hatari sana kwa mustakabali wa chama chetu (CCM).

Hakuna chama chochote kile cha siasa hapa Tanzania ambacho kingemvumilia mwanachama kama BASHE! Mifano ipo mingi sana.

Mbaya zaidi anayoyaongea Bashe bungeni hayana faida yoyote ile kwa wananchi wa jimbo lake! Kazi yako Bashe ni kuwawakilisha wapiga kura wa NZEGA na siyo kupigana na CCM na serikali yake!

Mheshimiwa Rais; naomba uunde kamati maalumu ndani ya CCM kwa ajili ya kumchunguza huyu bwana mdogo. Anakoelekea siko kabisa na hatufai tena ndani ya chama chetu.

Mimi nina uhakika wa 90% hata kama tukimfukuza uanachama huyu msaliti BASHE, jimbo la NZEGA bado tutalichukua. Wakati ni sasa!

By Son of Gamba.
Mchunguzeni vizuri huenda anashare na Manji nae kaguswa.
 
KUNA UMUHIMU WA KUBADIRI KATIBA HASA KIPENGERE KINACHOMFANYA MBUNGE KUPOTEZA UBUNGE PUNDE ANAPOPOKWA UWANACHAMA WAKE NA CHAMA CHAKE.
NAKUMBUKA ZITTO, KAFULILA WALIONEKANA WASALITI KWA KUVISEMA VYAMA VYAO.
Bashe keep it up. Pale nzega huna mpinzani, don't fear. Speak it up!
 
Ninapomsikia ccm akimtaja Mtakatifu Yesu nashikwa na hasira huku wivu wa Bwana ukinila nimtandike. Ccm wote komeni kuanzia leo kumtaja Bwana Yesu.
Utaisoma namba!

Bwana YESU ni wetu sote tunaomwamini.
 
KUNA UMUHIMU WA KUBADIRI KATIBA HASA KIPENGERE KINACHOMFANYA MBUNGE KUPOTEZA UBUNGE PUNDE ANAPOPOKWA UWANACHAMA WAKE NA CHAMA CHAKE.
NAKUMBUKA ZITTO, KAFULILA WALIONEKANA WASALITI KWA KUVISEMA VYAMA VYAO.
Bashe keep it up. Pale nzega huna mpinzani, don't fear. Speak it up!
Endelea kumdanganya tu.
 
Kiapo cha ccm Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko ni wana ccm wachache wanaoelewa kiapo hiki mmoja ni Bashe.
 
Bashe ni kielelezo cha uhuru wa kujieleza.Tz tungekuwa na akina Bashe ata 100 tu pale bungeni tungekuwa mbali sana.
 
Tutaisafisha ccm ndani kwa ndani, sasa tuna vijana wanao jiamini, hakuna cha mwenye kiti wala katibu mkuu. Bashe ni mbunge anae jiamini na anaaminiwa na wananchi wake. Leo hii akipigwa chini basi uchaguzi ukirudiwa atakua mgombea wa ACT na atashinda.
 
Ulichoandika ni jibu tosha kwanini wabunge wa ccm huwa mnapitisha miswada na bejeti za kipuuzi
 
Back
Top Bottom