Siku za Hussein Bashe ndani ya CCM zinahesabika!

Siku za Hussein Bashe ndani ya CCM zinahesabika!

Nadhani serikali haiwezi kila siku kukanusha habari za uvumi au zisizo na ukweli.

Hii ndiyo njia ambayo imeamua kuitumia.
Kutekwa watu ni uvumi? Unaishi wapi wewe mpaka hujui nini kinaendelea? Serikali hii imevunja rekodi ya kukanusha vitu vidogodogo tena hata vile vinavyoibuka facebook sasa unaitaka ipuuzie jambo nyeti kama hilo? Yule waziri jana alifata nini pale kama taarifa hazina ukweli?
 
Fukuzeni wabunge wote wanaojitambua kisha muwabakishe wapuuzi wanaoitikia ndiyooooo! Wewe unaona ni bora watanzania wafe kwa njaa kuliko wabunge kuiwajibisha serikali ya CCM siyo?
 
Ukweli ni jambo zuri sana kulisema, lakini uzalendo ni kitu bora zaidi kuliko kitu chochote kile.

Hussein Bashe wewe uko ndani ya CCM na ajabu wewe unaongoza kwa kuiponda CCM kuliko hata ambavyo unaviponda vyama vya upinzani. Katika siasa tabia kama hii haikubaliki hata kidogo.

Wana CCM tumekuwa tukikufuatilia kwa karibu sana, na matamko yako, yanaonesha wazi kabisa wewe siyo mzalendo kwa chama chako kilichokulea mpaka kukufikisha hapo ulipofika.

Inawezekana madai yako yakawa na ukweli ama la; lakini namna unavyoyawasilisha na mahali unapoyawasilisha siyo sahihi hata kidogo. Sidhani kama Mwenyekiti ataendelea kukuvumilia. Mimi nikiwa kama mwanachama wa CCM nimekerwa sana na matamshi yako unayoyatoa bungeni. Acha kutafuta cheap publicity!

Bashe wewe ni msaliti, tena inaonekana unatumiwa na CHADEMA sababu ulikuwa swahiba wa Lowassa. You are a traitor! You are a mole and you have to be removed!

Nakushauri Mwenyekiti wangu mpendwa na Rais wetu, ndugu John Pombe Magufuli, muondoe haraka sana huyu kijana ndani ya chama chetu sababu sasa ameshaota MAPEMBE. Bashe ni hatari sana kwa mustakabali wa chama chetu (CCM).

Hakuna chama chochote kile cha siasa hapa Tanzania ambacho kingemvumilia mwanachama kama BASHE! Mifano ipo mingi sana.

Mbaya zaidi anayoyaongea Bashe bungeni hayana faida yoyote ile kwa wananchi wa jimbo lake! Kazi yako Bashe ni kuwawakilisha wapiga kura wa NZEGA na siyo kupigana na CCM na serikali yake!

Mheshimiwa Rais; naomba uunde kamati maalumu ndani ya CCM kwa ajili ya kumchunguza huyu bwana mdogo. Anakoelekea siko kabisa na hatufai tena ndani ya chama chetu.

Mimi nina uhakika wa 90% hata kama tukimfukuza uanachama huyu msaliti BASHE, jimbo la NZEGA bado tutalichukua. Wakati ni sasa!

By Son of Gamba.
Kasumba yenu ni kuitikia ndiyoooooo....sasa huyu hataki hivyo
 
Son of Gamba hichi sio kikao cba CCM bali ni kikao cha bunge la taifa acha ubashite kwenye maswala nyeti ya kitaifa watekaji wakubwa nyie.
 
Haya ni mawazo duni ksbisa! Bashe haikandii ccm bali anaisaidia inaonekana wewe ni miongoni mwa wana ccm wanaodhani wako sahihi kila wakati na wasiotaka kusahihishwa
 
Mkiambiwa ukweli mnacharuka, kumbe mna tabia ya baba yenu. Shenzi kabisa
 
Ushauri wangu waende nae2 hafu wakamuache pale mwisho, maana huyo anatafta kick au umaarufu, nauzuri wa TZ washamfahamu.
 
Kuisifia serikali na chama ni uzalendo

Ila uzalendo zaidi ni kuikosoa serikali
 
Nchi kwanza chama baadae! Bashe endelea hivyo hivyo nchi hii sio mali ya MTU binafsi,
 
Kama "BABA MUNGU" ni mjomba wako, basi itakuwa hivyo.

Lakini kama BABA MUNGU ni wetu sote, basi nasema, "USHINDWE KWA JINA LA YESU KRISTO!
Ninapomsikia ccm akimtaja Mtakatifu Yesu nashikwa na hasira huku wivu wa Bwana ukinila nimtandike. Ccm wote komeni kuanzia leo kumtaja Bwana Yesu.
 
Kwani bashe kafanya jambo gani baya ndani ya CCM?

Mkuu wenu si anasema Msema kweli ni mpenzi wa Mungu? Sasa iweje aseme kweli wewe utokwe povu? Inaonekana nyie hamuupendi ukweli ee.

Je ni vizuri kuendekeza mapenzi kwa chama au maslahi ya nchi?

Tangu viroba vifungiwe watu hamnazo kabisa
 
bashe sio hatari ila sio mnafiki wabunge wengi wa ccm ni wanafiki wapo kama makondoo tu wao ni kuinama chini tu safi sana bashe hata wakikufukuza heshima na ukweli wako utadumu milele ,unataka awe kama lusindee si bora ukalime nyanya kuliko kuwa mbunge mnafiki kama wa ccm
 
Ukweli ni jambo zuri sana kulisema, lakini uzalendo ni kitu bora zaidi kuliko kitu chochote kile.

Hussein Bashe wewe uko ndani ya CCM na ajabu wewe unaongoza kwa kuiponda CCM kuliko hata ambavyo unaviponda vyama vya upinzani. Katika siasa tabia kama hii haikubaliki hata kidogo.

Wana CCM tumekuwa tukikufuatilia kwa karibu sana, na matamko yako, yanaonesha wazi kabisa wewe siyo mzalendo kwa chama chako kilichokulea mpaka kukufikisha hapo ulipofika.

Inawezekana madai yako yakawa na ukweli ama la; lakini namna unavyoyawasilisha na mahali unapoyawasilisha siyo sahihi hata kidogo. Sidhani kama Mwenyekiti ataendelea kukuvumilia. Mimi nikiwa kama mwanachama wa CCM nimekerwa sana na matamshi yako unayoyatoa bungeni. Acha kutafuta cheap publicity!

Bashe wewe ni msaliti, tena inaonekana unatumiwa na CHADEMA sababu ulikuwa swahiba wa Lowassa. You are a traitor! You are a mole and you have to be removed!

Nakushauri Mwenyekiti wangu mpendwa na Rais wetu, ndugu John Pombe Magufuli, muondoe haraka sana huyu kijana ndani ya chama chetu sababu sasa ameshaota MAPEMBE. Bashe ni hatari sana kwa mustakabali wa chama chetu (CCM).

Hakuna chama chochote kile cha siasa hapa Tanzania ambacho kingemvumilia mwanachama kama BASHE! Mifano ipo mingi sana.

Mbaya zaidi anayoyaongea Bashe bungeni hayana faida yoyote ile kwa wananchi wa jimbo lake! Kazi yako Bashe ni kuwawakilisha wapiga kura wa NZEGA na siyo kupigana na CCM na serikali yake!

Mheshimiwa Rais; naomba uunde kamati maalumu ndani ya CCM kwa ajili ya kumchunguza huyu bwana mdogo. Anakoelekea siko kabisa na hatufai tena ndani ya chama chetu.

Mimi nina uhakika wa 90% hata kama tukimfukuza uanachama huyu msaliti BASHE, jimbo la NZEGA bado tutalichukua. Wakati ni sasa!

By Son of Gamba.
Shida yenu CCM mkiambiwa ukweli hamuutaki ila unafiki unapokelewa vizuri.
 
Huenda ukawa unamuona si mfia chama, lkn sie tunamuona ni mzalendo kwa nchi yake.
Wapinzani wote wanamwona Bashe ni mzalendo. Lakini uzalendo unaanzia ndani ya chama chako. Huyu kijana siyo mzalendo hata kidogo bali ni mnafiki tu anayejipendekeza kwa wapinzani. Lengo lake ni kukidhoofisha chama chetu.
 
Back
Top Bottom