Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
Sijui kama wenzagu huwa mnakumbuka hizi enzi? au kwa kuwa tulishapita huko basi imetoka...Lakini katika mambo ya zamani nikumbukayo ni siku ya kwanza nilipoanza darasa la kwanza shule ya msingi kule mkoani kwetu. Hiii ni baada ya jaribio la awali kushindwa baada ya kupimwa kimo changu na kuonekana mi mdogo/mfupi kwa kushika sikio la upande wa kushoto kwa mkono wa kulia..Nilikuwa mgeni wa kila kitu na tukio moja lililonishangaza zaidi ni kupewa kaubao kadogo na chaki kwa ajili ya kujifunza kuandika sikuwa na wazo kuwa kuna siku na mimi nitakuwa mahali napuliziwa na kiyoyozi....Mwalimu wangu wa darasa la kwanza namkumbuka sana sijui kama bado yuko hai au la lakini natamani nikutane naye leo mtu huyo aliyeweka jiwe la kwanza la msingi katika safari ya maisha yangu...Wewe Je??