Siku yangu ya kwanza nilipoanza darasa la kwanza Primary School | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siku yangu ya kwanza nilipoanza darasa la kwanza Primary School

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sajenti, Dec 8, 2009.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Dec 8, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sijui kama wenzagu huwa mnakumbuka hizi enzi? au kwa kuwa tulishapita huko basi imetoka...Lakini katika mambo ya zamani nikumbukayo ni siku ya kwanza nilipoanza darasa la kwanza shule ya msingi kule mkoani kwetu. Hiii ni baada ya jaribio la awali kushindwa baada ya kupimwa kimo changu na kuonekana mi mdogo/mfupi kwa kushika sikio la upande wa kushoto kwa mkono wa kulia..Nilikuwa mgeni wa kila kitu na tukio moja lililonishangaza zaidi ni kupewa kaubao kadogo na chaki kwa ajili ya kujifunza kuandika sikuwa na wazo kuwa kuna siku na mimi nitakuwa mahali napuliziwa na kiyoyozi....Mwalimu wangu wa darasa la kwanza namkumbuka sana sijui kama bado yuko hai au la lakini natamani nikutane naye leo mtu huyo aliyeweka jiwe la kwanza la msingi katika safari ya maisha yangu...Wewe Je??
   
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Dec 8, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mimi nawasiliana sana na mwalimu wangu wa kwanza aliyenifundisha darasa la kwanza. Alikuwa ndo kwanza ametoka chuo, bado binti mbichi. Akawa ananituma mimi na washikaji tumpelekee barua jamaa aliyekuja kuwa mume wake. Alikuwa anafundisha shule jirani kama mwendo wa saa moja hivi! Sasa mwalimu wangu amekuwa mzee, kijana wake wa kwanza alioa mwaka jana na nilimpatia mchango wangu. Pamoja na huyo mama, namkumbuka sana mwalimu wangu wa hisabati na English darasa la saba (ila huyu alikuwa anapenda sasa totoz wa darasani kwetu na alikuwa anawatafuta kwa nguvu na kasi mpya)! Bila hao watu sina hakika kama sasa hivi ningekuwa nazijua taa za mjini na hii key board ya PC!
   
 3. GP

  GP JF-Expert Member

  #3
  Dec 8, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mkuu hii CHAI!.
   
 4. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #4
  Dec 8, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  dah! usinikumbushe aisee. siku ya kwanza niliokwenda shule praimari ,ndio siku nilojua kwamba Mungu kaumba, kale kamwalimu kalikonipokea na kunisajili kalikuwa kazuri ,kameumbika sana,kabinti kakicheka kanabonyea mashavuni. haka kamwalimu kaliwasababishia wanafunzi wengi kufeli mitihani. RIP mwalimu kama ushakufa kama hujafa na ni memba wa jf niPM.
   
 5. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #5
  Dec 8, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Mkuu Dark City, kwangu hata mimi huyo mwalimu wangu wa kwanza alikuwa mwanamke na mwili mdogo mdogo hivi. Pamoja na mambo yote kitu kimoja alichokuwa ananifanya nimuogope ni tabia yake ukikosea kitu yeye hukuchapa kwa kutumia rula ya mbao anakugonga kwenye vidole mazee maumivu yake ni balaa. Nakumbuka ukifika muda wa kwenda home anatuambia tuimbe kale kawimbo..Saasa saasa saa ya kwenda kwetu kwa heri mwalimu kwaheri tutaonana keshooooo!!! mwenzio anakusindikiza na kozi then moto mkubwa!!
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  Dec 8, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Duh mie wadau Siku ya kwanza kuanza shule, nilipelekwa na my mother hadi shule, siku hiyo shule ilikuwa inafunguliwa, so wote tulikuwa mstarini km palivyokuwa panaitwa au assembly, mwalim mkuu akaja alikuwa anaitwa Mwl Ngailo, kwa vile my late father alikuwa na wadhifa pale mkoani tulikuwa na access ya kuweza kumuona muda wowote si unajua bongo tena, mama akanikabidhisha kwake baada ya maongezi nikaenda na mie assembly, walimu kibao walikwepo pale na fimbo km kibao kama kuni dah niliogopa sana sisi ndo std one simjui mtu, akaja yule Mwl Mkuu akatukaribisha kwa ka hotuba akagawa majukumu pale, cha ajabu siku ile shule nzima tukarudishwa NYUMBANI, kesho yake ndo tukaanza masomo rasmi, hiki kitu cha kurudishwa home ktkk maisha yangu yote ya shule siku ya kufungua shule basi lazima niwahadithie rafiki zangu na haijawahi tokea tena. darasani sasa tulikuwa na walimu wawili mwl wa LUGHA na Mwandiko. Huyu wa Mwandiko alikuwa mwalimu mtu mzima sana wakati ule alikuwa hata na miaka 50 akiitwa mwl Assenga, kwa kweli alikuwa mwl mzuri ajabu alitu handle km wajukuu zake, tulifurahia sana wakati wa mwandiko huyu wa lugha nimemsahau alikuwa msichana wa km 28-32 wakati ule, alikuwa akituchapa fimbo za mgogoni na rula za kwenye nuckles si mchezo kweli lugha haikupanda sana. Nakumbuka wakati ule kwa sababu ya madarasa machache utakuta kuna kuwa na shift mbili, wengine wanaingia saa mbili na kutoka saa tano asubuhi wengine wanaingia saa tano asubuhi ikifika saa sita na nusu wanatoka warudi home kula mpaka saa nane kasorobo mnakuwa assembly mnakaguliwa saa nane kamili mnaingia darasani mpaka saa kumi na nusu ndo mnarudi home. sasa mie kwa sababu nilizoea wakati naanza nilianza na shift ya asubuhi kutoka saa tano, ilipofika shift ya kuingia sa tano na kutoka saa sita nanusu na kurudi saa nane mie ilikuwa sirudi tena, weee ile wiki ilipoisha tukarudi ya asubuhi kutoka saa tano yule mwalimu wa lugha akaanza kusoma majina ya watoro moja likiwa langu, tulikula fimbo za mapaja na adhabu za kichura chura sikurudia tena na sijasahau ile siku. lkn iko siku ntafunga safari mpaka Sumbawanga nikaione tu JANGWANI Primary school, kwa kweli kwa miaka 3 niliyosoma pale nna good memories sana za pale na marafiki zangu.
   
 7. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #7
  Dec 8, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mkuu, pia kulikuwa na kipindi cha kukagua kucha, meno na kama umeoga au la! Kweli tumetoka mbali sana!!
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  nakumbuka siku ya kwanza baba alinipeeka shule, tulipofika tu nikaandikishwa then baba akamwambia mwalimu huyu mtoto anatumia mkono wa kushoto kila kitu hadi kula analia mkono huu sasa naomba ufanye juu chini asiandikie mkono huu. chapa sana viboko kama hatasikia, mzee akaondoka.

  zoezi likaanza, nilikuwa kweli siwezi kabisa kufanya chochote na mkono wa kulia, basi yule mwalimu kabuni njia ya kuwa ananiwekea kipande cha jiwe kwenye mkono wa kulia kwa juu ili niandike a e i o u. ilinichukua mda sana, kumudu nashukuru maana kwa sasa naweza kuandikia mikono yote japo wa kulia uko slow na mwandiko wake ni mbaya sana kuliko nikiandika kwa mkono wa kushoto
   
 9. b

  bnhai JF-Expert Member

  #9
  Dec 8, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna tatizo mtu akiwa mashoto. (left handed)
   
 10. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #10
  Dec 8, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Pamoja na yote katika ugeni wangu nilipoanza darasa la kwanza primary nilikuwa navutiwa sana na wanafunzi waliokuwa wanapiga kwenye bendi ya shule muda wa kuingia darasani. Ila kuna tukio moja nalo huwa nalikumbuka la jamaa mmoja wa darasa la Sita alimtandika teacher mmoja kichwa then jamaa akasepa kisa mshikaji alikuwa mtoro wakaenda kumbeba mzobe mzobe kutoka nyumbani kwao. Jamaa siku hizi ni driver kwenye haya ma-trucks ya kwenda nchi jirani. Nilishangaa sana mwanafunzi kupiga mwalimu ukizingatia katika watu waliokuwa wakiheshimika pale kwenye eneo letu ni walimu!!! Mnakumbuka mambo ya mwandiko "mcharazo"??..
   
 11. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #11
  Dec 8, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ...Hilo hata mimi lilinikuta nakumbuka ilinichukua muda mrefu sana kuacha kuandika kwa mkono wa kushoto na yote hii ni baada ya mzee nae kuona kama vile kuandikia mkono wa kushoto ni jambo lisilowezekana. Lakini nina binti yangu wa miaka 8 anaandikia kushoto yuko vizuri sana darasani na hand writting nzuri sana!!! Hivi ni imani au uelewa mdogo??
   
 12. K

  Kabogo Member

  #12
  Dec 8, 2009
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli tumetoka mbali
   
 13. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #13
  Dec 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  MKUU
  Lazima ulianza Primary ukiwa tayari ushaanza kutumia mipira kwenye kamba..
  Bisha!
   
 14. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #14
  Dec 8, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Baba na mwalimu wote walikosea sana kukulazimishia kuandikia kulia wakati wewe ni mtu wa kushoto.
   
 15. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #15
  Dec 8, 2009
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  hapa mwanasayansi nasema "no komenti"
   
 16. i

  ishuguy Member

  #16
  Dec 8, 2009
  Joined: Nov 3, 2007
  Messages: 76
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  me nakumbuka first attempt iligoma..nilikuwa nikifika shule nalia sana mpaka wakanionea huruma..nadhani was not gud enoght to start sdt 1, 2nd attemp ikatiki.
   
 17. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #17
  Dec 8, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Unajua enzi zile primary school mazee jamaa walioko std 5,6 na 7 zilikuwa njemba ambazo nadhani kwa sasa ni wanafunzi wa "A"level hivi tatizo lilikuwa nini?? au yale mambo ya kuzungusha mkono mpaka kugusa sikio la upande wa pili ndio ilikuwa inachelewesha?? Mnakumbuka mambo ya chipukizi, kuimba kwaya na ngonjera kwa wale waliokuwa madarasa ya juu kidogo???
   
 18. S

  Senghor Member

  #18
  Dec 8, 2009
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Enzi hizo za darasa la kwanza kuna mwanafunzi mwenzetu alikuwa mtoro sana. Hii ilipelekea huyo mwanafunzi kulamba mvua za bakora ingawa wakati anaendelea kuadhibiwa alichomoka mikononi mwa walimu na kutimua mbio hadi nyumbani kwao. Kesho yake akaja na baba yake amebebwa mabegani hadi kwenye ofisi ya walimu, na ilikuwa vurugu ambapo baba alimwambia mtoto arudie kwa sauti maneno haya
  "nyie walimu wote wa*inga sana **mamayo zenu"
  mtoto aliyatamka maneno yale kisha wakasepa.
   
Loading...