Siku ya Wanawake ni wanawake wanaonung'unikia watoto wao

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,319
12,622
Wanawake ndio waliozaa watoto wote wa kike na kiume kwa uchungu na mahangaiko makubwa, kisha wakashiriki kwenye kuwakatia vitovu vyao mara tu baada ya kuwazaa. Wakawanyonyesha, kuwaogesha na kuwavisha na kuwasomesha hadi pale watoto walipoanza kujitegemea wenyewe.

Inatisha na inashangaza kuona wakinamama haohao kuonekana wakilalamiikia na kunung'unika juu ya watoto wao wa kiume kuwa eti wanawatesa, wanawanyonya, wanawadharau, wanawapunja, wanawakandamiza na wanawaonea mama zao. Hii inafikirisha sana.

Wakati huu tukielekea kwenye kilele cha siku ya wanawake lazima mijadala yetu ijikite kwenye kutafuta ukweli kuhusu:

1. Ni kweli wanaume wanawaonea wanawake (mama, dada, shangazi na bibi zao)?

2. Kama ni kweli wanawaonea, wanawaonea kwa namna gani?

3. Ni lini mwanaume anaanza kumuonea mwanamke?

4. Ni dalili zipi zinaonyesha kuwa mwanamke anaonewa na mwaume?

5. Kwanini mwanamke amekubali kuonewa na mwanaume (mtoto wake)?

6. Kwanini mwanaume aamue kumuonea mwanamke (mama, dada, shangazi, bibi) yake?

7. Ni sababu zipi zinamfanya mwanamke awe rahisi kuonewa na mwamke?

8. Mwanamke afanye nini ili asionewe na mwaume?

9. mwanamke atujuaje kama kuonewa na mwanaume sasa kumekwisha?

Hapa wanawake lazima wajichambue wao wenyewe kuona wapi wanasema kweli, wapi wanapotosha, wapi chanzo ni mwanamke mwenyewe, wapi wanakosea na wapi wajisahihishe badala ya kutupia shutuma zote wanaume (watoto wao wenyewe) na wakati huohuo kutegemea huruma za wanaume haohao kuondosha tatizo lao.

Madai yao mengi ni fake na bandia kwakuwa hayataji usawa wa mwanamke katika kukwea minazi na kuangua madafu, kumsaka simba anapokuwa amekula mifugo ya familia, kuzama chini kuchimba madini, kuendesha bodaboda, kuleta chakula mezani, kununua bia kule bar, kulipia guest wakati wa starehe ya mume na mke, kubeba mizigo kule bandarine (ukuli), hawadai usawa kwenda kuchunga mifugo porini, bali wanataka usawa kwenye kugawana mali na kazi za ofisini tu baaasi. Ni madai fake buana!!!
 
Back
Top Bottom