Siku Ya Uelewa wa Usonji Duniani. Je, unawezaje Kumtambua Mtoto mwenye Usonji?

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,026
1,622
Usonji ni changamoto ya Ukuaji ambayo hutokea pale ambapo Ubongo hufanya kazi kwa namna tofauti. Mtoto hupata changamoto hii anapokuwa tumboni na dalili huonekana kuanzia Umri wa Miaka Mitatu na kuendelea

Watu wenye Usonji hupata changamoto hasa za Kuwasiliana Kijamii. Kasi ya kukua kiakili kwa Watoto wenye Usonji huwa ndogo kulingana na kasi ya kukua Kimwili

Aprili 2 kila Mwaka ni maadhimisho Siku ya Uelewa wa Usonji, inayolenga kukuza Uelewa ili kuongeza ushirikishwaji wa Kijamii wa watu wanaoishi na hali ya Usonji

Je, unawezaje Kumtambua Mtoto mwenye Usonji?

1. Kutoitika anapoitwa kwa Majina yake, kutotabasamu pia huepuka kutazamana moja kwa moja Machoni

2. Hukasirika sana iwapo hawapendi ladha, harufu, au sauti ya kitu fulani, pia hufanya vitu kwa kujirudiarudia kama Kusugua Mikono au Kuvuta vidole

3. Kuwa Mkimya sana na endapo akiongea hurudia maneno yale yale
 
Back
Top Bottom