Septemba: Mwezi wa Uelewa wa Saratani za Utotoni Duniani

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Septemba kila mwaka ni Mwezi wa Uelewa wa Saratani ya Utotoni Duniani. Mwezi huu hutumika kutambua Watoto na Vijana walioathiriwa na aina mbalimbali za Saratani

Pia kuheshimu Vijana wanaougua Saratani, Familia zinazowatunza, Wataalamu wa Afya na Walezi wao, Walionusurika, Watoto waliopoteza maisha yao, na Wanasayansi waliojitolea kupambana saratani ya utotoni

Alama ya Mwezi huu ni Utepe wa dhahabu unawakilisha aina zote za Saratani inayoathiri Watoto na Vijana

Saratani inachangia vifo vingi vya Watoto na Vijana. Uwezekano wa kupona baada ya kugundulika na Saratani ya utotoni inategemea Nchi ambayo Mtoto anaishi

Kwa mujibu wa WHO, Katika Nchi za kipato cha juu, zaidi ya 80% ya Watoto walio na Saratani hupata Matibabu kamili na kupona, lakini Nchi nyingi za Kipato cha Kati na cha Chini chini ya 30% ya Watoto ndio hupona

Sababu za viwango vya chini vya kuishi katika Nchi hizo ni pamoja na: kuchelewa kugundulika, kutokuwa na uwezo wa kupata Uchunguzi sahihi, Tiba isiyoweza kufikiwa, kuacha Matibabu

Saratani hutokea kwa Watu wa rika zote na inaweza kuathiri sehemu yoyote ya Mwili. Huanza na mabadiliko ya kijenetiki katika Seli moja, kisha hukua na kuwa Uvimbe (Tumor), ambao huvamia sehemu zingine za mwili

Tofauti na Saratani kwa Watu wazima, idadi kubwa ya Saratani za Utotoni hazina sababu inayojulikana. Tafiti nyingi zimebaini ni Saratani chache kwa Watoto zinazosababishwa na Mazingira au Mtindo wa Maisha.

Dalili za saratani kwa watoto wadogo.

1.Kwanza kabisa mtoto anakuwa na uvimbe usio wa kawaida na ambao hauna maumivu kwenye sehemu za mashavu, kwenye shingo, tumbo, miguuni na sehemu zozote za mwili, kwa mara ya kwanza uvimbe huu unakuwa hauna maumivu hata kidogo lakini ikiwa umetibuliwa au kuchokonolewa uvimbe huu unaweza kubadilika na kutengeneza kitu kingine na kusababisha maumivu kwa mtoto.

2. Kwa hiyo baada ya kuona uvimbe wa aina hii na mtoto anaendelea na maisha bila kuonyesha Dalili yoyote ya maumivu kwanza kabisa mtoto anapaswa kupelekwa kwa wataalamu wa magonjwa ya saratani na epuka kabisa kutingisha uvimbe huu kwa kutumia waganga wa kienyeji ambao hawana utaalamu wowote au mzazi mwenyewe kuamua kuchokonoa uvimbe huu, mpeleke mtoto hospitalini ili aweze kupata utaratibu kutoka kwa wataalamu wa afya.

3. Macho ya mtoto kuwa mekundu kuvimba, kuongezeka, au upofu kwa ghafla.
Kwa kawaida kwa upande wa macho ya mtoto yanaanza kidogo kidogo kuwa mekundu na siku kwa siku wekundu unazidi na hatimaye mtoto anashindwa kuona linaweza kuanza jicho moja na baadae likaingia la pili au yote mawili yanaweza kupata shida kwa wakati mmoja na kama mtoto hajapata huduma mapema upofu unaweza kutokea kwa mtoto .

4. Pia kwa wakati mwingine damu utoka puani na kwenye fizi.
Na pia hizi ni mojawapo ya Dalili za saratani kwa watoto wadogo kwa sababu damu zikianza kutoka puani uanza kidogo kidogo na uongezeka zaidi pale kama kuna joto la kwenye mazingira likiwa juu na pia mtoto damu uanza kupungua siku kwa siku na hata damu ikiongezwa inapungua na kwa upande wa fizi ikitokea mtoto kama amefikia wakati wa kupiga maswaki akipiga damu utoka kwa wangi kwenye fizi. Kwa hiyo walezi na wazazi wanapaswa kufika kwa wataalamu wa afya ili kupata matibabu zaidi.

5. Mtoto kukonda na kupungua uzito bila sababu.
Kwa wakati mwingine mtoto anaanza kukonda na kupungua uzito bila sababu na huku anakuwa anacheza kawaida ila anakonda na uzito unapungua kwa hiyo Mama anapaswa kumpeleka mtoto huyo kwa wataalamu wa afya ili kuweza kujua tatizo ni nini kwa mtoto, na kwa wakati huu hata mtoto akipewa lishe ya aina yoyote anaongezeka kidogo na baadae hali inakuwa kama kawaida yaani kukonds na kupungua uzito.

6. Maumivu ya kichwa kwa mda mrefu na kutapika.
Kwa kawaida kwa watoto wale ambao wanaweza kuongea anaweza kukwambia jinsi anavyojisikia mara nyingi utasikia analalamika kuhusu kichwa kwa wale ambao hawajui kuongea atakuwa analia mara kwa mara , na pia kwa upande wa kutapika mtoto anaweza kutapika kwa mda mrefu hata kama hajala lolote anatapika tu na pia kwa wakati mwingine matapishi huwa mengi kuliko chakula ambacho anakula hali ambayo uwatia wasiwasi pia wazazi wengine wanaweza kuwa na imani potovu kuhusu hilo.

7. Mtoto anaweza kudhoofika na kuacha kucheza pamoja na watoto wengine.
Kwa upande mwingine mtoto anakosa raha anaanza kudhoofika na anashindwa kucheza na wengine kwa wakati mwingine Mama au walezi wanaweza kuchukulia kubwa ni sehemu ya maisha kubwa mtoto huwa hachezi kumbe kuna tatizo ndani yake kwa hiyo uchunguzi kwa mtoto ni lazima ili kuweza kuona kuna tatizo gani, kwa hiyo wazazi au walezi wanapaswa kuwa pamoja na watoto ili kuangalia mabadiliko katika makuzi yao.

8. Kwa wakati mwingine mtoto akipata ajali kidogo anatokea na damu nyingi ukilinganisha na kidonda chake kwa hiyo unakuta damu inapungua mwilini na kwa mara nyingine Dalili za wazi ujitokeza ambapo mtoto akipata ka jeraha na damu zikitoka anabadilika rangi na kuwa na rangi nyeupe fulani hivi kwenye mwili.

Saratani zinazowashambulia watoto.
1.Kwanza kabisa tunajua kuwa saratani ni Ugonjwa ambao utokea kwa sababu ya kuwepo kwa seli zisizohitajika zinaweza kutokea katika sehemu yoyote ile ya mwili . Kwa watoto Sababu za kuwepo kwa tatizo la saratani hazijathibitishwa bado ila kuna vitu ambavyo vinaweza kuchangia kama vile uvutaji wa sigara wakati wa ujauzito, pombe kali na mtindo wa maisha wa Mama kwa a ujumla wakati wa ujauzito unaweza kusababisha kuwepo kwa saratani kwa watoto. Kwa hiyo watoto wanashambuliwa na saratani zifuatazo.

2.Kuna saratani ya damu.
Aina hizi ya saratani utokea pale ambapo mtoto anakuwa anaishiwa na damu mara kwa mara inawezekana kupitia sehemu yoyote kama vile puani au inawezekana isipite sehemu yoyote ila mnaongeza damu ila baada ya siku chache mtoto anaishiawa damu, aina hii ya saratani kama haijafahamika mapema inaweza kumchukua mtoto mara moja kwa hiyo baada ya tatizo hili kutokea wazazi au walezi wanapaswa kuwasiliana na wataalamu zaidi wanaohusika na Magonjwa ya saratani.

3. Saratani ya macho.
Pia ni mojawapo ya saratani inayowapata watoto unakuta jicho la mtoto linakuwa na uvimbe mdogo na kuwasha na kadiri mda unavyokwenda unakuta uvimbe unaongezeka na mtoto anashindwa kuona na kwa wakati mwingine unakuta jicho limetokezea kwa nje na kumfanya mtoto kuangaika kwa sababu ya kuwepo kwa maumivu makali kwenye jicho. Kwa hiyo wazazi na walezi baada ya kuona tatizo kama hili mnapaswa kumpeleka mtoto hospitalini mapema ili kupunguza ukali wa tatizo.

4. Kuna saratani ya mifupa.
Pia na hii ni aina ya saratani ambayo ushambulia mifupa kwa na kabisa mtoto uanza kusikia maumivu anapotembea na pia kadri siku zinavyoenda anashindwa kutembea kabisa kwa sababu mifupa uanza kusagika na kwa hiyo ukimgusa sehemu yoyote ile anaanza kulia kwa hiyo mtoto anaweza kuishi kwa kulala maisha yake yote na kushindwa kuendelea kukua katika hatua za makuzi ya mtoto.

5. Kuna saratani ya ubongo na ngozi.
Aina hii tena ya saratani uwapata watoto chini ya miaka mitano kwa sababu unakuta watoto wanakuwa kama zezeta na wanashindwa kukua katika hatua za mtoto na pengine mtoto hawezi kukaa na kusimamia viungo na pia macho yao huwa yanaangalia makengeza na pengine mtoto anashindwa kuwa na balance. Hali utokea kwa sababu ya kukosa mawasiliano kati ya ubungo na misuli.

6. Pia kwenye ngozi ya mtoto panakuwepo na ma upele ambayo hayaeleweki na hata yakitibiwa mara hali inajirudia kuna wakati mwingine ngozi ya mtoto inaweza kubadilika kwa namna moja ama nyingine, pengine ngozi inaweza kuwa nyeupe au pengine nyeusi zaidi na kwa wakati mwingine kuwa na rangi ya mabaka mabaka kwa hiyo ngozi ubadilika Mara nyingi kwa hiyo baada ya kuona hali kama hizi ni wazi kubwa hiyo ni kansa ya ngozi.

===========

Leukemia ni aina ya saratani ya damu ambayo inaathiri tishu za utengenezaji wa seli za damu katika mfupa mdongo na mifupa mingine ya mwili. Watoto wanaweza kuathiriwa na aina mbalimbali za leukemia, lakini aina mbili kuu ni leukemia ya lymphoblastic (ALL) na leukemia ya myeloid (AML). Hapa kuna habari muhimu kuhusu leukemia kwa watoto:
  1. Leukemia ya Lymphoblastic (ALL): Hii ni aina ya kawaida zaidi ya leukemia kwa watoto. Inatokea katika seli za lymphoblast, ambazo ni aina ya seli za mfumo wa kinga. ALL inaweza kutokea katika watoto wa umri wowote, lakini mara nyingi hutokea katika watoto wa umri wa miaka 2 hadi 4.
  2. Leukemia ya Myeloid (AML): Hii ni aina nyingine ya leukemia ambayo inaweza kuathiri watoto, ingawa ni nadra kuliko ALL. AML inatokea katika seli za myeloid, ambazo ni sehemu ya utengenezaji wa seli za damu za mwili.
Sababu za Leukemia kwa Watoto:Sababu za kusababisha leukemia kwa watoto bado hazijulikani kikamilifu, lakini zinaweza kuwa zinahusishwa na mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya jeni au sababu za mazingira. Utafiti unaendelea kufanywa kuelewa vyema sababu za leukemia kwa watoto.
Dalili za Leukemia kwa Watoto:Dalili za leukemia kwa watoto zinaweza kujumuisha:
  • Uchovu na udhaifu.
  • Kutokwa na damu au kuvuja damu kwa urahisi.
  • Kuvimba kwa tezi za limfu.
  • Maumivu ya mifupa au viungo.
  • Kupungua kwa uzito bila sababu ya wazi.
  • Homa kubwa na maambukizo yanayotokea mara kwa mara.
Matibabu ya Leukemia kwa Watoto:Matibabu ya leukemia kwa watoto yanaweza kujumuisha:
  1. Chemotherapy (matibabu ya dawa za saratani) - Matibabu haya hutumika kuharibu seli za leukemia.
  2. Radiation therapy (matibabu ya mionzi) - Inaweza kutumika kama sehemu ya matibabu ya leukemia kwa kusaidia kuharibu seli za saratani.
  3. Stem cell transplant (upandikizaji wa seli shina) - Inaweza kuhitajika kwa baadhi ya watoto kulingana na aina na hatua ya leukemia.
Matibabu ya leukemia kwa watoto mara nyingi hufanywa katika vitengo maalum vya matibabu ya watoto na timu za wataalamu wa matibabu ya watoto.
Ni muhimu kuelewa kuwa matibabu ya leukemia kwa watoto yanaweza kuwa ngumu na yanaweza kuchukua muda mrefu. Msaada wa kisaikolojia na kijamii kwa familia ni muhimu wakati wa kushughulikia hali hii ngumu. Kwa hiyo, ni muhimu kuwa na mawasiliano mazuri na daktari wa mtoto wako na kufuata maelekezo yake kuhusu matibabu na huduma za utunzaji.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom