ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,956
- 7,002
Nani kakataa?KWANZA SIKU INAANZA JIONI
.... Ikawa jioni ikawa asubuhi siku moja... Mwanzo 1:5..Ikawa jioni ikawa asubuhi... Mwanzo 1: 8, 13, 19, 23, 31.
SIKU YA SABA MUNGU HAKUFANYA KAZI
.. Mungu akaibariki siku ya saba akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya Mwanzo 2:3
SIKU YA SABA NI LINI?
-Yesu alikufa saa tisa siku ya maandalio ya Sabato.... Marko 15:33 & 42 na alifufuka siku ya KWANZA ya juma baada ya Sabato... Marko 16: 1-6
-Siku ya maandalio ya Sabato ni ijumaa
USHAHIDI: Katoliki na waprotestanti wote wanaadhimisha "IJUMAA KUU" kwa dhana ya kwamba Yesu aliuwawa IJUMAA
-Sabato ni Jumamosi
USHAHIDI: Wayahudi hawajawahi kuacha kutunza Sabato "SIKU YAO YA SABATO NI JUMAMOSI"
Wakristo wote na wasabato wakiwemo, wanatambua jumamosi ndiyo siku ya sabato.
Kitu pekee wasichokubaliana ni isue ya kufanya kazi.
Wakati wakristo hufanya kazi 24/7, wasabato wanajitahidi kufanya 24/6, lkn siku zote wanashindwa.
Wakati wakristo hukutana siku ya kwanza, wasabato hukutana siku ya saba tofauti kabisa na maagizo. Agizo ni kupumzika, wao hulazimika kusafiri kwenda ibadani.
Yesu aliye kiongozi wetu, hakuwahi kupumzika, siku ya sabato pamoja na kuingia hekaluni kufundisha, lkn alipiga na kazi pia
Yesu alikufa ijumaa, tangu sabato inaingia alikuwa amepumzika hadi alipofufuka jumapili. Hakuna kazi aliyoifanya. Hivyo alipumzika kwelikweli. Ndivyo ilivyo hata kwa Mungu, sabato alipumzika akifurahia kazi ya mikono yake, hakufanya lolote.
Kumbuka, kuabudu nako ni kazi, zaidi ya hayo, huambatana na shughuli mbalimbali kama safari ambazo kwa baadhi ya watu ni ajira.
Pia watumishi ktk kanisa, nao huwa kazini.