Hilo hata wao wanajua ni vile tu wanashupaza shingo maana hata jumapili wanayoabudu wanasema ndiyo siku Yesu aliyofufuka na maandiko yanasema siku aliyofufuka ilikuwa siku ya kwanza sasa ukihesabu toka hiyo jumapili siku ya kwanza jumamosi itakuwa ya saba
Lakini watakataa watasema hiyo ilikuwa ya wayahudi lakini ni uongo maana pale Edeni ilipoanzishwa hapakuwa na wayahudi wowote Lakini kwa maneno ya Yesu mwenyewe anasema
MK. :2:27
Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato.
Sabato ni kwa ajili ya mwanadamu na sote tu wanadamu kwa hiyo ni ya kila mmoja mtanzania, mkenya, muarabu, mhindi, na wote duniani hapa na siyo wayahudi pekee
Kwa hiyo ukiikataa uikatae kwa sababu zako binafsi lakini biblia maandiko ya haki yanasema sabato ni kwa ajili ya wanadamu