Siku ya saba (Sabato) ni Jumamosi

Siku ya saba (Sabato) ni Jumamosi

Unaposema sabato za kishenzi au ni uhuni una maana gani?
Sabato (kwa Waebrania) ilikuwa na mazongwe zongwe mengi ambayo yalikuwa hayatekelezeki kamwe....kwa kifupi yalikuwa ni mambo ya kipuuzi ma ujinga (ushenzi tuu)

Yesu mwenyewe Bwana wa Sabato aliivunjilia mbali...
 
Najaribu kuwaza kuwa ikiwa sabato ilikuwa ni agizo la Mungu kwa watu wake, wewe unawezaje kusema kuwa agizo hilo ni la kishenzi?
Sabato ilikuwa ni Agizo la Mungu kwa Waebrania...ilikuwa ni pumziko kukumbuka kutolewa utumwani Misri...
 
Je hauoni utakuwa unamtusi aliyetoa agizo hilo zamani hizo ambaye ni Mungu mwenyewe?
Namtusije angali Yeye mwwnyewe ndiye aliyeivunja sabato ya kishenzi....

Yeye alisema " Ndiye bwana Wa Sabato" Sabato ilifanyika kwa ajili ya mtu lakini si mtu kwa ajili ya Sabato
 
. Waitaliano huiita jumamosi Sabato
2. Wagiriki huiita jumamosi Sabato
3. Kihispaniola jumamosi huitwa Sabado
Wacha uongo...narudia tena wacha uongo.....Unafikiri woote huku tunaakili au tumelishwa matango pori ya Mwanamke Ellen G White...

Ungekuwa na akili timamu ungetuwekea mtiririki wa majina ya siku za wiki kwenye nchi husika..

Eti umefanya utafiti....!!! Nyinyi watu nani kawaloga
 
Attachments

  • 9cfecc5c139fb53b2d7ce7e54d457929.png
    9cfecc5c139fb53b2d7ce7e54d457929.png
    10.2 KB · Views: 34
  • Screenshot_20190315-231303.png
    Screenshot_20190315-231303.png
    47.1 KB · Views: 29
  • Screenshot_20190315-231659.png
    Screenshot_20190315-231659.png
    75.5 KB · Views: 32
  • Screenshot_20190315-232558.png
    Screenshot_20190315-232558.png
    63 KB · Views: 30
Wacha uongo...narudia tena wacha uongo.....Unafikiri woote huku tunaakili au tumelishwa matango pori ya Mwanamke Ellen G White...

Ungekuwa na akili timamu ungetuwekea mtiririki wa majina ya siku za wiki kwenye nchi husika..

Eti umefanya utafiti....!!! Nyinyi watu nani kawaloga
Mkuu mimi sijalogwa wala siko under influence of any intoxication, ila nimejibu kile ambacho nimekitafiti na kukithibitisha.

Uzuri lugha majina ya siku ktk lugha hizo yapo mtandaoni, na nimekuwekea hapo juu. Nadhani kabla ya kuniita muongo ungefanya kwanza kuthibitisha kuwa je ndivyo ukweli ulivyo?

Swali ambalo unapaswa ujiulize ni kwa nini ktk hizo lugha wanaiita jumamosi sabato?
 
Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato (Mk 2:28). Waisraeli waliadhimisha Sabato kwa kuwa ndio siku waliotoka utamwani Misri. Wakristo (ukiacha Wasabato) wanaadhimisha mapumziko siku ya Kwanza ya Juma (Jumapili) kwa sababu ndio siku Yesu alishinda mauti (alifufuka), na kufufuka kwa Yesu ndio MSINGI wa Ukristo. Kama Kristo hakufufuka, basi, kuhubiri kwetu ni bure na imani yenu ni bure.(1 Kor 15:14).

Kwa hiyo SIO KOSA Wasabato wanapoadhimisha Siku ya Bwana Jumamosi, (kwa vile Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato) na vivyo hivyo SIO KOSA kwa madhehebu mengine kuadhimisha Jumapili. Maana halisi ya neno SABATO ni SIKU YA KUPUMZIKA (sio siku ya Jumamosi). Ndio maana ulikuwepo mwaka wa saba ulioitwa MWAKA WA SABATO. Biblia inasema:- Mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa Bwana; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu. (Law 25:4)
 
Kuna Sabato, ambayo ni Jumamosi, na Siku ya Bwana, ambayo ni Jumapili. Hii ni siku Bwana alifufuka. Roho Mtakatifu aliwashukia Mitume Jumapili pia. Ndiyo ya Bwana.

Wakristu walihamishia Ibada Jumapili tangu mwanzo. Soma Acts 20:7 na 1Corinthians 16:2 na Colossians 2:26-17. Haya maandiko yanasema Wakristu wamekuwa wakikutana katika Ibada Siku ya Bwana, sio Sabato.

Tunaishi Agano Jipya. Tuko na Yesu, sio viashiria tu kama amri ya kutairi ambayo Mitume waliiweka pembeni. Soma Galatians 5:1-6

Hao wanaosisitiza kuishi Agano la Kale wanatolea sadaka za kuchinja wanyama kila siku? Maana hiyo ni amri kwenye Agano la Kale.
 
Ndugu zangu, ngoja niwaambie hivi ; kusali Siku yoyote, kati ya jumapili hadi jumamosi hakutakupeleka katika uzima wa milele.
Kitakachokupeleka katika uzima wa milele, ni kumpokea Yesu, na kumkiri mbele za watu kuwa ni Bwana na mwokozi wako , na kisha kukaa ndani ya Yesu .
Mkristo ameagizwa kukesha akiomba, sasa mambo ya kugombea Siku ya kupumzika kunatoka wapi kama umeambiwa kesha ukiomba, maana yake kila iitwayo Siku wewe Uko katika maombi.
Yesu ndiye njia na kweli, na uzima, sio Siku. Kwanza majina ya Siku kuanzia jumapila hadi jumamosi ni majina ya miungu ya kipagani , kwa nini mnagombea majina ya miungu ya kipagani?.
Wakati MUNGU anafanya uumbaji, Siku aliyopumzika ilikuwa ni Siku ya saba, ambayo haikuwa na jina la jumamosi au Saturday . ni Siku ya saba.
Kesheni mkiomba ndugu zangu. Jumamosi, jumapili, ijumaaa, zitawapeleka motoni. Mtazame Yesu ili uurithi uzima wa milele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waarabu tena? Sasa kwa kiswahili jumamosi inaitwaje?

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mosi ni moja na wamefanya hivyo ili ijumaa ionekane ni siku ya saba lakini ulimwengu mzima unatambua kuwa siku ya saba ni jumamosi na si vinginevyo
 
KWANZA SIKU INAANZA JIONI
.... Ikawa jioni ikawa asubuhi siku moja... Mwanzo 1:5..Ikawa jioni ikawa asubuhi... Mwanzo 1: 8, 13, 19, 23, 31.

SIKU YA SABA MUNGU HAKUFANYA KAZI

.. Mungu akaibariki siku ya saba akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya Mwanzo 2:3

SIKU YA SABA NI LINI?

-Yesu alikufa saa tisa siku ya maandalio ya Sabato.... Marko 15:33 & 42 na alifufuka siku ya KWANZA ya juma baada ya Sabato... Marko 16: 1-6

-Siku ya maandalio ya Sabato ni ijumaa
USHAHIDI: Katoliki na waprotestanti wote wanaadhimisha "IJUMAA KUU" kwa dhana ya kwamba Yesu aliuwawa IJUMAA

-Sabato ni Jumamosi
USHAHIDI: Wayahudi hawajawahi kuacha kutunza Sabato "SIKU YAO YA SABATO NI JUMAMOSI"

Kwa Mujibu wa Kalenda ya Wakoloni ni wazi tunafahamu kwamba Jumamosi ni Siku ya Saba. Kwa hiyo unataka tufanyeje?
 
KWANZA SIKU INAANZA JIONI
.... Ikawa jioni ikawa asubuhi siku moja... Mwanzo 1:5..Ikawa jioni ikawa asubuhi... Mwanzo 1: 8, 13, 19, 23, 31.

SIKU YA SABA MUNGU HAKUFANYA KAZI

.. Mungu akaibariki siku ya saba akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya Mwanzo 2:3

SIKU YA SABA NI LINI?

-Yesu alikufa saa tisa siku ya maandalio ya Sabato.... Marko 15:33 & 42 na alifufuka siku ya KWANZA ya juma baada ya Sabato... Marko 16: 1-6

-Siku ya maandalio ya Sabato ni ijumaa
USHAHIDI: Katoliki na waprotestanti wote wanaadhimisha "IJUMAA KUU" kwa dhana ya kwamba Yesu aliuwawa IJUMAA

-Sabato ni Jumamosi
USHAHIDI: Wayahudi hawajawahi kuacha kutunza Sabato "SIKU YAO YA SABATO NI JUMAMOSI"
Wapi kwenye Biblia palipoandikwa Moja kwa Moja kuwa Sabato ni Jumamosi???.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom