Siku ya msiba wangu, kwake iwe ni sherehe

Siku ya msiba wangu, kwake iwe ni sherehe

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,080
Reaction score
1,449
Siku ya msiba wangu

Haoni navyoumia, sichoki kubembeleza
Kila siku ninalia, huku nikimueleza
Karibu nitajifia, Moyo ushajimaliza
Siku ya msiba wangu, kwake iwe ni sherehe

Aalike na vigoma, na wapiga vuvuzela
Kwake nimetia koma, ila anipa madhila
Aniona ja ukoma, haoni zangu fadhila
Siku ya msiba wangu, kwake iwe ni sherehe

Na anywe pombe alewe, nafsini asuuzike
Vipi asinielewe, anafanya niudhike
Mpaka napiga yowe, ndani kunao mvuke
Siku ya msiba wangu, kwake iwe ni sherehe

Bwana wa muda apate, kama hakuwa anaye
Mimi nipo petepete, yote sababu ni yeye
Nimeshamvisha pete, na bado siko mwenyewe
Siku ya msiba wangu, kwake iwe ni sherehe

Yananiua mahaba, kosa ni wangu upendo
Shingoni linimekaba, kama vile ni magendo
Atajakuwa kahaba, Hatapata wa mhendo
Siku ya msiba wangu, kwake iwe ni sherehe

Abuuabdillah ✍️
 
Attachments

  • 14d306b9c04aae47ff62487c9dc7c80c.jpg
    14d306b9c04aae47ff62487c9dc7c80c.jpg
    47.1 KB · Views: 30
Back
Top Bottom