Siku ya kwanza kuingia shule ya bweni ya Serikali

Siku ya kwanza nafika kidato cha 5 nikapokewa na watoto wa olevel wakanifikisha kwe bweni nililopangiwa sababu hiyo shule ilikua unapangwa kabla hata hujareport, nimefika tu nikatoa malapa nikaoge nabadili nguo kugeuka hamna malapa wala ndoo vyote vimeibiwa nilichukia shule mpaka nikaomba uhamisho
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Old moshi a.k.a Moshi Sec,karibu na Chuo cha Ushirika upande mwingine C.C.P,Chuo cha polisi, nilikutana na matope hatari.Udongo mwekundu unanata sana kipindi cha mvua.Matope bwenini unakwangua na jembe ndio uanze kudeki.Kuvaa gamboot kila mahali ,mpaka kwenda kuoga bafuni unavaa gamboot na taulo kiunoni ,kandambili mkononi.Ukifika bafuni unavua gamboot unavaa kandambili.ukimaliza unarudi tena kwenye gamboot.Chakula cha kugombania O levels wanafujo sana .Ugali na maharage au uji wanajaza kwenye ndoo ndogo,wengine wanakosa.Usiku hakuna walinzi kwa hiyo tunazurura tu mjini Moshi tupendavyo.Shule haikuwa na fence.Ni uamuzi wako uende prepal kusoma au kuzurura.Nilimaliza miaka miwili ya A level.
Hii ya kuvaa rain boots na taulo nimecheka hahahahahahaha
 
Nakumbuka shule yetu ilikuwa na wanafunzi wengi walikuwa ni kutoka Kigoma,Tabora na Mwanza...washamba balaa...umeme ukikatika tunawapa ndoo wakachote umeme...yaani hata watu wazima walikuwa wanabeba ndoo kwenda kuchota umeme.....na tulikuwa tunawaambia wasiporudi na umeme wabaki huko huko....walipata taabu sana
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ khaa nimecheka mpk tumbo linauma,,khaa
 
Ile nimefika tu form V pale mjini Tanga, nilifika kwa kuchelewa kama wiki 3. Nakuta watu wanasolve necta ya form VI tena maswali ya complex number wakati hata topic nilikuwa siijui inahusu nini. Nilipagawa.
Hahahah ungemuita jamaa mmoja anaitwa msocha akusaidie
 
Mimi nakumbuka ilikuwa shule ya Sokondari Bagamoyo enzi hizo ilikuwa ni day and boarding school. Wasichana na baadhi ya wavulana wachache sana walikuwa day walikuwa hawafiki hata mia kwa ujumla wao nikakuta vijana wanaita Bagamoyo Boys High School wakati kuna wadada, nilipo fuatilia sababu nikaambiwa wale wadada walikuwa na sura kama za wavulana. Isingekuwa sketi zile zenye rangi nyekundu mtu angedhani wote ni boys kweli!
 
Shuke za boarding miaka ile zilikuwa ni shida sana, tabu tupu, wakati naanza form 1 milambo sekondari tabora kulikuwa na pisi 1 la kisukuma linaitwa Maduhu Bunyenyeke kutokea shinyanga, huyu jamaa kama yumo jf kwa kweli daah, huwa simsahau, alituchapa sana mikwaju, akipewa adhabu ya kufyeka ananyakua form 1 ili afyeke, nakumbuka alinipa sent 50, ati nikamnunulie sigara 5, kipande 1 cha sabuni na nirudishe change shs 20, ila jamaa hakunaliza shule alifukuzwa mwaka huo huo akiwa form 2
 
Nakumbuka Lyamungo aisee,nimefika form one pale sema nilichelewa kidogo,nimemaliza kufanya registration, napelekwa bwenini wakatokea watu wakabeba tranka langu kama jeneza wakawa wanalia wakaongezeka wengine wanarusha na maua kabisa!

Daah karibu nigeuze aisee,sema nilikuja kulipiza na Mimi baada ya kuzoea kwa form one waliofuatia!
Hahahaha, kaka milambo sec lilikuwa ni godoro la sufi, yaani wakiona new comers wanaingia getini na wanafunzi wamekaa viungani wakipiga story wote wanaacha wanaanza kulia, ati umebeba maiti
 
Hahahaha, kaka milambo sec lilikuwa ni godoro la sufi, yaani wakiona new comers wanaingia getini na wanafunzi wamekaa viungani wakipiga story wote wanaacha wanaanza kulia, ati umebeba maiti
Hahaha,kumbe hata Milambo huo mchezo ulikuepo?
 

Heaven Sent hivi ulisoma hii mpenzi? Haki mkwe sina.

BTW mkwe umefichika wapi?
Nilifika shule usiku sana bweni lina harufu kali sijapata kuisikia vile kuna mwalimu alinipokea akaniambia asubuhi tu niende ofisini kufanya usajili.

Asubuhi mapema nikawahi ofisin kwenda kufanya usahili bwenini nikawaacha madogo kadhaa wa o level wanajiandaa kwenda madarasani.

Ofisini ile kulipa ada zao na kukamilisha usahili wakague vyeti na kukutana na wagen wengine wapya hapa na pale nikamaliza kila kitu saa nne.

Kurudi bwenini washavunja kufuli saa nyingi Dawa kubwa zile za mswaki, makatoni ya sabuni za kuogea na za unga, mafuta ya kupaka, kalamu na mazaga yote wale washamba wameiba wameniacha na counter book, nguo taulo na vitabu vichache

Roho iliniuma sana vile uzoefu wa maisha ya boarding nayajua nikahisi ni uzembe wangu jambo moja wahuni walikosa hela sikuweka kwenye sanduku la chuma.

Baada ya tukio sikureport popote nilienda kununua dawa ndogo ya mswaki, mswaki mmoja na sabuni ndogo ya kuoegea

vitu vingine vyote nikaanza kuiba kimya kimya niliiba bila huruma nilikua naiba ile mbaya mwaka mzima wezi wanatajwa hakuna anayenihisi vunja vunja makufuli wako darasani naiba vingine hata sina shida navyo natupa chooni iba iba mbaya sana.

Uchaguzi TYCS nachaguliwa kua katibu mkuu hakuna anayewaza mwizi ni mimi bwenini nakemea uwizi asubuhi jion na vunja.

Baadaye nikaamua kuacha mwenyewe. Nilisimulia marafiki kadhaa baada ya kumaliza shule miaka mingi ilivyopita. Mama alisema niwaombe msamaha. Sikuwahi kufanya hivyo.
 
Kuna shule inaitwa Mwakavuta (wenyeji wanaiita Mwakauta) nikavuta siku za kuripoti kwa kua nilitaka nitoke nyumbani baada ya valentine day.

Nafika siku hiyo ni jumapili siku ya wali. Nikala kidogo nikaugawa, naenda kuosha sahani ghafla ukungu umetanda kiasi hauwezi kuona hatua mbili mbele.
Nikasimama pale pale kwa zaidi ya dakika 45 ili ukungu upite nisije nikapotea nikaingia msituni. Sehemu yenye baridi kali kama haujavaa viatu au ni vyepesi vidole vya miguuni unaanza kuhisi vinachomwa chomwa na sindano. Nahisi ni dalili za kua frostbitten.

Ukungu unamalizikia vidole vikawa vinaonyesha kama damu imevilia. Tumelala bwenini nakutana na watu kutoka Chunya, Kilimanjaro, Moshi, Kigoma, Mafinga n.k. na wote wanasema baridi la pale si mchezo.

Asubuhi naamka. Njia za shule zote zina theluji, boksa niliyoiacha jana kwenye kamba imeganda kwa barafu.

Nikaanza kupima pros na cons.
-Kwanza walimu walituambia watoto wa O Level wote wana ngoma, kumbe na wale watoto waliambiwa sisi wote tuna ngoma. Ingawa wakinga siyo wabanaji lakini hilo doa litachukua muda wangu.

-Shule haina mabinti wazuri, hao waliopo wavuna mbao na wanakijiji wote mnawagombea.

-Unaweza kua na hela lakini hakuna cha kununua.

-Umbali mpaka wilayani ni 22KM na gari ni moja likipita limepita ama utembee, nilitembea aisee nilikoma, kila sehem ya mwili iliuma. Nilienda kupiga PPS hadi PPS zinatoka ndo nagundua kuna makamasi yalikua yananitoka. Sijui mpiga picha alidhani urembo.

-Rate ya kupiga puchu ikawa juu.

-Walimu wawili wa masomo yangu walikua wanakukaririsha kitu cha kitabuni hawakichambui wala nini halafu ni unasomewa sasa akiwa anasoma unagundua na yeye kuna vitu anavijua hapo. Mmoja alienda Mbeya akakaa zaidi ya mwezi huku somo limesimama.

-Chakula kibaya sijapata kujua. Kuna wadudu hua wanaranda randa kwenye balbu ukiwaua wanatoa harufu mbaya, sasa wale unawakuta kwenye maharage wapo kibao. Wali ikawa ndiyo luxury food, ugali unaula kidogo, asubuhi unanywea uji, makande, unakula kidogo asubuhi unanywea uji.
Wali ulisababisha watu wapigane, kulikua kuna paper two sasa form six wanajihisi wao ndiyo wanatakiwa kuanza, jamaa wa form five akafosi kingi ebwana washkaji wawili akaanza kumpiga.
Ila baadaye na yeye aliwatafuta mmoja mmoja na wakamheshimu.

Nilifeli kwa mengi.
Umenichekesha hapo kwenye kamasi na PPS eti cjui mpiga picha alizani urembo hahahahaaaaaaa my ribs
 
Kuna kitu inaitwa sifongo, kitu porage halina sukari.

Mchana unakutana na gazeti, yan ule ukoko wa ugali unaumwagia chuzi la maharage yenye mazagazaga(mazagazaga ni vitunguu vilivyokaangwa na pilipili)

Ukitoka hapo unauchapa usingiz wa nguvu, saa kumi jioni tunaibukia self reliance... unachimba mashimo ya mizabibu dadek au kumwagilia milonge then michezo

Maisha yalikua interesting sana boarding skuli zote nlizopita

Usiku ni mwendo wa kubundi

Bihawana
Tosaganga
Songea boys
Pugu boys

It was fun
 
Back
Top Bottom