Siku ya kwanza kuendesha teksi

WISDOM SEEDS

JF-Expert Member
Jun 1, 2011
841
282
Dereva mmoja ambaye ni mtu wa makamo alikuwa kapaki taxi yake kwenye eneo la maegesho,
akaja mtu mmoja aliyehitaji huduma ya usafiri. Baada ya makubaliano walianza safari yao, baada ya
safari ya dakika kadhaa yule abiria alimgusa dereva kwenye bega kumweleza kuwa keshafika safari yake.
Dereva alishtuka sana na kutoa macho kwa woga huku gari yake ikiserereka hadi kwenye mtaro.

Abiria wake akashangaa sana na kumuuliza kulikoni, dereva alimjibu kuwa hii ni mara yake ya kwanza
kuendesha gari ya abiria, siku zote alikuwa akiendesha gari ya maiti...
 
Hivi inakuwaje watu wengi wanaogopa maiti, na ikitokea mtu aliyezimia na wati wakafikiria kuwa amekufa, akiamka watu wengi ukimbia, sielewi kwanini na kwa sababu gani wanakimbia na kuogopa.
 
duh!!!in reality madereva waliozoea kuendesha magar makubwa ya mizigo muda mrefu ukiwapa gar ndogo tena iwe auto huwa wateseka sana,wengine hushindwa kabisa.
 
WS, hi kali aisee, nilikuwa najaribu kutafakari ingekuwaa ni mimi ningefanyaje!
Hahahahaaaaaaaaaa!!!!
 
Hii kali!maiti inatisha ukiwa hujazoea!ila waliozoea kuendesha hayo magari ya maiti wanaona ni kawaida kabisa!hawana hofu hata!wanabeba kama mizigo mingine tuu!mimi oneday nilikutana na jamaa yangu alifiwa na katoto nje ya nchi!akaniambia mwanangu aliugua bahati mbaya amefariki!ndio ninaye hapa nampeleka nyumbani!nikamuuliza mwili uko wapi?akasema nimeshacheck inn!du nilihamaki sana!ila baada ya kuzika nikamtafuta nikamuuliza kulikoni!akasema kama ange declare kama marehemu angelipa like 5,000 usd hv!ila kwa vile ulikua kama parcel tuu unalipia packing fees tu basi!jamaa wana upark fresh unabeba like the normal cargo!ila jamaa wenye ndege wanakua wanajua!
 
Back
Top Bottom