Siku ya kwanza kijiweni kama dereva bodaboda

Kama upo kigamboni uwe unawahi pale uhasibu kuanzia saa 10 alfajiri pale pesa hatari ,mida hiyo hakuna kabisa bodaboda

Pili na muhimu Sana ,vaa helmet muda wote na usiwe na haraka barabani na jitahidi Sana ufwate sheria

Kingine Kama pikipiki Ni mpya uwe makini kupakia abria wa kuingia vichochoroni
Boda ziko nyingi tu mida iyo, na abiria we ng wa kigamboni bei zao za kupoza tu.
 
Asante sana mkuu, hili napita nalo moja kwa moja
Nikupongeze kwa uamuzi mgumu kama huu.
Ili ufanikiwe...tengeneza identity yako ili utengeneze wateja wako mwenyewe;

1. Uendeshe kwa mwendo wa wastani

2.Uwe makini barabaranibusiingie hovyo

3. Epuka kutongoza hovyo

4. Uwe mkweli ukiahidi muda wa kufika kwa mteja

5. Lugha iwe laini kwa wote

6. Uwe msafi usinuke

7. Ucheshi kiasi
 
Nakushauri ukiweza unaweza ku-park kariakoo

Kama una ndugu au jamaa yako (mwenye biashara kkoo) anaweza kukudhamini madukani ongea nae halafu mpite madukani akutambulishe ukipatikana mzigo unapigiwa simu unawapelekea wateja

Ukifanya mizigo inaweza kukulipa zaidi
Mf:kutoka kkoo kupeleka mzigo fire 5,000
Mbezi stendi ni 12,000
Kwa siku ukipata mizigo hata 6 inatosha



Ni uaminifu tu.
Hili ni wazo zuri sana
 
Back
Top Bottom