Siku ya Kimataifa ya Usikivu: Maoni na Ushauri kutoka kwa Daktari Bingwa kuhusu changamoto ya Usikivu

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Leo tarehe 3 mwezi Machi 2021 ni siku ya usikivu duniani. Hii ni siku ambayo inasherehekewa duniani na kampeni yake inaendeshwa na Ofisi inayojulikana kama “Prevention of Blindness and Deafness” ya Shirika la Afya Duniani (W.H.O)

Jambo kubwa linalofanyika katika siku ya leo ni kukumbushana namna mbalimbali za kufanya ili kuzuia kupoteza usikivu na kuhamasisha kujali usikivu kwa mbinu anuai.

IMG_20210303_141534_704.jpg


Chanzo cha Siku hii

Siku ya Afya ya Usikivu duniani ilianza mwaka 2007 na kabla ya mwaka 2016 ilikuwa ikijulikana kama “International ear care” yaani Siku ya kimataifa ya huduma ya Masikio.

Kuanzia 2017, siku hii inajulikana kama siku ya usikivu duniani yaani (World Hearing Day). Kaulimbiu ya mwaka huu ni “Hearing care for all” (afya ya usikivu kwa wote).

Vitu ambavyo tunavisisitiza mwaka huu ni kuanza kuchunguza usikivu, kufanya ukarabati kwa maana unaweza kuona baada ya kuchunguza ukaona mtu ana shida gani na kutatua tatizo.


Dkt. Mfuko achambua Afya ya Sikio

Inner-Ear-1.jpg


Katika mahojiano na JamiiForums, Dkt. Godlove Mfuko ameeleza kwa kina juu ya Afya ya Sikio katika siku hii maalum. Dkt. Mfuko ni Daktari Bingwa Mbobevu wa upasuaji magonjwa ya mfumo wa fahamu wa usikivu na magonjwa ya usawa na kizunguzungu Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila

Anaanza kwa kufafanua juu ya vitu vya kutokufanya na vya kukumbuka:

“Kwanza, tuna changamoto hapa Tanzania, hatuna takwimu nzuri ambazo ni za uhakika kueleza ukubwa wa tatizo katika nchi yetu. Kwa takwimu za dunia, tuna taarifa kuwa tuna watu wenye matatizo ya usikivu wengi sana hata wale wadogo kabisa wanakaribia 1.7 billioni, takribani bilioni 2 lakini wale watu ambao wana ule usikivu ambao ni ‘disabling sensory hearing loss’ yaani shida ya usikivu ambayo inalemaza kabisa ni takribani watu milioni 500.

Kitu cha msingi kwetu Madaktari wa Masikio, Pua na Koo (ENT) tunalo jukumu la kujenga uelewa kwa watu wajue kuwa kuna shida.

Kuna tafiti zimewahi kufanyika Afrika Kusini na Marekani kujaribu kuangalia utayari wa watu kwenda kupima masikio. Watu wanaweza kukaa na shida ya masikio hata kwa miaka kumi. Mtaani mnakuta kuna mtu mnaweza kumuongelesha lakini hasikii vizuri na haendi hospitali, lakini kuna intervention inaweza kufanyika na mzigo na gharama kubwa sana kifedha.

Hali ya Tanzania

Kwa Tanzania, kuna tafiti zimefanyika kwenye baadhi ya makundi ya watu kwa mfano utafiti umewahi kufanywa na madaktari wa Muhimbili kuona madhara ya usikivu kwa watu wanaofanya kazi katika viwanda ambapo walipata takwimu ambazo zilistua sana. Utafiti huo ulifanyika mwaka 2015 na pia kuna utafiti mwaka huo ulifanywa kuangalia shida ya usikivu au madhara yanayoweza kusababisha shida ya usikivu kwa wanaofanya kazi migodini.

Ukiangalia hizo takwimu mbili za 2015 kwa Tanzania, unaona takribani 30% ya watu wanaofanya kazi katika mazingira yenye kelele sana wana tatizo la usikivu. Tatizo ni kubwa na inaleta shida kwenye tija (productivity) katika jamii kwa sababu mtu kama hasikii kuna vitu anaweza kushindwa kuvifanya.

Kama ni mtoto mdogo anaweza akawa na shida katika kujifunza. Mtu mzima anaweza akashindwa hata kujichanganya vema katika jamii; kuna madhara makubwa sana ya kukosa usikivu.

Changamoto ya watu kutoenda hospitali wanapoumwa

Kuna utafiti umefanyika South Afrika unaonesha kuwa watu wanaokwenda hospitali ni chini ya 20% kwa ujumla. Kuna kundi kubwa la watu mtaani ambao wana shida za kiafya lakini wanakaa tu hawaendi hospitalini.

Dkt. Mfuko anawashauri watu waende kufanya screening lakini pia anaishukuru Wizara ya Afya kwa ushirikiano inaowapa madaktari wa mifumo ya masikio, upumuaji na koo (ENT) katika kuandaa mipango mikakati ya Wizara katika eneo la masuala ya usikivu na kutoa ushauri wa kitaalamu. Kuna mipango inapangwa sasa, kuona jinsi gani tunaweza kuhusisha suala la usikivu kwenye hata sensa ili tuweze kuapata takwimu na kuziangaza kwa mapana.

Wanaovaa Headphones washauriwa kuwa makini

20210303_115755_0000.png


Dkt. Mfuko anasisitiza: "Kitu cha msingi zaidi cha kusisitiza kwenye haya masuala ya usikivu ni makelele kama watu wanaovaa headphones. Sababu za kukosa usikivu zipo nyingi lakini sababu kubwa zaidi ni hizi kukaa kwenye makelele muda mrefu. Headphones zinasababisha madhara yanatokea taratibu. Ndani ya miaka 5 hadi 10 mtu anaweza kuwa hasikii tena.

Kumtambua mwenye changamoto ya usikivu

20210303_123652_0000.png


Namna rahisi ya kumjua kwa mfano kama ni mtoto mdogo utaona hata kukiwa na makelele hageuki wala hastuki, mpeleke hospitali kupima. Pia, kwa mtoto inapelekea kutofanya vema katika masomo yake. Kwa mtu mzima, unaweza kukuta unaongea naye mpo jirani yeye anapayuka kanakwamba husikii; anakuwa akidhani humsikii. Kama familia watoto wanazaliwa hawasikii, wanatakiwa waende hospitali mapema.

Jitihada zinafanywa na Serikali

Kuna suluhu kadhaa zinazofanyika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Madaktari wanapandikiza mpaka vifaa vya usikivu, mashine za kumfanya mtu asikie, hivyo vyote vinaweza kumfanya mtu aboreshe usikivu wake na ubora wa maisha yake na akawa mtu bora zaidi kabla ya mwanzoni.
 
Back
Top Bottom