Februari 6, Siku ya Kimataifa ya kutokomeza Ukeketaji

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Ukeketaji inayoadhimishwa kila Mwaka tarehe 6 Februari, hutoa fursa ya Wadau kuongeza Uelewa kwa Jamii kuhusu madhara ya vitendo hivyo pamoja na kusherekea mafanikio katika utokomezaji

Ukeketaji unajumuisha taratibu zote ambazo husababisha kubadilisha au kuumiza sehemu za siri za Wanawake kwa sababu zisizo za kitabibu na unatambuliwa Kimataifa kama uvunjaji wa Haki Za Binadamu na ukiukwaji wa Misingi ya afya, na utu wa Wanawake

Wasichana waliokeketwa hukumbana na matatizo ya muda mfupi kama maumivu makali, mshtuko, kutokwa damu nyingi, maambukizi, na ugumu katika kujisaidia haja ndogo, pamoja na athari za muda mrefu kama maumivu katika kujamiiana, uzazi na afya yao ya akili.

Kwa mujibu wa UN Women, Zaidi ya Wasichana na Wanawake milioni 200 Duniani kote wamepitia Ukeketaji. Mwaka huu wa 2024, takriban Wasichana milioni 4.4 watakuwa katika hatari ya kufanyiwa Ukatili huu hii ikiwa ni wastani wa zaidi ya Kesi 12,000 kila Siku

Hata hivyo, hali inaonesha kupungua katika Miongo Mitatu iliyopita katika Nchi 31 zenye Data za Uwakilishi wa Kitaifa kuhusu viwango. Kwa sasa, hali inaonesha karibu Msichana 1 kati ya 3 mwenye Umri wa Miaka 15 hadi 19 amefanyiwa Ukeketaji ikilinganishwa na Msichana 1 kati ya 2 katika Miaka ya 1990.
 
Back
Top Bottom