Siku ya Usikivu Duniani: kufikia mwaka 2050, karibu watu bilioni 2.5 wanatarajiwa kuwa na kiwango fulani cha kupoteza uwezo wa kusikia

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Ikiwa leo ni siku ya usikivu wa masikio duniani utafiti wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO lumeonyesha kuwa zaidi ya watu milioni 400 duniani wanahitaji msaada wa kuwezeshwa kusikia, lakini ni asilimia 20 pekee wanaopata vifaa hivyo kutokana na ukosefu wa rasilimali fedha , rasilimali watu, na chuki za kijamii.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Geneva, Dkt. Shelly Chadha, anayesimamia kazi ya WHO juu ya kuzuia uziwi na upotevu wa uwezo wa kusikia, amesema "Ni mtu mmoja tu kati ya watano wanaopata fursa ya urekebishaji wa kusikia kwa wale wanaohitaji,"

Akizungumza kwa ajili ya siku hii inayoadhimishwa kila mwaka Machi 3 amekumbusha kwamba shirika la afya duniani mara kwa mara limetoa tahadhari kwa tatizo hili linaloendelea kukua katika miaka michache iliyopita.

Kuna "vizuizi kadhaa vinavyochangia tatizo hilo”, amesema Dkt. Chadha alielezea, kikubwa zaidi ni uhaba wa kimataifa wa wataalam wa huduma ya kusikia. Miongozo mipya ya WHO inawajibika kusaidia kushinda vizuizi hivyo.

Ulimwengu wenye usikivu finyu wa masikio
Kulingana na takwimu za hivi karibuni za WHO, kufikia mwaka 2050, karibu watu bilioni 2.5 wanatarajiwa kuwa na kiwango fulani cha kupoteza uwezo wa kusikia, na angalau watu milioni 700 watahitaji urekebishaji wa kuweza kusikia.

Zaidi ya hayo, zaidi ya vijana bilioni moja wako katika hatari ya kupoteza uwezo wa kusikia unaoweza kuepukika unaosababishwa na usikilizaji usio salama wa sauti za juu.

Ili kukabiliana na tatizo hilo, WHO inatafakari upya jinsi huduma za usaidizi wa kusikia zinavyotolewa, hasa katika maeneo ambayo rasilimali, hususan rasilimali watu, ni ndogo.

Kwa mujibu wa mtaalam wa WHO kanuni ya msingi ya mbinu mpya ni kugawana kazi miongoni mwa wataalamu wenye mafunzo yanayohitajika na wataalamu wasio na na mafunzo.

"Baadhi ya kazi ambazo kijadi huwa chini ya wataalam waliosoma sana na waliofunzwa kama wataalamu wa sauti zinaweza kufanywa na wasio wataalamu kwa mafunzo maalum," amesema Dkt. Chadha akielezea matumaini kwamba hii itasaidia kutoa huduma zaidi za misaada ya kusikia kwa watu katika nchi za kipato cha chini na kati.
 
Back
Top Bottom