Siku ya Kifo Changu

Siku ya Kifo Changu

Ni kweli kila mmoja wetu atakufa na kwa mtu yeyote aliye makini ni lazima siku moja utajaribu kuimagine siku hiyo ya kifo chako itakuwaje na huku nyuma mambo yatabaki vipi? Lakini ni ukweli usiopingika kwamba marehemu huwa hana mamlaka na mwili wake bali wafiwa ndio wenye mamlaka, hivyo kuna mambo unaweza kuagiza lakini yasitekelezwe!

Mfano: Huwezizuia watu wasikulilie pindi utakapokufa, kilio huja kutokana na hisia za huzuni pale watu wanajaribu kukumbuka katika umuhimu na uwepo wako!

Pia huweziamrisha watu watawanyike masaa 7 tu baada ya kifo chako maana huwezijua utakufa lini na utafia wapi na wakati unakufa je wale ndugu muhimu kama Mama, Baba, kaka,dada, mke, watoto watakuwa karibu nawe? Hawa ndio wataamua uzikwe wapi na uzikwe lini!

Hiyo pesa uloanza kujiwekea nashauri usiiweke bali kama unaishi katika nyumba yako mwenyewe basi tenga chumba maalum, kanunulie sanduku unalotaka kuziwa nalo na vingine vyote uhifadhi humo ili siku ya kifo chako wavichukue na kuvitumia, lakini ukiacha pesa zitachukuliwa na hazitatumika bali michango ya watu ndo hutumika kufanikisha hilo suala, kwanza siku hiyo hata mkeo tu hawezi kabisa kuwa na nguvu hata ya kuinuka kwenda huko benk, chezea kufiwa na mtu wa tegemeo kwa familia kama baba wa familia huwa si mchezo!

Umeandika vizuri sana. Ila kauli ya Marehemu lazima iheshimike. Maagizo yangu yanatekelezeka. Nifikia hewani, that is my destiny , I cannot change

Thank you , je kwa wewe ni mambo gani ukifa leo, huyopenda ufanyiwe?
 
Mimi kifo najua kipo na kitakuja tu...hakina siku saa.
Hivyo Basi...najiandaa na maisha baada ya kifo ambayo naamini yapo.

Nachoomba nife Hali ya kuwa Mola want yu radhi nami.

Kuzikwa nizikwe kwa taratibu za Dini yangu..ya uisilamu.

Hivyo yaani
 
Naunga mkono hoja hapo post #43.

Jukumu lako wewe ni kufa tu mengine tuachie wanaobaki, kulia au kutolia, kupiga bia au kutopiga bia, kutawanyika ama kukaa hilo wataamua wao kulingana na mazingira ya wakati huo.

Umeandika meengi what if ukipotea kwenye ajali ya ndege kama ile ndege ya Malaysia ?

Nikirudi kwenye mada, kifo ni bayana.

Nikipotea that is my destiny , I cannot help
 
Umeandika vizuri sana. Ila kauli ya Marehemu lazima iheshimike. Maagizo yangu yanatekelezeka. Nifikia hewani, that is my destiny , I cannot change

Thank you , je kwa wewe ni mambo gani ukifa leo, huyopenda ufanyiwe?
Sawa mkuu nimekueleza hayo sababu nakumbuka hata mzee wangu aliagiza akifa akazikwe kijijini alikozikwa mama yake mzazi, lakini baada ya kifo chake kamati ya mazishi iliamua tofauti na akazikwa palepale mkoa alipofiwa na hayo yalikuwa maombi ya mkewe kuwa awe jirani na kaburi la mumewe.
Pia mzee aliacha wosia na mgawanyo wa mali, lakini suala la mirathi lilipofikishwa mahakamani, mahakama iliukataa wosia wake na kuagiza kitu tofauti na maagizo yake japo mahakama yenyewe inakiri kuwa wosia wa marehemu unawakilisha kauli yake halisi!
Mimi binafsi ningependa nikifa nizikwe tu kwa taratibu za kawaida kama walivyozikwa marehemu wengine walionitangulia, Lakini zaidi ningependa kila anayenifahamu popote alipo akinikumbuka aseme neno lolote kuniombea pumziko la amani huko nitakakokuwa sababu mimi pia nina utamaduni wa kuwaombea marehemu wote popote kila ninapohudhuria misiba au ibada makanisani!
 
Mimi sihofii kufa...Nina hofu nitakufaje.
Engine failure?(means my body systems are down?)
By accident.
By Illness.
I wish nikufe Bila maumivu yeyote.

Lakini Nakuja kukumbuka siwezi kucontol hayo niliyoyatamani hapo juu.
Haijalishi Ni mara ngapi nitalalama Nitatamani ,
Ila nitafall kwenye Category moja wapo Tajwa hapo juu.
We all live once.
 
Unajitabiria kufa kifo kitakufuata badala ya kumuomba Mungu uishi kwa lile dhumuni lake la kutuleta duniani ili tumuabudu . tunaishi kwa imani na imeandikwa Zab 118:17 sitakufa bali nitaishi ......Muombe Mungu uishi maisha marefu na mazuri umtukuze huku ukisifu matendo yake makuu .
Mungu yupo huko juu....hapa chini Ni sisi.
 
Nasoma lkn sielewi,mtu anakuwa na courage ya kusema sitaki mwili wangu as if ni kitu cha maana sana,ninachoamini mimi ni kuwa there is life after death,hii miili tunayoita ya kwetu na kuipangia masharti itabaki hapa duniani na itaoza,roho zetu ndio zitabaki hai,hii ni either peponi au motoni...
 
Sitaki niwekwe mortuary namwogopa Mshana Jr atanibaka.

Sitaki wakanizike alikozikwa Mr. kule wana roho mbaya maana hata mali zote za Mr. plus nyumba niliyojenga Naye wamenipora,

Wanizike na joho langu la uzee wa kanisa, Bible yangu na kinanda changu.

Siyo lazima wawasubiri ndugu zangu wafike ndo nizikwe acha wakifika wakute kaburi.

Mali nimeshawaambia, kila mtu anajua chake, mali zangu binafsi wafanye watakavyoamua.

Kifo kipo tukubali tu.
Uzikwe na kinanda cha kazi gani sasa? Hicho niachie mimi niwe napiga kukukumbuka.
 
Mie nikutakie kifo chema, ila tunaomba uweke simu ya my wife wako tuwe tunamjulia hali na kumpa co.
 
Baada ya kuhudhuria mafunzo ya FBI na China-MSS, nilielewa kwamba binadamu yeyote mwenye AKILI kubwa ni lazima ailazimishe akili yake kukikubali KIFO.
-
Tukiwa na training team ya China MSS, swali la kwanza kuulizwa ni; " Do you fear death ? My honest answer, as we were taught never to lie, was Yes, I do.
-
Tulijibiwa kwamba How could that be possible; you fear something you never had any experience before? They said, is there any person in all our recorded history ever experienced The Go and Return?
-
I said, I don't know!
-
Wakatuambia, ili mjifunze and to serve the world, kwanza you guys have to accept death as the matter of TRUTH. Pili, No one knows the TRUTH but we think we do. We are all living in myths and fantasies of the past just to secure our insecurities.
-
It is one of those days that I came to realize that many people have been dying without living the life . Ni wachache sana wamefanikiwa kufunua BUSWATI na kuona the glimpse of life. Kibaya zaidi haya mambo you can not be taught. Verily, you have to check it by yourself. Curiosity never killed the Cat. THINK!
-
Siku ya KIFO Changu

1. Sitotaka mwili wangu kusafirishwa kupelekwa Kilimanjaro Unless nimefia NAMIBIA, kitu ambacho siamini hivo, siku zangu zikikaribia, for sure I will know, nitarejea nyumbani. Nitapenda kuzeekea Dar es salaam, mji ambao ninaupenda sana.

2. Nimefungua death account kila mwezi naweka dola 100 kwa ajili ya kugharamia maziko yangu, I have documented that on my Diary. sitaki yeyote atoe senti yake kwa maziko yangu.

3. Sitohitaji watu wakae matanga, nikishafukiwa, kila mtu aondoke kwenda kufanya yanayomuhusu.

4. Masaa 7 Tangu kifo changu niwe nimeshazikwa, naamini nitakuwa sijaanza kutoa harufu ya kuliwa na bacteria.

5. Kaburi langu lisijengewe wala kuandikwa jina.

6. Nisivikwe nguo yoyote zaidi ya kitambaa kitakachohifadhi tupu zangu.

7. Sitoruhusu kwa mtu yeyote aliyelewa kuhudhuria maziko yangu na wala kwenye maziko yangu sitoruhusu pombe

8. Sitopenda nyimbo zozote zipigwe wala mtu yeyote kuimba. It is the moment of silence to honor my existence

9. Haitoruhusiwa Kulia. Kwanini ulie? Kwani hukuwahi kujua kwamba tumezaliwa ili tufe, jiandae kwa sababu for sure Utakufa.

10. Ndugu yoyote hausiki kwenye Mali zangu kwa namna yoyote ile , mali zangu ni za watoto wangu na mke wangu tu , I have documented that on my diary, Bank accounts and legal issues.
-

Je, siku ukifa, ungependa vitu gani usifanyiwe kwenye maziko yako? na je ungependa ni nani awe mrithi wa mali zako?

Thank you and Rest In Peace to all the humans who have stepped into the truth of death. To all the humans who Have died due to Covid-19, and for those who are continuing dying due to COVID -19.

Chukua Tahadhari. Akili za kuambiwa, Changanya na zako.
When i die, bury me inside the Gucci store.

When i die, bury me inside the Louis store.

Haya ni maneno yake mwenyewe 2 chain katika wimbo wake wa birthday song
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom