Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,036
Shirika la ndege la ATCL hatimaye limechukua hatua ya makusudi ya kuwazuga Wabunge kuanzisha safari za kwenda Dodoma kuanzia wiki ijayo ili kuoanisha na bajeti ya Wizara ya Miundo Mbinu. Lengo kubwa la kuzuga huku ni kuhakikisha kuwa wabunge hatimaye wanaipitisha bajeti hiyo pasipo "kelele" nyingi ili hatimaye wapatiwe Shs. Bilioni 7 ambazo wameiomba serikali kuweza kujikwamua na madeni.
Endapo bajeti ya Miundo Mbinu itapita bila kelele na hatimae hela nyingine kumwagwa tena ndani ya shirika hilo ambalo linajiendesha kwa hasara likiwa na deni la zaidi ya Bilioni 30 basi watanzania watashuhudia uzugaji uliofanikiwa kupita yote.
Viongozi mbalimbali wa ATC wanaelekea Dodoma ili kuongeza nguvu ya uzugaji ili kuwalainisha wabunge.
wanachoogopa zaidi ni uwezekano wa wabunge kuagiza kufanyika kwa special auditing au independent auditors kufika hapo bila taarifa na kuanza ukaguzi. Hilo wakuu hao wameapa halitatokea.

Last edited by a moderator: