Siku wabunge walipozugwa wakazugika!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Shirika la ndege la ATCL hatimaye limechukua hatua ya makusudi ya kuwazuga Wabunge kuanzisha safari za kwenda Dodoma kuanzia wiki ijayo ili kuoanisha na bajeti ya Wizara ya Miundo Mbinu. Lengo kubwa la kuzuga huku ni kuhakikisha kuwa wabunge hatimaye wanaipitisha bajeti hiyo pasipo "kelele" nyingi ili hatimaye wapatiwe Shs. Bilioni 7 ambazo wameiomba serikali kuweza kujikwamua na madeni.

Endapo bajeti ya Miundo Mbinu itapita bila kelele na hatimae hela nyingine kumwagwa tena ndani ya shirika hilo ambalo linajiendesha kwa hasara likiwa na deni la zaidi ya Bilioni 30 basi watanzania watashuhudia uzugaji uliofanikiwa kupita yote.

Viongozi mbalimbali wa ATC wanaelekea Dodoma ili kuongeza nguvu ya uzugaji ili kuwalainisha wabunge.

wanachoogopa zaidi ni uwezekano wa wabunge kuagiza kufanyika kwa special auditing au independent auditors kufika hapo bila taarifa na kuanza ukaguzi. Hilo wakuu hao wameapa halitatokea.
 
Last edited by a moderator:
Hii sasa inakuwa kama movie. ATCL ni shirika la umma, linahitaji bil 7 kujikwamua inakuwa mzozo.Shirika la binafsi lilihitaji bil.3 wamepewa mara moja bila hata ya kulazimika kumuomba mbunge yeyote aunge mkono.where are our priorities?
 
atcl wasipatiwe pesa ya mtanzania bila ya kupelekwa special auditors kwanza kukagua mahesabu ya shirika hilo.
kabla ya kupewa pesa hizo tunahitaji kujua ilikuwaje hata atcl ikafikia kuwa na madeni ya bilioni 30. na kama kumepita ubadhirifu tunataka kuona mtu anawajibishwa kwanza ndio pesa ya mwananchi itumike.
ni aibu nchi kuwa hakuna vifaa vya hospitali lakini kila leo shirika linalotumiwa na watanzania wachache kupewa pesa kila siku.
 
Hapa sio wabunge wanazugwa, ni watanzania kama kawaida. ni shirika gani la umma linaloweza kuomba au kubembeleza lisifanyiwe auditing iwe special au ya aina yeyote ile.

ni muhimu sana kabla ya hizo fedha kutolewa waangaliwe kwa undani ili wajue mapungufu yao na wajirekebishe kama kweli wanataka kuondokana na madeni na utendaji mbovu.
 
Hii sasa inakuwa kama movie. ATCL ni shirika la umma, linahitaji bil 7 kujikwamua inakuwa mzozo.Shirika la binafsi lilihitaji bil.3 wamepewa mara moja bila hata ya kulazimika kumuomba mbunge yeyote aunge mkono.where are our priorities?

Zemarcopolo,
Udikiteta ulio fanywa wa kuchukua hela zetu kumuhonga muhindi masikini aliyekuja na briefcase yake tupu akijifanya muwekezaji, na sasa inaanza kujazwa mabilioni, hauhalalishi kuendelea kupoteza hela zetu kwa ATC inayo ogopa kukaguliwa!

Kuna shida gani hapo?, obvious, hizo bilioni saba wanazo taka si kwa jili ya shirika hilo bali ni kwa ufisadi wao huo huo wataenda zigawanya kama destrui yao na shirika litakufa hivi hivi, likisha kuwa taabani watakuja na lugha za kulinusuru tunahitaji muwekezaji then wanampa kwa bei ya mil 700 ambayo atalipa 70 mil. na kuendelea kupeta tena mkataba ukihitaji alipwe kila siku sijui wanaita capacity nini... grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr!!

Inatia hasira sana!
 
Hii sasa inakuwa kama movie. ATCL ni shirika la umma, linahitaji bil 7 kujikwamua inakuwa mzozo.Shirika la binafsi lilihitaji bil.3 wamepewa mara moja bila hata ya kulazimika kumuomba mbunge yeyote aunge mkono.where are our priorities?

Two wrongs don't make one right! Na hata hivyo ATCL has been around for decades and is a bottomless pit, throwing good money at bad is not the solution. Just dissolve the whole charade. Wacha mashirika binafsi wajijenge. Kwani umesikia wapi kwamba USA ina national carrier? Unafikiri walishindwa au wameona siyo busara? Na EU yenyewe imeamua kubinafsisha na kuachana na biashara ya airline, hao waitaliano wameng'ang'ania angalia Alitalia ilivyofilisika na kutia aibu. Airline is business siyo masuala ya mashirika ya umma. If ATCL can be free of politics na ikajiendesha yeneywe say after 2 years well and good but that is not going to happen when politicians think that national carrier equals private jet also akina Mattaka et al wanajichukulia chao mapema!
 
I was right.. and at least wabunge walizugwa, wakazugika... now I know our leaders are the reflection of ourselves!
 
ATC hawana hulka ya responsibility na financial discipline hata wakipewa billion 100 bado sidhani watafanya chochote, kwanza ubiwa wao na Oman airways ilikuwa ni kichekesho tu, hufanyi strategic alliance na mchovu hata siku moja, ili mfe pamoja au vision yenu ni ipi?
 
Two wrongs don't make one right! Na hata hivyo ATCL has been around for decades and is a bottomless pit, throwing good money at bad is not the solution. Just dissolve the whole charade. Wacha mashirika binafsi wajijenge. Kwani umesikia wapi kwamba USA ina national carrier? Unafikiri walishindwa au wameona siyo busara? Na EU yenyewe imeamua kubinafsisha na kuachana na biashara ya airline, hao waitaliano wameng'ang'ania angalia Alitalia ilivyofilisika na kutia aibu. Airline is business siyo masuala ya mashirika ya umma. If ATCL can be free of politics na ikajiendesha yeneywe say after 2 years well and good but that is not going to happen when politicians think that national carrier equals private jet also akina Mattaka et al wanajichukulia chao mapema!

hapa nimekupata, tatizo wanaoperate in confidence kuwa should any thing go bad serikali itawaokoa hiyo ni biashara kichaa sasa. Sina uhakika hata wana five year plans kuwa wanataka kuwa wapi, usanii mwingi tu.
 
Kesho si Waziri Mkuu anapata yale maswali ya papo kwa hapo... labda kuna mbunge anaweza akajitolea kumuuliza "what happened to the planes"... na kama wanapata abiria wa kutosha.... (is it worthy it?)
 
Kuna Kamradi Kapya Nimekasikia Kameanzishwa Na Lawyer Wao!!!natafuta Uhakika Alie Uko.....kuna Kalawyer Kao Pccb Wanakafwatilia Kamekuwa Kakifanya Mradi W Akula Pesa Za Atc Kwa Kushirikiana Na Majaji Na Makampuni Ya Wanasheria....nimedokezwa Kuna Vijikesi Kama 3 Jamaa Wameshinda Kajamaa Kakishirikiana Na Mmoja Wa Ofisa Wa Hapo Hr Wamekuwa Wakiappeal Zaidi Ya Mar Tatu Ili Kula Hela Za Kampuni!!!!1jamani Mkuu David Hufumbuki Hata Kwa Wizi Wa Kimachomacho Kama Huo Jamani!!!!embu Nikamshtue Mzee Wangu Utouh Aje Uko Inaonekana Hela Zinaliwa Ovyo Sana!!!!
 
Kwa nini serikali isiwe na utaratibu wa kuwa na Town Meetings ili kuwashirikisha wananchi husika na miradi ya maendeleo ya nchi yetu.......ili kupata maoni mbali mbali kabla haijatekelezwa?.................sehemu nyingi nilizopita/ishi huu utaratibu upo na ni mzuri......na unakuwa spearheaded na wawakilishi i.e. MPs
 
makosa yalianza zamani sana tangu Mkapa alipoamua kuigawa ATC kwa SAA

Ni kweli hasa hicho ndo kiini cha mporomoko wa ATC, lakini bado way out haiwezi kuwa kuendelea kuwa miminia mabilioni yetu wajanja wachache wakaendelea kuneemeka nayo bila hata kuleta badiliko lolote la kulifufua shirika!
 
I was right.. and at least wabunge walizugwa, wakazugika... now I know our leaders are the reflection of ourselves!

Msemo huu haukunipendeza nilipousikia mara ya kwanza. Inawezekana nimeshindwa kuuelewa?

Bwana mmoja mwenye upeo mkubwa tu alitamka siku moja "Bongo... maisha ni usanii!"; ...nilimshangaa sana. Nilitegemea mtu limbukeni ndiye angeyatamka haya. BOY, how naïve I was, nimetoka huko mikoani nisijue maisha ya jijini yalivyo.

"Our leaders are the reflection of ourselves!"
Eventually sote tutakuwa wasanii. Je: ugonjwa huu tumekuwa nao ama tumeambukizwa? Chanzo chake nini? Kwa nini Bongo tu?

Note:
"Our leaders are the reflection of ourselves!"
"We are the reflection of our leaders!"

There is no difference at all or is there?

.
 
Back
Top Bottom