Baba Joseph17
JF-Expert Member
- Jul 15, 2013
- 9,518
- 9,792
Kuna day nimekula mtungi sana kuanzia mida ya asubuhi hivi saa nne. Nililewa sana asee kiasi kwamba mpaka saa tisa hivi alasiri nilifanya kubebwa nipelekwe home.
Nikaingia chumbani nikavua nguo zote nikalala, mida ya saa 12 jioni mkojo umebana nikasema ngoja nitoke nje nikakojoe.. Ile natoka na wenge langu uchi wa mnyama kumbe watu wamekaa nje bi mkubwa na mashangazi walikimbia ghafla sikuona mtu nilirudi ndani kwa aibu hata mkojo sikuusikia tena.
Niliona aibu sana nikawa nafanya kuamka asubuhi kabla ya wote nasepa kama week hivi. Nikaona bora nihame home tu nisije kuzua mengine. Nikakaa mda sana bila kula mtungi. Saivi nakunywa kistaarabu
Sent using Jamii Forums mobile app
Pole sana nimecheka story yako inanikumbusha mtu mmoja miaka ya tisini alikuwa analewa pombe akirudi nyumbani mlango anafunguliwa na mke wake hafu jamaa anamkubatia mke mabusu nk, sikuyasiku kagonga mama mkwe kaja kufungua sasa jamaa mazoea yale akamkumbatia na kumbusu mama mkwe, jamaa alivyoambiwa asubh yake alipotea nyumbani kama mwezi na akaacha pombe hadi Leo Sent using Jamii Forums mobile app
