Siku niliyotamani kiama

Siku niliyotamani kiama

Daah utoto bana, kipindi nipo form 4, nilikuwa nimechukua rafiki zangu wawili tumeeka kambi home, nilikiwa ninaishi na bibi yangu, wazee wapo dar.

hiyo siku bibi akaniaga anaenda marangu, atarudi kesho yake nimebaki na beki tatu na wanangu tukaingia pub alberto, nikarudi na demu tukajisevia, cha ajabu wote tulikuja kushtuka saa 6 mchana tumechoka, demu mwenyewe alikuwa amevaa nguo za hovyo na nnasikia sauti bibi amerudi na yupo na bro wake wanaongea sitting rum, demu kakurupuka anataka kuondoka haelewi na njia pekee ni kupita sebuleni, na kwa zile kelele bibi akajua huku kuna mtu wa ziada akaanza kuniita...nikatoka akauliza nipo na nani nikamwambia mwanafunz mwenzangu jana tulikuwa tunasoma, bana akaniambia muitee...hapo ndipo nilitamani niwe ndotoni namletaje yule malaya na anaishi mitaa ile ile nikaona nizame chumbani kwake kwenye kabati chini kabisa nikavuta kanga nikampelekea demu avae, tukatoka

ha ha kumbe zile kanga za bibi ni za TANU 1961, bibi kapanic kauliza hii kanga ya nani, nikamwambia yake kaja nayo, hapo ndipo nilipomkorofisha zaiidi, kanyanyua simu kapiga kwa mshua, hata wiki haijapita na nyumbani nikahamishwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii huwa inatokea mara nyingi sana nikiwa chuo.kwa anaesoma sheria ataelewa zaidi. yani unasoma majina ya kesi fresh unakalili sasa kesho kufika kwenye paper,umesahau unachokumbuka ni material fact tu. Yani utatamani ulie na swali unaambiwa usupport na case na huna hata moja.
 
Ee bhana eeh hapa duniani huwaga kuna nyakati ngumu sana ambapo unaweza tamani kiama kitokee utoweke kuliko fedhedha au hali flani ya aibu na maumivu yanayokukuta .

Leo nimekumbuka tukio moja ambalo siwezi lisahau maisha yangu yote ,nilikuwa advance enzi hizo miaka kadhaa ilopita ticha wa kemia akasema kutakuwa na test(Physical chemistry) test enyewe ni swali moja tu la calculation na mfano wa hilo swali tushafanya na nimeelewa vizuri tu ,basi buana siku kaa mbili hivi kila mtu anajiandaa .

siku ya mtihani ikafika swali likaja lile lile hadi data hazijabadilika lina marks 25 na lipo moja tu,tukagawiwa karatasi tukapewa dakika tano tusome swali ,nilipoliona swali nikafurahi pia mana naona kabisa 25 yote nachukuwa ha ha

Nikachukua karatasi nikaandika jina ile nashika tu peni nianze kuandika data ,akili ikafuta kila kitu hata kucollect data siwezi yani sielewi ,nikawa najaribu nikumbuke basi hata fomula itanisaidia kucollect data nikashindwa pia kukumbuka fomula ,kumbuka hilo swali nalijua na nimelisoma vilivyo.

Dah nikawa naangalia pembeni je wenzangu wanafanya? kiukweli darasa nzima kila mtu alikuwa bize kukokotoa isipokuwa mimi tu.

Teacher anapita anaangalia jinsi watu wanafanya naona anapita kwangu mimi nimeandika tu jina huku zishatangazwa zimebaki dk 15 tu time iishe.

Nikainama juu ya dawati nikawa nasali Mungu anikumbushe kanuni ,kiukweli sikukumbuka ,nikakemea pepo la usahaulifu wapi mwisho wa siku nikabadili maombi ,nikawa natamani litokee janga lolote tetemeko au kiama woote tutoweke tu kuliko vile majibu yanavyoenda kuwa mimi nina 0/25 wenzangu wooote wana 25/25

Maombi hayo pia Mungu akuyajibu ,nikasikia pens down ,tukakusanya mimi nimeandika jina tu.

Kila mtu anafuraha vicheko na kumshukuru teacher kwa ile feva ,ilibidi niende tu bwenini kulala

Majibu yalitoka robo tatu ya darasa ilipata 25/25 mimi nikapata 2/25 hizo 2 niliwekewa tu kama zawadi ya kuandika jina na kuaribu karatasi ha ha.

Kitu gani kimewahi kukupata kama mimi???
#TIRIRIKA
#TUNATOKAMBALI

Sent using Jamii Forums mobile app

Kaka pole sana, mimi nakumbukua nilikua nafanya Pure Math form 6 kwenye swali la 1 paper 1, huwezi amini nilishindwa nianzie wapi wakati ndio huwa swali langu la 1 kila siku
 
Hivi vitu ni kawaida mkuu, hutokea pia kwenye oral interview, unajikuta mzee unaweza Hata kusahau jina lako.. Wale panel members huwa wana enjoy saana

daaahh juzi tu imenitokea jamaa walikua wanacheka afu najua kabisa wanachouliza ila kujibu unashindwa
 
Kuna siku kaja Mgeni nyumbani na Gari lake Kaweka Funguo Mezani mimi huyo si nikachukua Funguo nikaendeshe Gari duh niligonga Gari la watu Mbele na Nyuma Vibaya mno Nikagonga Ukuta Nusu Nidumbukize Gari Chooni Dah Nilihisi naota

Sent using Jamii Forums mobile app
We jamaa umenichekesha sana stress zote zimeisha...thanks sana hahahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm juzi tu hp tulikuwa na dua nyumbani cc ni waislam ss sura zilikuwa nyingiiiii kila mmoja akapewa zke ww utasoma sura flani ziwe 40 yule atasoma sura flani ziwe 60 na kadhalika mm nilipewa sura nyepesiiiii na nnaijua hainisumbui hata kdg coz nilipita madrasa bc umefika muda wa kuanza kusoma bakhti nzr tunasoma kwa pamoja ila kila mmoja anasoma chake bc mm nikatembelea nyota zle sauti za wenzangu wanaosoma sikusoma hata sura moja yaani kila nikijaribu naishia "bismillahi" memory haiji kabsaaaaaa cjui ni nn huwa kinatokea!

Sent using Jamii Forums mobile app
Rahiman rahim.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa twende ukweni kutoa Mahali sasa kwa shy nikaona nile tungi la kutosha ili nisone shy daa si nikazidisha ikabidi msindikizaji wangu anishauri nile ndizi mbivu ili harufu itoke si unajua Serengeti ilivyo.Nikanunua ndizi nikaona mbona bado si akashauri ninunue packet ya maziwa Lato fresh milk ninywe kukata kilevi aisee kumbe nimeharibu tumbo likaanza kuunguruma gesi tumboni ikajaa mida ikafika mezani tukakaa mezani aisee Shuzi si likanitoka tena la sauti kama talumbeta kubwa aisee nilitamani kipindi cha kukabidhiana mahali kiishe mapema aisee.NIMEJAMBA MBELE ZA WAKWE

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahah we jamaa umezidi kunichekeka my ndugu hahahaha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitosahau siku nilipopigana na private kambini baada ya kunihisi namkula manzi aliyemchomolea enzi nikiwa kuruta
 
Nakumbuka nikiwa msingi nilikuwaga mtundu sana. Ila pamoja utundu wangu nilikiwa kichwa darasani. Kawaida yangu ni kuchelewa shule mara nije nikute mwalimu anafundisha mimi nazama najifanya nimetoka chooni,Siku zingine nikija napitia dirishani. Siku ya siku mzee wa kuchelewa ikanilipukia.

Nimetoka zangu home saa mbili nkamwona mwalimu kule shuleni anagawa mboko tu. Nilichoamua haraka haraka nikachukua madaftari nkampa mwanafunzi mwingine aliyechelewa pia. Mwanafunzi mwenyewe kumbe niwa kitongoji nyingine. Simjui ndio mara ya kwanza kumwona halafu isitoshe ni darasa la chini nilijua tu ni la kwanza wakati mimi niko la tatu. Nilimkabidhi kwa moyo nikijua itakuwa rahisi kumpata.

Mimi nkajiendea hospitalini na siumwi nkamdanganya docta naumwa na tumbo kumbe nilikuwa nakwepa fimbo. Nimefika kwa dokta kama mnavojua wale wa zamani kanipima pima kwa kuniwekea kitu kifuani uzuri kanipa daftari kaandika tu mwandiko wake wa kishua tu kama kawaida ya mdokta. Nimerudi shuleni nimefanikiwa ila sasa mtoto kumbe hakuwa hata wa darasa nililodhani sijui. Nimeingia la kwanza saa mwalimu hayupo naangalia watoto kama zezeta sioni mtu du nilichoka na huku nikikumbuka mdingi ni mtu sio kidogo kwa mboko. Nilitamani dunia ichimbike nizame. Nilienda dasani nikawa napewa madaftari ya wenzangu nazuga naandika saa ticha akiingia. Nishuka kielimu mno kwa sababu ya mastres tatizo mdingi nilikuwa namwogopa sana. Mwishoni baada ya miezi kama 2 nkashangaa mdingi amenipa madfari 7 nilifurahi japo begi langu bado halikuisha kichwani na moyoni maana ilikuwa na madaftari yaliyokuwa yamejaa vema na mia kwa mia na materio kibao. Mwishoni mwa kumaliza darasa ndo akatokea jamaa wa darasa ndo akaniambia kuna mtoto ana madaftari yaliyoandikwa majina yangu huko kitongojini kwao. Nilifurahi sana tukafuata nkaenda nae kwenda kufuata.

Kisa cha pili tumeambiwa na kiranja tukafanye usafi tugama. Akaenda kutushtaki. Kesho yake mwalimu huyo saa nne katuita majina akaanza kutuambia tulale. Wa kwanza alipewa marungu ya kutosha. Wa pili hivyo wa tatu hadi wa mwisho wakata yao du mimi nilikuwa naomba tu ardhi ipasuke nizame nisipate hayo maraungu. Mwishowe akili ikaniambia dawa ni mbio tu. Ilipofika zamu yangu nilitimua shule nzima wakaambiwa wanifukuze.Nilikimbia huku nikizomewa nilipoingia shambani kwa mtu aliyepita yake kama nikuotesha mahindi au maharage hakuna haja ya kuchimba mashimo.

NliIizidiwa nkashikwa ila nilipekwa kwa huyo mwalimu nkakuta ndio anafundisha watoto wameingia madarasani. Nlipofukishwa tu hata haja niuliza swali nkamwambia mwalimu nifute shule. Ndipo akasema nipelekwe kwa mwalimu mkuu nilipofika nkamwambia mwalimu mkuu nifute shule du mwalimu mkuu alichoka akaniambia nenda darasani kesho umwite mzazi. Ukweli sikumwita ikawa kwenye somo la huyo mwalimu alikuwa anafundisha kilimo akija tu anambia toko nje. Ilikuwa kero sometime ananisahau ila alikuwa akiingia tu ni mafadhaiko hadi mwisho masomo yote nafaulu ila lake lilikuwa linanipa 0 tu.Kweli dunia hadaa mpaka sasa sisahau visa vya msingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa twende ukweni kutoa Mahali sasa kwa shy nikaona nile tungi la kutosha ili nisone shy daa si nikazidisha ikabidi msindikizaji wangu anishauri nile ndizi mbivu ili harufu itoke si unajua Serengeti ilivyo.Nikanunua ndizi nikaona mbona bado si akashauri ninunue packet ya maziwa Lato fresh milk ninywe kukata kilevi aisee kumbe nimeharibu tumbo likaanza kuunguruma gesi tumboni ikajaa mida ikafika mezani tukakaa mezani aisee Shuzi si likanitoka tena la sauti kama talumbeta kubwa aisee nilitamani kipindi cha kukabidhiana mahali kiishe mapema aisee.NIMEJAMBA MBELE ZA WAKWE

Sent using Jamii Forums mobile app
Haaaaaaa mkuu, poleee sanaaaa
 
Sitosahau siku nilimwingiza Mwanamke room kwangu nile mzigo ambapo ili nifike room kwangu lazima nipite coridor ya kwa Mama. Ebana nikategea Mama kaondoka mtoto akazama ndani kama kawaida yangu sijawahi kuacha viatu nje hata siku moja nikiwa kula papuchi.

Nimekula papuchi nimemaliza nashika simu nakuta missed call 12 za Mama hapa nliisi kufa nikaingia bath room uzuri ilikua ni ndani kwa ndani nikanawa uso maana niliambiwa eti ukila mzigo jicho linakua jekundu kama nyanyaa

Nikampigia Mama akanambia nipo nje hapa maini yalivurugika sana tumboni nikafungua mlango akanangalia kwa asira sana machoni akanambia umekula chakula Kwa ukali, nikajibu nilikua nimelala . Ebana akanambia nenda shop kanchukulie vocha nlivoenda narudi nakuta mama na binti wako room kwangu nliona aibu sana binti alilia sana.

Ila mama aliyamaliza kwa ushauri mzito mno! Now days siishi kwa mama naendaga kumsalimia tu. Mtoto kwa mama akui
Duuuh, hatarii binti alilia kwasababu gan mkuu?
 
Duuuh, hatarii binti alilia kwasababu gan mkuu?
Haha mkuu nilikuta kikao kashaekewa hivyo mambo yalikua sio poa aibu tupu yani. Ila Mama mwepesi kusamehe na kusahau now ananiambiaga tu nikifika age 29 nitafute mtoto
 
Ilikuwa twende ukweni kutoa Mahali sasa kwa shy nikaona nile tungi la kutosha ili nisone shy daa si nikazidisha ikabidi msindikizaji wangu anishauri nile ndizi mbivu ili harufu itoke si unajua Serengeti ilivyo.Nikanunua ndizi nikaona mbona bado si akashauri ninunue packet ya maziwa Lato fresh milk ninywe kukata kilevi aisee kumbe nimeharibu tumbo likaanza kuunguruma gesi tumboni ikajaa mida ikafika mezani tukakaa mezani aisee Shuzi si likanitoka tena la sauti kama talumbeta kubwa aisee nilitamani kipindi cha kukabidhiana mahali kiishe mapema aisee.NIMEJAMBA MBELE ZA WAKWE

Sent using Jamii Forums mobile app


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilinitokea hiyo o level kny paper ya kemia ya practical ktk mtihani wa necta,sikufanya kitu kwa kweli,na hiyo ndio ilipelekea nisipate div one,nikaishia kupata div two ya kwanza,hata hivyo namshukuru mungu sikupata F kemia bali D,inaonekana paper ya theory ndiyo iliyonibeba
yalinikuta na mimi hayo kwenye kemia practical o level
 
Back
Top Bottom