Muda mwingine nashindwa hata kulifafanua hili neno kwa hapa kwetu tz, muda mwingine unakuwa huna nia ya kutoa ila mazingira yanakulazimu ufanye hivyo, binafsi nimeshatoa rushwa mara tatu na zote kwa askari, mara mbili kwa wa usalama barabarani na moja kwa wale wanaoitwa tigo wanaozurura na pikipiki.
Sisemi rushwa ni nzuri ila nataka kusema tu kuwa mara zote nilizotoa ilinisaidia kufanikiwa kilichofanya nikatoa rushwa.
Maoni yangu.......Rushwa sio nzuri hata kidogo maana kwanza ni ubinafsi na roho mbaya, nachukia ninapoitoa.......hembu fikiria unafika hospital unatoa rushwa utibiwe pengine haraka kuliko wale uliowakuta kwenye line, unajisikiaje ktk hali kama hiyo?
Hii maana yake ni mwenye nguvu kumkandamiza mnyonge, unajisikiaje wewe kama polisi unamkamata mtu na kumlazimisha kuwa bidhaa alizonazo si za uhalali, pamoja nakuonyeshwa risiti lakini unamsumbua na kumpotezea muda mpaka upewe chochote, hii si sawa lkn kwa Taifa letu lilipofikia hakuna hata anayejali na rushwa imekuwa sehemu ya maisha yetu, tunatoa na kupokea kila kukicha.......wakubwa walitaka kuihalalisha kwa kuibatiza izaliwe upya na kuitwa TAKRIMA.