Siku Muhimu zenye mafundisho Maishani

Siku Muhimu zenye mafundisho Maishani

Lighton

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2019
Posts
2,097
Reaction score
3,542
Wakuu kuna moments huwa binadamu tunazipitia, zinakuwa ni nyakati ngumu zinazokupa mzigo kichwani kias kwamba unakata tamaa kabisa unajiambia moyoni hapa sitoboi dadek, ila unajipa moyo ngoja niendelee kujaribu ikishindikana basi.

Halafu unaona mambo yanaanza kuclick, unaanza kuelekea kwenye kusolve, mara umesolve, unajiuliza niliwezaje?

Kwa upande wangu mimi kuna visa kama viwili

Kisa cha kwanza........ Niliwahi kupata msala mzito, Nilipata majanga nikapelekwa mahabusu, pesa ilikuwa inatakiwa Mingi sana halafu kwenye familia yetu mimi ndo kidogo nilikuwa na mwelekeo wakati huo, Na msala ulikuja ghafla baada ya kutoka kulipa bills flani. Aisee nilipambana sana kipindi kile, Nilikuwa na marafiki wengine maaskari, nwingine mbunge nk Lakini wala sikuona msaada wowote, Namimi nikiwaga busy kupambania jambo langu, wewe hata usipoonyesha ushirikiano mimi lazima nitapambana tu. Kiufupi nilifanikiwa na nilisave date, Ni siku muhimu sana kwangu.

Kisa cha pili......... Niliwahi kufall in love kwa binti flani hivi, Demu alikuwa mkali, nakumbuka jamaa walifukuzia sana kitaa, ila mimi nilifanikiwa kumnyakua yule binti, Demu alidai kwamba yeye ni bikra so aliniambiya kwamba ili tusex lazima nimuoe kwanza, Dah ilikuwa changamoto sana Nikimcheki mtoto mkali, Halafu jamaa wanamfukuzia, nikajisemea moyoni huyu mtoto siku watakuja kumtafuna, kumbe nilikuwa najisumbua bure, Sikuwa na pesa ila demu nilimpa karibia kila nilichokuwa nacho, mpaka niliingia madeni, nilifikiria kumuhudumia, na kufanya maandilizi ya ndoa at the same time, ilikuwa ngumu, nilijitahidi mwishowe aliishia kunivunja nguvu.

Maandiko yanaasa tuishi na hawa viumbe kwa akili mnoo, Niliacha kumuhudumia, nikawa nafanya maisha yangu, Nilijua tu siku moja mtu mwenye pesa mingi anaweza kumnyakua siku moja, na kweli siku ya siku demu alinyakuliwa na Nigga flani hivi, ambaye alikuwa kajipata.
Ni moment pia ambayo ilikuja kupita na kunipa funzo kuhusu hawa viumbe.

Wakuu miongoni mwa Tarehe ambayo nimeipa kitu spesho, ni ile siku niliposomewa gharama ya majanga niliyopata nikiwa sina hata mia ndani.

Wakuu tusave date, tukijifunza kwa kutorudia makosa tutafanikiwa.
 
Back
Top Bottom