Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau, amani iwe kwenu.
Katika viongozi wa kisiasa waliofanikiwa kugroom wanasiasa vijana wa kike basi ni huyu Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikael Mbowe. Ni Mbowe ndiye aliyemuibua Halima James Mdee kusikojulikana. Ni Mbowe ndiye aliyefanikiwa kumfanya Joyce Mukya kuwa mbunge wa viti maalum kwa awamu mbili mfululizo. Ni Freeman Mbowe ndiye aliyemfanya Esther Matiko akakubalika na kung'ara kisiasa.
Namkumbuka sana FAREEMAN MBOWE alivyomtengeneza Jesca Kishoa hadi kuwa mhimili mkubwa kisiasa. Hata ndoa ya Kafulila na Kishoa iligharamiwa kwa kiasi kikubwa na Mbowe ili kumfanya mwanasiasa huyo awe na utulivu wa kisiasa. Mnakumbuka ujio wa Bulaya CCM? Ni nani aliyefanikisha kama si Mdee na Mbowe?
Madam Wema Sepetu nusura aukwae ubunge wa viti maalum. ilikuwa ni jitihada zake ili kuhakikisha CHADEMA inakuwa na wabunge vijana wenye mvuto katika jamii. Majadiliano yalikuwa yanaendelea baina ya Mbowe na Mange Kimambi ili 2020 autwae ubunge wa viti maalum.
Mpaka hapo naamini tunakubaliana kuwa wabunge wengi wa viti maalum na hata wa kiume kama akina John Mnyika ni uzao wa Freeman Mbowe. Siku Mbowe akaamua kujiengua kwenye chama hicho au hata kuwa nje tu ya uongozi wa CHADEMA, yupo mbunge wa viti Maalum atakuwa na ujasiri wa kubaki? Kama yupo basi nitajieni nimtunuku nishani ya ushujaa.
Nawasilisha