Siku 60 za Rais Samia madarakani: Tunakushukuru sana kwa uongozi wako makini, hakika umerejesha tumaini na furaha

Siku ya tatu mfumo wa kununua umeme wa TANESCO nchi nzima uko "dawn" wazazi ambao vitoto vyao njiti vipo kwenye incubators jiandaeni kubeba "maiti" vitakufa tu, hospitali nyingi hasa za umma hawana genereta za dharula...
Na izo chanjo zenu za covid sijuhi tumuombe Mh. Uhuru Kenyatta atuhifadhie mana huku hakuna uhakika kabisa wa usalama wake!
 
bado anatakiwa awe mfuatiliaji zaidi kama alivyo kuwa mtangulizi wake,

Ufuatiliaji kwa umakini mambo yote yenye masilahi kwa nchi, mfano kama tulivyo ona Hayayi Maguguli alivyo baini makinikia yaliyo kuwa yanasafirishwa yakidaiwa kuwa ni mchanga.
hapa lazima awe na wasaidizi wenye utiiiiiiii na uadilifu ktk kila idara za serikali,kuanzia juu mpaka chini vinginevyo wapo baadhi ya viongozi wajanja watakao mdanganya na kumpumbaza vizuri sana.

Rais peke yake hawezi kutimiza na kutekeleza matarajio ya wananchi bila uongozi imara kutoka kwa PM,

PM aongeze ufuatiliaji na kuchukua hatua haraka, kwani tumeona ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma ktk halmashauri nyingi.

Usimamizi na ufuatiliaji bado hatujaona.
 
Ushauri wako naamini ataufanyia kazi
 
Huh... hakikisha?

Did you really mean that?

Hakikisha?

Hakuna chochote ninachopaswa kuhakikisha hapa.

Siwajibiki kuhakikisha wala kutohakikisha lolote.

Unaweza kuendelea kulitetea JIZI la msoga.
Eventually nimejua kumbe unapambana ukiamin juu ya conspiracy theories!! Bas kwa mantiki hiyo hutendei haki jukwaa hili kama utashindwa hata ku defend hoja yako kwa facts.
 
Samia atatufikisha mbali, kwa sera zake rafiki kwa wawekezaji zitakazokuza uchumi wa nchi na kutoa ajira kwa wAtanzania, biashara kati ya Tanzania na nchi jirani pia imerudi, nchi itastawi
 
Siku ya tatu mfumo wa kununua umeme wa TANESCO nchi nzima uko "dawn" wazazi ambao vitoto vyao njiti vipo kwenye incubators jiandaeni kubeba "maiti" vitakufa tu, hospitali nyingi hasa za umma hawana genereta za dharula...
Na izo chanjo zenu za covid sijuhi tumuombe Mh. Uhuru Kenyatta atuhifadhie mana huku hakuna uhakika kabisa wa usalama wake!

Angekua magu leo mtu tanesco angerudi kijijin kwao, hii nchi imekua utopolo kabisa, wanajua jembe kashaondoka sasa hivi wanafanya wanavyotaka na Mama yuko kimya tu na ushungi wake kama kiroba cha bangi
 
Hata wakati wa magu palikua na mgao mkali wa umeme.
 
Mama SSH ndio Raisi wa Jamhuri. Hatukuzoea kuwa na Lady Boss.
Naona yupo vizuri tena zaidi kuliko hao marais waliomtangulia.Mungu ampe afya njema.
 
Huyo BIBI KIZEE hawezi kuwa mfuatiliaji.

Kwanza amejichokea kwa urojo na udhaifu, hata ukimueleza habari za makinikia sijui kama anaelewa ni kitu gani?

Anajua hata maana ya makinikia kweli?

Achana na chuma JPM wewe... a man who understands each word he says!

Huyu BIBI USHUNGI na malipstick yake anatupotezea WAKTI tu!
Jambo la msingi ni utimamu wa akili yake na busara alizo tunukiwa na Muumba wake hizo ndio nyezo kuu na za msingi zitakazo muwezesha kubaini na kung'amua mambo mbalimbali.

ukijumlisha na kivumishi kielezi= kivumishi kihisishi.
 
Mheshimiwa Rais.

Awali ya yote nakutakia Amani ya Mwenyezi Mungu BWANA wa Majeshi na Nakusalimia kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nipende kuchukua fursa hii kukupongeza kwa uchapakazi makini, kwa uongozi thabiti na serikali inayosikia na kuzingatia maoni, matakwa na maslahi ya wananchi. Kwa hakika uongozi wako umekuwa ni faraja kubwa na matumaini makubwa sana kwetu hasa ukizingatia aina ya utawala uliopita, utawala ambao haukujali vilio vya wananchi, utawala uliojaa uonevu, propaganda na matumizi mabaya kabisa ya madaraka.

Mheshimiwa Rais nafahamu kuwa haya unayoyatekeleza ni wajibu wako, lakini sisi Watanzania ni waungwana, kwa hiyo si vibaya kuonyesha uungwana wetu kwa kushukuru. Hata kwenye vitabu vitakatifu tumefundishwa kuwa kushukuru ni jambo zuri na hata Mwenyezi Mungu amesema kuwa Mwenye kumshukuru basi humuongezea. Kwa hiyo mheshimiwa rais tunashukuru kwa aina ya uongozi wako, uongozi uliojaa utu, huruma, uzalendo, haki na vision kubwa ya maendeleo

Tangu umechukua uongozi baada ya kifo cha rais aliyekutangulia Ndugu Magufuli yapata siku 60, lakini katika hizo siku umefanya mambo makubwa, yenye manufaa sana kwa nchi yetu na hapa chini nitaorodhesha machache

1. Ndani ya Siku 60 za uongozi wako, umeshawaondolea wananchi riba (retention fee) ya 6% kwenye mikopo yao ya elimu ya juu.
Mheshimiwa hili ulilolifanya ni jambo zuri mno, hii riba ndiyo iliyokuwa ikiwafanya watu walipe deni miaka na miaka lakini lisiishe maana deni lilikuwa inaendelea kujiaccumulate hata baada ya kulipunguza. Hakika tunakushukuru sana mheshimiwa rais kwa uamuzi huu wa busara

2. Umetangaza Ajira 40000 kwa mwaka huu, na umeshatoa kibali cha ajira takriban 10000 kwanza.

Mheshimiwa rais ubarikiwe sana, hili ni jambo kubwa, vijana wetu walikuwa wanatangatanga mitaani, ajira hakuna, mzigo wa kulea hawa watoto uliendelea kuwa mzigo kwa familia ambazo zimeshatumia kila senti na ndululu kuwasomesha lakini mwishowe wanakosa ajira. Hili suala kwa hakika lilikuwa linayafanya maisha yazidi kuwa magumu lakini umetusaidia sana, na nakuomba uendelee kutoa ajira kadri hali ya uchumi itakavyoboreka

3. Mheshimiwa rais, ndani ya siku 60, umetusaidia kuongeza umri wa mtoto kunufaika na NHIF kutoka miaka 18 hadi 21.
Hili jambo limekuwa msaada mkubwa kwetu wananchi, hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa vijana wa miaka 18 kimsingi wanakuwa bado hawajaanza kusimama vizuri kwa miguu yao, kwa hiyo zigo la matibabu yao lilikuwa linarudi tena kwa mzazi au mlezi, kitendo chako cha kuongeza umri wa kunufaika na Bima ya Afya hadi miaka 21 chini ya cover ya mzazi/mlezi kimeleta unafuu mkubwa kwa hawa vijana na familia zao kiujumla

4. Mheshimiwa ndani ya siku 60 umesaidia kurudisha bei za vifurushi vya internet kuwa angalau kama zamani, na umefungulia mitandao iwe huru.

Nikupongeze sana mheshimiwa rais kwa Intervention yako, Serikali iliyopita ya Magufuli ilituhadaa wananchi kuwa inakwenda kukaa na makampuni ya simu ili yashushe bei za vifurushi, kilichotokea hapo ni uwongo mtupu, bei zilipanda na sisi wananchi tukaumia sana, maana zilikuwa ni bei ambazo majority ya wananchi wasingeweza kuzimudu. Wewe umetusaidia kuzirudisha angalau kwa bei ya awali. Nafahamu kuwa licha ya kuwa yapo makampuni korofi yanajivutavuta, lakini hata yenyewe yameshusha kidogo, na yapo yaliyotii kabisa agizo lako, kwetu sisi wananchi tunasema hili si haba, na tunaomba hayo makampuni korofi yafuatiliwe bila kuathiri uwekezaji wao ili iwepo win-win.

Pia mheshimiwa rais, ndani ya siku zako 60, Umeachia mitandao iwe huru zaidi, Leo hii hatuhitaji rena VPN kuipata twitter, na wale waliokuwa na online TV umewaachia huru. Kwa hakika hii ni hatua muhimu sana ya kulinda demokrasia yetu na uhuru wa habari.

5.Mheshimiwa rais, ndani ya siku zako 60 Umeachia huru wafungwa wa waliobambikiziwa kesi.

Miongoni mwao wamo wale waliowekwa ndani kwa sababu za Kisiasa, mheshimiwa jana peke yake umeachia huru wafungwa takriban 147 ambao makosa yao yalikuwa ni ya kubumba, hawa walibambikiziwa kesi mbayambaya za uhujumu uchumi ili waozee jela kwa sababu za ajabuajabu kabisa ikiwemo ugomvi wa kisiasa tu.

6. Ndani ya siku 60, umeonyesha uongozi makini wenye kuzingatia sayansi kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa korona.

Kiukweli kabisa, Nchi yetu ilifanikiwa kupata mafanikio katika wimbi la kwanza kwa sababu tulipigana katika angle tatu, tulipambana kwa kufuata recommendations kadha wa kadha za kisayansi, pia tukawa tunatumia na njia zetu za asili bila kusahau spiritual front. Lakini kwenye wimbi la pili tukawa wabishi, sayansi tukaikataa, tukapromote njia zetu za asili peke yake na huku upande wa Spiritual tukawa wanafiki zaidi, Tukataka kulitumia Jina la Mungu kuficha kutowajibika kwetu, matokeo yake wimbi la pili likawa disaster sana.

Nakupongeza mheshimiwa raisi kwa kurudisha common sense kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa huu, ba ushauri wangu ni kuwa lazima tuendelee kupambana na huu ugonjwa kisayansi, bila kusahau njia zetu za asili na bila kumsahau Mungu, na tuwe genuine kabisa, tusimtumie Mungu kisiasa ili kuficha kutowajibika kwetu. Nakupongeza kwa kupromote barakoa badala ya kuzibeza.

7. Ndani ya siku 60 umeshawezesha Mahindi yetu kuendelea kupata soko Kenya na Umeweza kuingia mkataba wa kujenga bomba la gesi ili tuwauzie Wakenya.

Mheshimiwa, wote tunajua kuwa Wakenya walikerwa na kauli ya rais Magufuli juu ya kuwakebehi kwa lockdown waliyoweka kwao, na Magufuli akajitapa kuwauzia chakula kwa bei ghali, kwa hiyo Wakenya wakafanya retaliation. Ila kutokana na uwezo wako mkubwa kwenye diplomasia umewezesha kutatua hilo tatizo na sasa mahindi yetu yanapata soko huko Kenya, wakulima wetu wananufaika.
Pia ndani ya siku 60 umetia saini mkataba wa kujenga bomba la gesi ili tuwauzie Wakenya gesi. Kwa hakika hili ni hambo kubwa kiuchumi, litakapokamilika litasaidia kukuza uchumi wetu.

8. Mheshimiwa, ndani ya siku 60 umeonyesha nia kuzungumza na wapinzani na kujenga mazibgira ya siasa za kuaminiana katika spirit ya kupingana bila kupigana.

Mheshimiwa rais, chini ya utawala wa Rais Magufuli, siasa za nchi hii zikitawaliwa na ubabe, uporaji wa haki ya wananchi kuchagua viongozi wao kwa haki(rejea chaguzi za serikali za mitaa), polisi kuvamia ofisi za wapinzani, kuvuruga mikutano yao hata ile ya ndani, kubambikiza kesi wapinzani na hata wengine kupigwa risasi mchana kweupe bila uchunguzi wowote. Mheshimiwa, sisi tunakupongeza kwa kutaka au kukubali mazungumzo na wapinzani, maana at the end of the day, hii nchi ni yetu sote na ni lazima kila chama kiwe na haki ya kuoperate nchini bila kufanyiana fujo na vurugu.

9. Ndani ya siku 60, umetuonyesha kuwa uko tayari kung'oa Washenzi na waonevu katika nyadhifa za utumishi.
Kitendo cha kumchunguza yule bwana wa bandari na yule kijana mkuu wa wilaya, ni message kali kwa viongozi wengine kuwa hauko tayari kuvumilia ushenzi. Nimependezwa na approach yako ya kuwachunguza na hatimaye kuchukua hatua, maana haitoshi tu kumtumbua mtu, bali atumbuliwe huku ukiwepo ushahidi wa kutosha kumfikisha katika mkono wa sheria, lakini pia inalinda haki yake kama labda anasingiziwa.

10. Mheshimiwa rais, ndani ya siku 60, umeagiza wale walikuwa na elimu ya darasa la saba waliofukuzwa kazi bila kulipwa stahiki zao walipwe

Mheshimiwa hili ni jambo zuri, ni jambo la haki, maana wale ni wanadamu, wana haki zao za msingi, kitendo cha wewe kuzitambua, ni jambo la faraja sana.

OMBI MAALUM KWAKO MHESHIMIWA RAIS
1. Mheshimiwa Rais, Mwenyezi Mungu amekuweka katika hiyo nafasi, basi tunaomba sisi wananchi utujengee MIFUMO mizuri ili kesho na keshokutwa upo au haupo tuweze kusema kuwa umetuacha tukiwa na HAKI zaidi katika nchi, tukiwa HURU zaidi katika nchi, Tukiweza KUWAWAJIBISHA Viongozi wetu zaidi katika nchi, TUKINUFAIKA na rasilimali zetu zaidi katika nchi.

Na hilo halitiwezekana chini ya katiba hii ya sasa, Hii ni katiba ya KIDIKTETA yaani hata wewe hapo mheshimiwa rais ukiamua kuwa Dikteta katiba hii inakupa ushirikiano mkubwa. Sasa tunaomba utupe MUAFAKA mzuri zaidi wa Kitaifa, na Muafaka huo ni Katiba mpya iliyo nzuri na bora. Mhwshimiwa hili ndo litatufanya tukukumbuke zaidi kuliko hata kama utaweka mabomba ya asali katika kila nyumba!.

2. Pili naomba wale waliovunjiwa nyumba zao Kimara-Mbezi, serikali yako iwaangalie, maana Serikali iliyopita ilionyesha ubaguzi kwenye kutekeleza zoezi la ubomoaji, wale wa Mwanza ilisema wasibomolewe eti kwa sababu walimpa kura Magufuli kwenye uchaguzi wa mwaka 2015, ila wale wa Kimara-Mbezi serikali ikawabomolea bila kujali kuwa walikuwa na Stop order ya Mahakama kuzuia ubomoaji huo. Mheshimiwa Rais naomba uwape kifuta machozi wananchi wa Kimara Mbezi maana kuna ukatili mkubwa na double standard kubwa sana ilifanyika pale.

3. Tunaomba zile sheria za kidhalimu, zenye lengo la kuupalilia udikteta nchini zifanyiwe marekebisho au ziondolewe kabisa. Mheshimiwa rais tunaomba uondoe sheria inayowapa kinga Spika, Naibu wake na Waziri mkuu Kinga ya kutoshitakiwa, hawa wanataka wasishitakiwe kwa nini?, pia sheria za mitandao, vyombo vya habari na kanuni zake zibadirishwe. Hizo sheria siyo conducive kujenga Taifa la watu wenye FIKRA huru kutoa maoni yao kikamilifu, na hazilindi wala kupanua Demkrasia yetu.

4. Pia Mheshimiwa Rais, nchini katika majela yetu kumejaa Masheikh wengi ambao wamo ndani kwa kesi za kubambikiza ikiwemo Masheikh wa UAMSHO na wengine wengi nchini, hawa bado hawajaachiwa, nakuomba Masheikh hawa wasio na hatia nao waachiwe kama wafungwa wengine waliobambikiziwa makosa mbalimbali ikiwemo ya kisiasa wanavyoachiwa.

Mwisho kabisa nimalize kwa kusema. Mheshimwa, Upo kwenye right track sana, yaani uongozi wako ni mzuri na makini mno endelea kuchapa kazi

Kazi iendelee!
Nipo kwenye gari natoka mjini hapa Jijini Mwanza. Kuna daladala nimeiona inapiga ruti ya Airport - Nyashishi nyuma imeandikwa "USIFURAHIE MWANZO, FURAHIA MWISHO"!
 
Mbona unahangaika sana kumtetea huyo BIBI KIZEE dhaifu?

Mara sijui ng'ara sijui nini!

Hawezi kung'ara kwa kuvaa ushungi na kupaka lipstic!

Lazima afanye vitu tangible vya maendeleo vinavyoonekana na kushikika!

Afya, elimu, miundo mbinu nk.... kushughulikia mafisadi na wauza ngada.

Sasa hivi huyo BIBI KIZEE yuko bize anawatetea mafisadi! Ati walionewa!

Si ajabu na yeye anauza ngada, maana sio kwa spidi hiyo aliyoingia nayo ya kuwatetea WAHALIFU na MAJIZI.

Unakuja na habari hafifu za "ng'ara mama ng'ara mama"....... for what exactly? Bando?

Man, are you stooopid or something?
Babu kizee ,tulia ,watu wale furaha,ya uhuru amani na upendo.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Vizuri sana kweli tunamshukuru Mungu Mkuu kwa muujiza aliotutendea tulikuwa kama watumwa kwenye nchi yetu wenyewe sasa mambo yanakwenda shwari kabisa.
 
hamna lolote ashapoteza mvuto hata siku mia 100 hazijaisha....watu wanataka kuona vitendo na sio maneno,uzanzibari umetamalaki wengine twaona kero tu tunatamani 2025 ifike haraka maisha yaendelee.

Tumechoka na tuko wengi.
Mko wengi mataga na sukuma gang ila watanzania wazalendo tunaona mama yuko vizuri.
 
hamna lolote ashapoteza mvuto hata siku mia 100 hazijaisha....watu wanataka kuona vitendo na sio maneno,uzanzibari umetamalaki wengine twaona kero tu tunatamani 2025 ifike haraka maisha yaendelee.

Tumechoka na tuko wengi.
Nenda kapumzike hapa hadi 2025 ifike
tapatalk_1621283175890.jpg
 
Back
Top Bottom