Sikizeni enyi masheikh na maaskofu!

Kadogoo

JF-Expert Member
Feb 26, 2007
2,073
341
Makala hii kuhusu Masheikh na Maaskofu imeandikwa na Mzee Mwanakijiji inatia moyo kuonyesha angalau mwana JF mmoja amejitokeza waziwazi kwa kuwakosoa Viongozi wetu wa dini 2 kubwa hapa nchini! soma makala yenyewe:

Nisikilizeni enyi masheikh na maaskofu!

Mimi nakubaliana na yote uliyotaja Mzee ila ushauri wangu kwa viongozi wa dini kama wataungana kwa lengo la kupinga dhulma basi muungano huo usiwe wa kibubusa bali uwe na masharti na kama masharti hayo yatavunjwa basi muungano huo uvunjike na kila mtu achukue jembe akalime!

Baadhi ya masharti hayo ya kuungana viongozi wa dini nashauri yafuatayo:

1) Kanisa liombe radhi kwa Watanzania kwa kufurahia madhambi yote yaliyofanywa na Serikali tangu ya awamu ya kwanza, ya pili, na ya 3! baadhi ya madhambi hayo ni Utawala wa Julius kuwakamata na kuwatia jela viongozi wa dini ya Kiislamu bila ya kuwafikisha mahakamani!

Mfano ni Mufti mkuu wa kwanza Tanzania Sheikh Mohamed Bin Ameir, Rais wa Jumuiya ya EAMWA Tanzania Sheikh Tewa Saidi tewa, Katibu Mkuu wa EAMWA Bibi Titi Mohamed na Julius kuivunja jumuiya hiyo tukufu iliyowaletea maendeleo makubwa Waislamu wa Tanzania na kuwaletea BAKWATA iliyoasisiwa kwa kutumia katiba inayofanana na katiba ya TANU! ndio maana mpaka leo tuna Shehe wa Mkoa, wilaya, kata na kijiji kama ilivyo kwa CCM mwenyekiti wa CCM mkoa, wilaya nk.

2) Kanisa liombe radhi kwa kushirikiana na Serikali ya Nyerere kumpachika Padre ktk Wizara ya Elimu ili asimamie uchakachuaji wa mitihani ya Secondary, high school na hata Chuo kikuu cha Dar, ili kuwachuja wanafunzi walio waislamu na kuwapendelea wakristo!

Mfano mimi mwenyewe nikiwa darasa la 7 jumla ya wanafunzi tulikuwa 30, waislamu walikuwa 17, wakristo 8, na Hindus 5 na kila mtihani kuanzia darasa la 4-7 mitihani yote walikuwa waislamu wakiongoza kuanzia namba 1,2,3,4,5,mpaka 7 lakini cha kusikitisha matokeo ya kuingia Secondary walifaulu wakristo 7, waislamu 2 na baniani 1 kwanini? ina maana hawa waislamu hawakudurusu?

Ukifuatilia ya Secondary mpaka chuo kikuu utakuta mapungufu kama hayo!

3) Kanisa liombe radhi kwa kunyamaza wakati Serikali ya Mwinyi ilipowauwa Waislamu wa zanzibar walipoandamana mwaka 1988 wakipinga kauli ya Mama Sofia kauwawa ya kutaka Qurani ifanyiwe mabadiliko!

4) Kanisa liombe radhi kwa kuishinikiza serikali ya Mkapa kuwakamata Waislamu na kisha kuwauwa ndani ya msikiti wa Mwembechai na kusababisha wengine kuwa walemavu wa maisha mfano ni Mtoto Chiku alimiminiwa risasi kama maji! Rejea kauli ya Paroko Camilius Lwambano An-nuur Na. 201

4) Kanisa liombe radhi kwa kubariki mauaji ya Wafuasi wa CUF huko Unguja na Pemba mwaka 2001!

5) Kanisa lisijiingize ktk madai ya Waislamu kwa Serikali kuhusu Mahakama ya Kadhi na OIC!

6) Makanisa hasa ya Kilokole yawache tabia ya kutembelea nyumba wanazoishi waislamu na kugawa Biblia bure kwani Waislamu wakijibu mapigo sidhani kama Kanisa litafurahi!

7) Makanisa ya Kisabato na Kilokole waache tabia ya kuja na magari ya tarumbeta na kuimba kwa sauti kubwa karibu na Misikiti wakati Waislamu wako ktk sala hivyo kusababisha usumbufu na kukosa utulivu ndani ya ibada zao! huo ni uchokozi!!

8) Mwisho na muhimu- Kanisa liwe na tabia ya uvumilivu pale Waislamu wanapohubiri kuwa Yesu si Mungu kwani wao nao huvumilia wakisikia Wakristo wakimuita Yesu kuwa ni Mungu!

Kama Kanisa liko tayari kufuata masharti haya basi Waislamu wako tayari kushirikiana na Kanisa kukemea maovu ktk msimamo wa pamoja kinyume chake kila mbwa afoke kivyake!

Nakushukuru Mzee Mwanakijiji kwa makala yako safi lakini...............
 
8) Mwisho na muhimu- Kanisa liwe na tabia ya uvumilivu pale Waislamu wanapohubiri kuwa Yesu si Mungu kwani wao nao huvumilia wakisikia Wakristo wakimuita Yesu kuwa ni Mungu! kwani Yesu kwa Waislamu ni mtume Issa ambae mama ake ni mariamu huku kikristo akiitwa Maria bikira!

9) Kanisa liache tabia ya uchonganishi kwa kuwagonganisha Waislamu na Serikali!

Kama Kanisa liko tayari kufuata masharti haya basi Waislamu wako tayari kushirikiana na Kanisa kukemea maovu ktk msimamo wa pamoja kinyume chake kila mbwa afoke kivyake!

Nakushukuru Mzee Mwanakijiji kwa makala yako safi lakini...............
 
M.M. Mwanakijiji​
KAMA kuna wakati nimetamani kunyofoa nywele zangu kwa hasira na kushangazwa ni wakati kama huu. Hakuna watu ambao wamenishangaza juu ya misimamo yao kuhusu maslahi ya taifa kama hawa ndugu zetu masheikh na maaskofu.

Kuna kitu hakiko sawa katika kundi hili na kuna wakati mtu ajitokeze na kuwaambia ukweli. Nadhani wanatumia majoho na kanzu zao za ibada kuanza kulichanganya taifa na kutugawanya wananchi kwa misingi ya kidini huku wao wenyewe wakijiaminisha kuwa wanafanya “mapenzi ya Mungu”. Nisikizeni enzi maaskofu na masheikh!

Sasa hivi kuna mgongano wa wazi kati ya viongozi hawa wa dini huku kundi moja likionekana kuwa kali dhidi ya serikali na kundi jingine likionekana kutafuta udhuru na kuitetea serikali.

Yote mawili yanajaribu kuaminisha watu kuwa yanafanya hivyo kwa masilahi ya taifa au masilahi ya watu wa kundi lao. Lakini kinachonishangaza zaidi ni kuwa mgongano huu wa viongozi wa dini haumsaidii Mtanzania wa kawaida bali unawaimarisha watawala madarakani; kwani wanajua kuwa nguvu ya kuwakemea haiko katika umoja.

Niliandika makala mwaka 2009 mwezi Oktoba nikielezea kile nilichokiita kuwa ni “uenzetu huu” yaani kama nilivyofafanua kuwa ni hisia ya kuona mtu mnayefanana kwa namna fulani anaonewa, kunyanyaswa au kulengwa na wengine kwa sababu ya vitu mnavyofanana na si sababu halisi. Nilielezea kwa kirefu katika makala ile kuwa mojawapo ya mambo ya hatari yanayotokea katika Tanzania ni kuwa tunauangalia ufisadi, uongozi na vitendo vya kukiuka maadili ya uongozi kwa rangi ya “uenzetu”.

Nakumbuka nilihoji (kama masheikh walivyohoji hivi majuzi) kuwa kuna mambo ambayo ni ya kifisadi yalifanyika chini ya utawala wa Rais Mkapa (Mkatoliki) ambayo yamelisababishia taifa hasara kubwa na aibu ya kutosha tu.

Nikauliza kuwa: “Hakuna kiongozi yeyote wa Kikatoliki aliyekuwa na ujasiri wa kupiga kelele na kutaka Mkapa arudishe mali hizo za Watanzania alizojipatia kinyemela kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi ya mwaka 1998 (ambayo yeye mwenyewe aliisaini).

Na hata leo hii ambapo serikali imekiri kuwa Mkapa alijipatia vitu hivyo kinyemela na kuamua kuvirudisha serikalini na kuwabambikizia Watanzania gharama ya kulipa madeni ya Kiwira hakuna kiongozi yeyote wa Kanisa aliyemtaka Mkapa kuwaomba radhi Watanzania na kutengeneza alichoharibu (reparation)?”

Nisikilizeni enyi masheikh na maaskofu!

Na nikasema kuwa: “Lakini leo hii (maaskofu) wamepata ujasiri mkubwa wa kusema ukweli mbele ya wenye madaraka (speaking truth to power) hasa pale wanayemsemea ni Mwislamu! Hapa, mtu mwingine anaona kuwa kama wangekuwa na ujasiri huo wa kukemea uovu mbele ya Mkapa labda mengine yasingefika huku.” Kauli yangu hiyo imerudiwa hivi juzi na uongozi wa Kiislamu kwenye tamko lao la Karimjee. Ukweli ni kuwa uongozi wa Uislamu una hoja katika hilo.

Ni kweli wanahoja kwa sababu wakati leo hii kina Kardinali Pengo wanashangazwa na wananchi kuuawa mikononi mwa vyombo vya dola wengine tunauliza mbona walikufa watu Mwembechai na Pemba mikononi mwa polisi na hakuna maaskofu waliokuja juu?

Je, yawezekana ni kweli kuwa hawakuweza kufanya hivyo kwa sababu serikali ilikuwa inaongozwa na “Rais Mkristu” mwenzao? Hii hoja inaweza kuwa na nguvu zaidi kwa sababu miaka zaidi ya mitano tangu Mkapa atoke madarakani uongozi wa Wakristu nchini bado hawajathubutu kunyoshea mkono utawala wake kuwa ulichochea ufisadi huku sote tunajua kuwa wizi wa EPA, Meremeta na uvurugaji wa Katiba ulifanyika chini ya utawala wa Mkapa?

Sasa leo maaskofu wanaposimama na kuinyoshea vidole serikali ya Kikwete (Mwislamu) kwanini baadhi ya Waislamu wasione kuwa linatokea kwa sababu za tofauti ya kidini? Nisikizeni enyi maaskofu!

Ili maaskofu wapate mahali pa kusimamia wanapoikosoa serikali ya Kikwete ni lazima kwanza waombe msamaha kwa ukimya wao wakati Watanzania wameuawa Pemba na Mwembechai; si kwa sababu Waislamu waliuawa bali kwa sababu wananchi wameuawa.

Msimamo huo ungetakiwa uwe hivyo hata kama waliouawa wangekuwa ni Wapagani! Kwa kadiri maaskofu hawatoi tamko la kuchukua msimamo wa ufisadi na kutaja kwa majina utawala wa Mkapa, hawana ujasiri wa kumkemea Kikwete; si kwamba hawana hoja au hawana sababu lakini bila ya kusahihisha kosa lao la awali, Waislamu ni lazima na wana haki ya kushuku sababu ya maaskofu kufanya hivyo.

Lakini katika makala ile ile niliandika kitu kingine ambacho nacho kinatokea tena sasa hivi. Nisikilizeni enyi masheikh!

Niliandika hivi: “Upande wa pili tunauona leo hii mahusiano kati ya baadhi ya makundi ya Waislamu na utawala wa Rais Kikwete ambaye naye ni Mwislamu. Licha ya madudu ambayo yanafanywa mbele yetu na mengine yenye kuwaathiri Waislamu bado hakujatokea kiongozi au uongozi wa Waislamu ambao wamethubutu kumuambia Kikwete na serikali yake maneno yenye ukweli.”

Jambo hili nililiandika 2009 na sasa mwaka 2011 bado linasimama kama ushahidi wa usahihi wake. Hakuna kiongozi wa Kiislamu au chombo cha Waislamu ambao wamethubutu kunyoshea kidole serikali ya Kikwete kwenye masuala ya kitaifa.

Nilifafanua hili kwa sababu naam, wamekuwepo viongozi wa Kiislamu ambao wameilalamikia serikali kwenye masuala “yenye kuwahusu Waislamu” na tumeliona hili tena siku ya Jumamosi ambapo hoja zao za utetezi zinahusu kile wanachokiita kuwa ni “masilahi ya Waislamu”. Kama mtu amefuatilia mjadala wao na tamko walilolitoa ni wazi kuwa wamekerwa zaidi na maaskofu waliozungumzia suala la mauaji ya wananchi Arusha si kwa sababu maaskofu wamesema kitu kibaya bali zaidi kwa sababu maaskofu hawakuonyesha kujali hivyo wakati “Waislamu” walivyouawa huko nyuma. Kwao suala hili ni suala la kidini zaidi.

Niliandika hivi kwa kuhoji katika makala ile kama unabii wa kule tulikokuwa tunaelekea na hatimaye sasa tumefika: “Hapa sizungumzii katika masuala yenye kuwagusa Waislamu tu (kama Kadhi, OIC, Hija n.k) bali nazungumzia yale ambayo yanawagusa wao pia kama Watanzania na wananchi. Masuala ya nishati, madini, nafasi za ajira n.k
Leo tunashuhudia mabilioni ya fedha zetu yanatumika kama hayana mwenyewe wakati watoto wetu bado wanahangaika na majengo mabovu ya shule, huduma na miundombinu mibovu katika maeneo mbalimbali licha ya mafanikio ya hapa na pale.

“Masuala ya Richmond, Dowans, Loliondo n.k ambayo yanawahusisha baadhi ya watu wenye kufungamana na nchi za Kiislamu hakujavutia hasira ya Waislamu wa Tanzania. Kwanini? Kwa sababu ni “wenzao”? Kwamba kwa vile watu hawa wanajulikana kuwa ni Waislamu au wanatoka nchi za Kiislamu basi wasipingwe sana kwani wote hawa ni sehemu ya “umma” wa Waislamu?”

Matokeo yake ni kuwa uongozi wa Waislamu Jumamosi hawajatoa tamko lolote kuhusu malipo ya Dowans kwa sabababu wanazozijua wao. Shura ya Maimamu hawajasimama kuhoji uhalali wa wananchi kuuawa huko Mbarali na Arusha kwa sababu “mbona huko nyuma wananchi wengine walikufa mikononi mwa serikali?”

Marafiki zangu kama kina Prof. Njozi (aliyeandika kitabu cha Mwembechai) mbona hajatoa tamko lolote la kuonyesha kukerwa na mauaji haya? Yawezekana uongozi wa Waislamu hawataki kuonekana na wenyewe wamesimama dhidi ya Rais “Mwislamu” mwenzao?

Nisikizeni enyi maaskofu na masheikh!

Tanzania ni Tanzania na ni kubwa kuliko makundi yenu ya kidini. Watanzania ni Watanzania zaidi ya Wachagga, Wandengereko, Wamatumbi na Wanyiha! Utanzania wetu uko juu zaidi kuliko dini zetu.

Wale ambao wanataka kutugawa kwa sababu ya dini zetu wanafanya makosa ambayo gharama yake ni kuua Utanzania wetu.

Tunataka viongozi wa kidini ambao wanaposimama kutetea haki basi watetee haki bila kujali anayedhulumiwa ni nani! Hatutaki viongozi wa kidini ambao wanauliza kwanza “ni dini gani” badala ya kusimama na kupinga dhulma.

Jumatatu hii iliyopita huko Marekani wameadhimisha siku ya mwanaharakati za haki za kiraia na za kibinadamu Mchng. Martin Luther King Jr. Mchg. MLKJr. alitambua kuwa kutetea haki za watu weusi nchini mle haikuwa kwa sababu ya “Ukristo” wake kwani wengi walikuwa si Wakristu.

Hata Malcom X baadaye alikuja kuelewa kuwa ni haki za watu weusi wote zilizokuwa zinadhulumiwa. Uovu hauna dini na unatakiwa kupingwa na wenye dini na wasio na dini.

Nisikilizeni enyi masheikh na maaskofu; pataneni dhidi ya uovu ili muweze kuukabili. Msipopatana tutawaacha kwenye mataa na kama nilivyowahi kusema huko nyuma mtakuwa hamna mpango (you will become irrelevant)! Kwani wananchi watawashtukia kuwa na nyie mnaongozwa na majoho na kanzu zenu na hivyo Watanzania wasiwategemee kuwa ni watetezi wao.

Kwani hata hao maaskofu ambao leo hii wanaonyesha kuwa wanakerwa mbona hakuna hata aliyesimama kuandamana kupinga vitendo hivi vya kifisadi na dhuluma? Ni lini tutawaona “walioshtushwa” kina Pengo na Laizer wakisimama na kuongoza maandamano ya kuipinga serikali au uongozi wa dhulma? Je, Masheikh hawataweza kusimama dhidi ya ufisadi hata kama aneyehusishwa ni mtu wa “msikiti” wao? Au yanakuwa ni maslahi hadi pale yanpogusa maslahi ya Waislamu tu?

Ndugu zangu, kila zama zina mashujaa wake na kila shujaa ana ujumbe wake. Hizi ni zama zetu na ni katika zama hizi tutangeneza mashujaa wetu sisi wenyewe au historia itawanyanyua kati yetu. Haijalishi kama mashujaa hao watakuwa ni Wakristu, Waislamu, wasioamini, wenye kuamini kijadi au vinginevyo.

Hawa maaskofu na masheikh ambao wanafikiri wanaukiritimba wa mbinguni nina ujumbe mmoja kwao; sikilizeni enyi maaskofu na masheikh kwani nanyi zama zenu zinapita na Watanzania watasimama hata kama ni peke yao; kama watawala wetu walioshindwa nanyi msipoangalia mtaingia katika shimo la kusahauliwa kwa kushindwa kuukemea uovu na kumaanisha hivyo.

Ujumbe wangu uko wazi. Pataneni dhidi ya dhuluma na uovu kwani ni katika hilo tu mtahukumiwa. Kwani kama alivyosema Luther “dhuluma mahali popote, ni dhuluma mahali pote”.

Nisikilizeni enyi masheikh na maaskofu!

Source: Tanzania Daima
Tar. 19 January 2011,
By M.M. Mwanakijiji
 
Mi pia jana usiku nilifanikiwa kusikiliza mjadala wa washeikh kupitia Redio Iman. Kwa kweli mjadala ulijaa uchochezi wa hali ya juu na kama leo wataendelea basi nita-record afu niulete hapa jamvini muone wenywe. So nimeona hii article ya Mwanakijiji niiweke hapa ili wale masheikh wa jana na maaskofu wa kesho wajifunze kitu kupitia maoni ya great thinkers yatakayotolewa hapa. So if there is anyone with a burning point to share with us please you are most welcome!
 
Hawa wameshakubaliana kutokubaliana kwa kigezo cha nani yuko IKULU. Mwanakijiji hapa anapigia mbuzi gitaa. Wanatofautiana sana hasa KIELIMU.
 
Hawa wameshakubaliana kutokubaliana kwa kigezo cha nani yuko IKULU. Mwanakijiji hapa anapigia mbuzi gitaa. Wanatofautiana sana hasa KIELIMU.
Kwenye waraka wa waislamu uliokua unasoma redioni hawakutaja kabisa mambo kama dowans, gharama za umeme, maisha kupanda, mauaji ya arusha n.k. bali walionekana kuwanyooshea maaskofu vidole kwa kukemea serikali inayoongozwa na mwislamu mwenzo. Hata madai ya katiba wanasema waislamu waungane wachangamke kudai kuingizwe vipengele vya mahakama ya kadhi, IOC, n.k. Kweli kazi ipo........
 
DUUUUUU,

M.M.Mwanakijiji Kwa kweli nakuunga mkono 100 Kwa 100 Yote uliosema ni kweli hapa kuna mgongano wa mawazo baina ya Masheikh na Maaskofu.

Ili tuwaelewe na twende pamoja nao ni kweli wakae chini waelezane wapi kila mmoja alikosea na nini watanzania tunategemea kutoka kwao waelewe kuwa Dini ni imani lakini Amani bila Imani hakuna na ili tuwe na Imani thabiti ni vema wao wote wawe nalengo moja, sijafika Ulaya ila nasikia baadhi ya Majengo yaliyotumika kama nyumba zaibada yamegeuka kuwa Majumba ya starehe.

Hata hapa kwetu hilo siku moja litatokea pindi tu tukijua hawa jamaa wapo kwa maslahi yao na si Watanzania.

Tuungane kudai Maslahi ya Watanzania na si waislam wala wakristu.
 
Kwenye hili la maslahi ya kitaifa masheikh watoeni,kwenye maslahi ya waislamu pekee na dini yao..........count them in! Wao wanaamini shida walizonazo zinatokana na wao kuwa waislamu na kutokupewa haki sawa kwa kuwa wao ni waislamu na si kama watanzania as if shida zimegawanyika kutokana na dini au effect za ufisadi zinaenda kwa watu wa dini fulani tu.
Maaskofu tuko nao kwenye maslahi ya kitaifa na ya kujenga roho,sasa sioni wapi watakutana???wawe na sauti moja. kila mmoja ana priority na kufikia malengo yao kuna wanaotumia akili na busara na wapo wanaotumia hisia.:A S 39:
 
DUUUUUU M.M.Mwanakijiji Kwa kweli nakuunga mkono 100 Kwa 100 Yote uliosema ni kweli hapa kuna mgongano wa mawazo baina ya Masheik na Maaskofu ili tuwaelewe na twende pamoja nao ni kweli wakae chini waelezane wapi kila mmoja alikosea na nini watanzania tunategemea kutoka kwao waelewe kuwa Dini ni imani lakini Amani bila Imani hakuna na ili tuwe na Imani thabiti ni vema wao wote wawe nalengo moja, sijafika Ulaya ila nasikia baadhi ya Majengo yaliyotumika kama nyumba zaibada yamegeuka kuwa Majumba ya starehe.hata hapa kwetu hilo siku moja litatokea pindi tu tukijua hawa jamaa wapo kwa maslahi yao na si Watanzania.Tuungane kudai Maslahi ya Watanzania na si waislam wala wakristu.

Unajua mkuu, waaskofu sasahivi wamebadilika na sii kama zamani ile ilivyokuwa bora liende. Sasa hivi wanaikosoa serikali waziwazi na bila woga pale viongozi wao wanapotenda ndivyo sivyo. Sasa bahati mbaya ni kipindi cha waislamu kuongoza nchi ndo maana masheikh wanawatetea.
 
Huu ni uchambuzi makini na muhimu saaana, NGOJA NIUWEKE KUMBUKUMBU KABISAAA.
 
Unajua mkuu, waaskofu sasahivi wamebadilika na sii kama zamani ile ilivyokuwa bora liende. Sasa hivi wanaikosoa serikali waziwazi na bila woga pale viongozi wao wanapotenda ndivyo sivyo. Sasa bahati mbaya ni kipindi cha waislamu kuongoza nchi ndo maana masheikh wanawatetea.
Ni kipindi cha Waislamu kuongoza NCHI? Sisi tumemchagua JK sio kwa UISLAMU wake! Ingawa naye ana mchango wake kwenye huu udini unaotajwatajwa sasa. Alipokosa asilimia 80 ya kura akadhani ni udini umesababisha. Akasahau mwaka 2005 aligombea na WAKRISTO pia kama Dr Slaa.
 
Msheikh wameshtuka baada ya kugundua kuwa anapokuwepo muislam ikulu ndo maaskofu hutoa matamko na mawaraka mengi lakaini akiwepo mkristu mwenzao hutasikia kabisa utadhani wamefungwa mdomo au kama vile mambo yamenyooka.Vuta kumbukumbuku utawala wa Nyerere amabapo watu wengi walikufa wakati wa vijiji vya ujamaa,hali mbaya ya uchumi amabapo nchi ilifilisika kabisa hata sabuni ya magwanji au nguo ya mtumba vilikuwa shida kupatikana.Maskofu walisema kitu? Njoo utawala wa Mwinyi nenda kwenye maktaba za makanisa utakuta mawaraka na matamko kibao.Njoo kwa Mkapa ambapo mengi mabaya yalitokea hata watu walikufa kwa njaa lakini maaskofu kimyaaa.Sasa Kikwete ona maaskofu wanavyotoa matamko na mawaraka kibao utadhani nchi inakaribia kuanagamia sasa wanataka kuikoa.Wakao kuwepo wasuburi akija Rais mkiristu utaona kama watafungua mdomo kuikemea serikali.Haya yote ni unafiki wa maaskofu na chuki dhidi ya waislamu.
Kuna baadhi ya wakristu wantoa kashfa kwa masheikh eti hawana elimu.Hivi kwao elimu ni kujua kusoma kingereza tu? Unawezaje kusema mtu mwenye degree ya Uislam kutoka chuo kikuu kwa mfano cha Al-azhar Misri kuwa hana elimu? Unawezaje kusema kuwa mtu anaeweza kusoma Quran na kuitafsiri kwa kiswahi eti hana elimu?
 
mi nadhani umefika wakati tukubaliane kuwa kunatatizo hapo,kwani kipindi waislamu wanapewa nafasi chache za kimasomo hakuna askofu aliye kuja na kusema ama kukemea juu ya kwa nini inakuwa hivi,mpaka kigoma malima alipo tusaidia kwa kutumia namba na si majina atleast nasi sasa tunaonekana,
kiukweli hapa tunatatizo la mshikamano na umoja kati ya hawa watu wawili Shehe na Askofu

Kwani kipindi cha mkapa mengi yamefanyika lakini waislaam hawakuwa mstari wa mbele kukemea ila waliomba kile ambacho kinawahusu na hata hivyo hawakupewa,lakini ebu angalia sasa yawezekana kikwete ana andamwa sana may be kutokana na DINI yake ingawaje ni kweli ktk uongozi wake kuna matatizo mengi lakini tutambue kuwa si yote ni yake mengine kayaridhi kutoka kwa Mkapa

Hivyo ndugu zangu tuondoe Ukristo na Uislaam tushirikiane kwa kila jambo ili hii nchi iende
la sivyo tutakuwa tukinyoosheana vidole huku mafisadi wakila nchi yetu

MSEMA KWELII HAPENDWI DAIMAAA
MAPINDUZIIII DAIMAAAAA:frusty:
 
Lakini.. bado hujasema upande wa pili, Mashehe nao wafanye nini?

anadhani hawana wajibu katika kuleta amani nchini: angeongeza hii: makanisa yooooooooooooooote, na misikiti yooooooooooooooote iwe sound proof na nyumba yoyote ya ibada isiwe na supika za nje. Mihadhara yoooooooooooooooooooooote na mikutano yooooooooooooooote ya kiroho isiitaje dini nyingine.
 
Kalamazoo,
Ni Maaskofu haohao ambao mwaka 2005 walisema JK ni chaguo la Mungu. Kwa nini sasa wamemgeuka hivi? Kwa upande wa elimu wala hauwezi kubisha kwamba Maaskofu wengi (ukiacha akina KAkobe, Mwingira, wa Upako) wamesoma vizuri mno kuliko Masheikh. Masheikh waliosoma vizuri wanajua JK hayuko Ikulu kwa kuwa ni Mwislamu.
 
Mchango Huu nimeudaka kwenye forum ya wanabidii, nadhani unatoa picha ya masuala mengi kuhusiana na mada hii:

Kwa mujibu wa baadhi ya Magazeti, halikuwa Tamko la BAKWATA, ingawa katika Kongamano kulikuwa na baadhi ya Viongozi wa BAKWATA waliotajwa ambao yasemekana walililiunga mkono na kusema kwamba Tamko hili "ni la maana sana na likifanikiwa litaleta faraja kwa Waislamu na wananchi wote" (taz. Tanzania Daima ya jana).

Kimsingi Tamko hilo lilikuwa na mambo mengi ambayo mengi mengine tumeyazoea kuyasikia kutoka kwa Shehe Issa Ponda na Bassaleh. Nisingependa kuyarudia yote yaiyosemwa na viongozi hao lakini ningeomba kuongelea yale yaliyowatofautisha na maaskofu mintarafu vurugu za Arusha. Kwa ufupi wao walitofautiana na Maaskofu kwa kusema kwamba "yaliyotokea Arusha ni mgogoro wa kisiasa kwa hio si busara kwa Maaskofu kusimama mbele ya Chadema" na kuongeza kwamba: "kwa nini Maaskofu walikaa kimya wakati wa mauaji ya Zanzibar na sasa wanapiga kelele juu ya mauaji ya Arusha".

Kwanza sina uhakika kwamba ni kwa kiwango gani tunaweza kusema vurugu za Aurusha ni mgogoro wa kisiasa tu na hivyo Maaskofu hawapaswi kuingilia... Lakini zaidi ya hayo ni kwamba, Tamko hilo lilikuwa na mapungufu ya ukweli wa kihistoria, ama lilitaka kupotosha kwa makusudi umma kwa kusema kwamba Maaskofu walikaa kimya wakati wa mauaji ya Zanzibar.

Ukweli ni kwamba, baada ya mauaji ya raia 23 wasio na hatia yaliyotokea Zanzibar tarehe 26 na 27 Januari mwaka 2001, Maaskofu wakatoliki walitoa Tamko lao tarehe 23 Februari 2001 la kuelezea masikitiko yao juu ya ukatili uliofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia hao, na kuitaka Serikali ya Rais Mkapa wakati ule kufanya uchunguzi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wote waliohusika.

Baada ya hapo, Maaskofu wa Kanisa katoliki hawakuishia hapo, wakawa mstari wa mbele ili kuhakikisha kwamba matukio ya kusikitisha kama hayo, hayajirudii tena katika nchi hii. Wakashawishi kuundwa kwa jukwaa la Viongozi wa dini mbali mbali kwa ajili ya kushughulikia amani na mazungumzano linalohirikisha wajumbe kutoka BAKWATA, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Jumuiya ya Kikristo Tanzania na Ofisi ya Mufti Zanzaibar. Tangu wakati huo mpaka sasa, Maaskofu Katoliki wamekuwa wakibeba gharama zote za uendeshaji wa Jukwaa hilo ikiwemo mikutano n.k.

Wakati wa uchaguzi uliopita, Jukwaa hilo liliwatembelea viongozi wa vyama mbali mbali na kuwasihi wawaelekeze wafuasi wao kuwa na uvumilivu wa kisiasa wakati w kampeni, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi; na lilifaulu kuwatembelea, Maalim Seif Shariff Hamad, Dr. Slaa, Prof. Lipumba na Mhe. Kikwete. Baada ya kuyasema hayo, naomba niseme kwamba, mshangao wangu ulikuwa mkubwa zaidi niliposoma katika gazeti hilo kwamba kiongozi huyo wa BAKWATA ambaye ni mjumbe wa Jukwaa hilo aliunga mkono Tamko hilo wakati yeye mwenyewe anajua mchango wa viongozi wenzake (Maaskofu) katika ujenzi wa amani na mazungumzano miongoni mwa wanajamii hapa Tanzania.

Amekuwa akishiriki vikao vingi tu na kuonyesha angalau apparently, nia yake ya kutaka kupigania amani na maelewano miongoni mwa Watanzania. Sina uhakika kama aliyasema maneno hayo ambayo magazeti yalimnukuu ama kama alikuwa anaunga mkono yote yaliyokuwemo katika Tamko hilo. Kama kweli aliyatamka hayo, na anaunga mkono yote yaliyo katika Tamko hilo, naanza kupata mashaka mengi juu ya baadhi ya viongozi wa dini kama wana nia ya kutusaidia kujenga na kulinda amani katika nchi hii.

Na moja kwa moja naelekea kupata mawazo kwamba pengine viongozi wengine wa dini wanatumika kwa maslahi ya kisiasa. Na jambo hili, licha ya kuwashushia heshima, ushawishi na mvuto baadhi ya viongozi wa dini mbele ya jamii, ni hatari kwa amani ya nchi yetu!

Source:

from
cleardot.gif
Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>reply-to
cleardot.gif
wanabidii@googlegroups.com
to
cleardot.gif
Wanabidii Mawazo <wanabidii@googlegroups.com>
date
cleardot.gif
18 January 2011 17:11subject
cleardot.gif
RE: [wanabidii] TAMKO LA BAKWATA DSM KUHUSU ARUSHAmailing list
cleardot.gif
<wanabidii.googlegroups.com>
 
Kwenye hili la maslahi ya kitaifa masheikh watoeni,kwenye maslahi ya waislamu pekee na dini yao..........count them in! Wao wanaamini shida walizonazo zinatokana na wao kuwa waislamu na kutokupewa haki sawa kwa kuwa wao ni waislamu na si kama watanzania as if shida zimegawanyika kutokana na dini au effect za ufisadi zinaenda kwa watu wa dini fulani tu.
Maaskofu tuko nao kwenye maslahi ya kitaifa na ya kujenga roho,sasa sioni wapi watakutana???wawe na sauti moja. kila mmoja ana priority na kufikia malengo yao kuna wanaotumia akili na busara na wapo wanaotumia hisia.:A S 39:
Nilianza kujisikia vibaya but thanks to God kwamba kuna watu wanajaribu kufikiria!Hivi hawa watu ambao kila kukicha wana hoja za kuwagawa wenzao kimafungu(kimakundi) wanatafuta nini hawa?Kwa nini tusiangalie tu hata swala la wakati,mwamko wa wananchi na mengine kama hayo ambayo yanawezakuwa kuwa yalifanya watu wasiseme at that time?Au ni nani amewahi kusema labda Bosi Mkapa ni msafi kwenye hilo la ufisadi.Lakini hivi na hawa wanaona kuwa hata huyo "mwenzao" hataki huyo bosi agusweguswe? Hivi ni kweli HATUONI KUWA HOJA YA MAASKOFU NA WATANZANIA WOTE NI KWA MASLAHI YA NCHI? Au mimi sifuatilii haya mambo vizuri hivi hata pale Arusha Maaskofu walisema kwa sababu wameuawa wananchi wasio na hatia au kwa sababu aliyeathirika ni Mkristo? Hivi hapakuwa na Mwislamu Pale?......SHAME ON THEM! Ifikie wakati tuanze kufikiria! Au nitoe msimamo binafsi Guys......no offence but naanza kupata wasiwasi na Elimu plus Thinking capacity za baadhi ya ndugu zetu. NA HAWA WA JAMII HIYO WALIOSOMA WAJITOLEE KUWASAIDIA WENZAO KUWASILISHA MAWAZO SAHIHI!
 
Makala hii kuhusu Masheikh na Maaskofu imeandikwa na Mzee Mwanakijiji inatia moyo kuonyesha angalau mwana JF mmoja amejitokeza waziwazi kwa kuwakosoa Viongozi wetu wa dini 2 kubwa hapa nchini! soma makala yenyewe:

Nisikilizeni enyi masheikh na maaskofu!

Mimi nakubaliana na yote uliyotaja Mzee ila ushauri wangu kwa viongozi wa dini kama wataungana kwa lengo la kupinga dhulma basi muungano huo usiwe wa kibubusa bali uwe na masharti na kama masharti hayo yatavunjwa basi muungano huo uvunjike na kila mtu achukue jembe akalime!

Baadhi ya masharti hayo ya kuungana viongozi wa dini nashauri yafuatayo:

1) Kanisa liombe radhi kwa Watanzania kwa kufurahia madhambi yote yaliyofanywa na Serikali tangu ya awamu ya kwanza, ya pili, na ya 3! baadhi ya madhambi hayo ni Utawala wa Julius kuwakamata na kuwatia jela viongozi wa dini ya Kiislamu bila ya kuwafikisha mahakamani!

Mfano ni Mufti mkuu wa kwanza Tanzania Sheikh Mohamed Bin Ameir, Rais wa Jumuiya ya EAMWA Tanzania Sheikh Tewa Saidi tewa, Katibu Mkuu wa EAMWA Bibi Titi Mohamed na Julius kuivunja jumuiya hiyo tukufu iliyowaletea maendeleo makubwa Waislamu wa Tanzania na kuwaletea BAKWATA iliyoasisiwa kwa kutumia katiba inayofanana na katiba ya TANU! ndio maana mpaka leo tuna Shehe wa Mkoa, wilaya, kata na kijiji kama ilivyo kwa CCM mwenyekiti wa CCM mkoa, wilaya nk.

2) Kanisa liombe radhi kwa kushirikiana na Serikali ya Nyerere kumpachika Padre ktk Wizara ya Elimu ili asimamie uchakachuaji wa mitihani ya Secondary, high school na hata Chuo kikuu cha Dar, ili kuwachuja wanafunzi walio waislamu na kuwapendelea wakristo!

Mfano mimi mwenyewe nikiwa darasa la 7 jumla ya wanafunzi tulikuwa 30, waislamu walikuwa 17, wakristo 8, na Hindus 5 na kila mtihani kuanzia darasa la 4-7 mitihani yote walikuwa waislamu wakiongoza kuanzia namba 1,2,3,4,5,mpaka 7 lakini cha kusikitisha matokeo ya kuingia Secondary walifaulu wakristo 7, waislamu 2 na baniani 1 kwanini? ina maana hawa waislamu hawakudurusu?

Ukifuatilia ya Secondary mpaka chuo kikuu utakuta mapungufu kama hayo!

3) Kanisa liombe radhi kwa kunyamaza wakati Serikali ya Mwinyi ilipowauwa Waislamu wa zanzibar walipoandamana mwaka 1988 wakipinga kauli ya Mama Sofia kauwawa ya kutaka Qurani ifanyiwe mabadiliko!

4) Kanisa liombe radhi kwa kuishinikiza serikali ya Mkapa kuwakamata Waislamu na kisha kuwauwa ndani ya msikiti wa Mwembechai na kusababisha wengine kuwa walemavu wa maisha mfano ni Mtoto Chiku alimiminiwa risasi kama maji! Rejea kauli ya Paroko Camilius Lwambano An-nuur Na. 201

4) Kanisa liombe radhi kwa kubariki mauaji ya Wafuasi wa CUF huko Unguja na Pemba mwaka 2001!

5) Kanisa lisijiingize ktk madai ya Waislamu kwa Serikali kuhusu Mahakama ya Kadhi na OIC!

6) Makanisa hasa ya Kilokole yawache tabia ya kutembelea nyumba wanazoishi waislamu na kugawa Biblia bure kwani Waislamu wakijibu mapigo sidhani kama Kanisa litafurahi!

7) Makanisa ya Kisabato na Kilokole waache tabia ya kuja na magari ya tarumbeta na kuimba kwa sauti kubwa karibu na Misikiti wakati Waislamu wako ktk sala hivyo kusababisha usumbufu na kukosa utulivu ndani ya ibada zao! huo ni uchokozi!!

8) Mwisho na muhimu- Kanisa liwe na tabia ya uvumilivu pale Waislamu wanapohubiri kuwa Yesu si Mungu kwani wao nao huvumilia wakisikia Wakristo wakimuita Yesu kuwa ni Mungu!

Kama Kanisa liko tayari kufuata masharti haya basi Waislamu wako tayari kushirikiana na Kanisa kukemea maovu ktk msimamo wa pamoja kinyume chake kila mbwa afoke kivyake!

Nakushukuru Mzee Mwanakijiji kwa makala yako safi lakini...............

Nashukuru kwa mawazo yako mema Mkulu!
Ila kuna msemo kwamba sikio la kufa halisikii na nabii hakubaliki kwao!

Kadogo ametoa masharti kwamba Kanisa liombe radhi na ameyataja ya kuyaombea radhi
Nimejiuliza kama kanisa nani aombe radhi Luambano Pengo Malasusa Kilaini Pope Benedicti ima Mtikila
mf;Mtikila alimsema sana Nyerere kuhusu uongozi wake! akamsema Mkapa kwamba hana uchungu na nchi hii kwa sababu ni Mmetu toka msumbiji Kilaini alitamka kwamba Kikwete ni chaguo la Mungu wengi wakapinga hao Wote ni Kanisa kwa mujibu wa kadogoo wote waombe radhi.

Ameshindwa kutenganisha kauli ya mtu binafsi na Kanisa. na hilo ni tatizo
Mf;Kanisa katoliki wana taratibu ya kutoa matamko yao kupitia NYARAKA ZA KICHUNGAJI na wanahimiza matendo mema na kuelekeza kuchagua viongozi waadilifu leo mkichagua kiongozi asiye muadilifu Kanisa Katoliki linahusika vipi?

Suluhisho!;
Waislamu wanaamini kwamba kisasi ni haki lakini Allaah amemshushia Mtume wake(Mohammad Saw) Uvuvio kwamba KUSAMEHE NI BORA!! Kumbe basi kusamehe kama ni bora tufuate kilicho bora ni kauli ya Haki Mungu, Kama mmeona mmeonewa Sameheni!
MSAMAHA NI BORA!
Tuanze mkutano wa katiba inayo kidhi haja ya wote wenye nchi.....
 
Huwa najitahidi sana kutokushiriki mjadala wowote unaogusia masuala ya imani, hii ni kwa sababu mara nyingi wengi wetu tunajikuta badala ya kuangalia masuala yanayotugusa wote (bila kujali imani zetu), tunaishia kuvutana kuwa nani ana imani bora na yenye uhakika wa kuiona pepo zaidi. Kuna masuala ya hali duni ya maisha ya mtanzania, mahitaji muhimu kama nishati, miundo mbinu mibovu, huduma za afya zisizo za uhakika (hasa kwa wenzetu wa maeneo ya vijijini - bila kuwa na maana kuwa za mijini zinajitosheleza). Hivi kweli issue zote hizi zinahitaji uwe na dini ili kuziona au kukemea kama mambo hayaendi sawa?

Na kwa sasa tunaanza kunyoshea vidole viongozi wa dini kuwa ooh utawala wa Nyerere/Mkapa walikuwa wapi, may be its very true kuwa viongozi wote wa kidini walikuwa wamelala usingizi mnono, kwa sababu wote walikuwa na nafasi ya kukemea uozo uliokuwa unafanyika! Mimi nafikiri utandawazi nao unafumbua mambo, inawezekana kabisa kuwa miaka 10 - 15, haya madudu yanayofichuliwa sasa hivi yalikuwa mara 100 zaidi kwa sababu tu hatukuwa na taarifa nayo. Sasa leo hii tunasikia ma-issue ya EPA, roho ndio zinazidi kutuuma zaidi kuona hamna cha maana kinachofanyika zaidi ya waliopelekea yote hayo bado wanapewa kahawa na kashata, na kushiriki kahawa hiyo pamoja na wale tunaotegemea wawakemee.

Tujiulize swali fupi, kwani sie tunaotoa maoni hapa, haya maoni na mijadala hii kwa nini haikufanyika hicho kipindi cha nyuma? Je, nasi tulaumiwe kwa kukalia maoni hayo hadi leo hii?
 
Back
Top Bottom