Sikizeni enyi masheikh na maaskofu!

Sikizeni enyi masheikh na maaskofu!

Huu utapiamlo wa udini utaifikisha wapi Tanzania? Viongozi wa kweli wa kidini hawaweki maslahi binafsi mbele, kinachoongelewa hapa ni ubinafsi tu hakuna dini, viongozi wa kweli wa kidini hukemea maovu bila kujali nani anaongoza, uraisi wa Kikwete unamnufaisha vipi muislamu wa kawaida? Watanzania wengi wanakabiliwa na hali ngumu ya maisha badala ya kuongelea masula ya kimsingi, tunakwepesha hoja na kuangelea mambo ambayo hayana maslahi kitaifa. Dini ina nafasi yake ndani ya jamii lakini ni hatari inapotumika kuendeleza maovu. Tuangalie mfano hai Tunisia waliomuondoa madarakani Beni Alli si waislamu bali watunisia waliopinga udhalimu wake. Dini na siasa haviendi pamoja, mashekhe na maaskofu/mapadri mnaotaka kujiingiza kwenye siasa vueni kanzu na majoho vinginevyo mtakuwa wanafiki.

umekuja vizuriii mwishoni umejchanganya

Huyu askofu au shehe katiba ya nchi inamruhusu kushiriki siasa
Pia ni kiungo kati ya binadamu na Mungu.

Utamkwepea wapi mtu wa dini
Hata siku moja Huwezi kumkwepa!
Mwizi unapo mkemea wewe ni mwizi acha Wizi sidhani kama atafurahi mwanangu.

Ukisikia kelele vueni majoho ujue hapo fisadi limebanwa kiukweli

siasa haina unifomu eti joho kanga au suti pia haina ubaguzi wa aina yeyote

Tumeanza kukua sasa mwanangu!
 
Jukwaa limeshagawanyika tayari kwa misingi ya udini!!! It is a shame!
Hii inanikumbusha kipindi fulani kwenye bunge la tisa ambapo maada ilikuwa 'mahakama ya kadhi' hapo ndipo bunge lilipasuka ghafla na kula la dini ya waisilamu vs wakristo!
Jambo hili lilinisononesha sana kama ilivyo sasa kwa jukwaa hili!!!
Jamani maswala yoyote yanayohusu kikundi fulani cha dini yajadiriwe kwenye misikiti/masinagogi na wala yasiihusishe intervention ya serikali ama watu wengine wasiohusika na kikundi hicho cha dini!:shock::shock::shock::shock:
 
Nimewasoma sana yaliyoongelewa yana maana sana kwa pande zote mbili, tukianza chuki kuwa mtu anajiona hafai kwa kuwa hakupewa nafasi katika jamii fulani kuongoza serikali basi tutakuwa watumwa, kila dini, kila kabira likianza kutoa mawazo yake na mtazamo wake na kuusililiza hatutafika mbali, kwani kuna unafiki mwingi, kujipendelea, wivu na wengi mabaya, tukianza na dini, wanapotaja taja Watu wa dhehebu la Kristo sio wote kuwa wanajumuika wote kudai haki yao, kwenye Ukristo kuna Dini Zaid ya Mia na Kwenye Uislam Zaidi ya nane, Ubaguzi huu sio tu ni kwa jumuia ya Wanzania hata huko Ulaya mambo haya yapo. Ukienda India kuna madhehebu ya Kikrsto ambayo dini ya Kiislamu inadhulumu aki yao , hata kufikia kuwaua kabisa. Tukirudi kwenye Makabila yapo makabila mbali kuwa na uwezo wa kuongoza lakini yalipigwa STOP wti kwa kuwa ni makubwa yatmeza wengine, hilo sio sahihi. Kuwa kiongozi sio lazima utoke kabila fulani kwani Tanzania ni ya wote sote. Kama kuna maana nyingine ya kuchagua viongozi kwa kutumia dini, Basi tufanye Hivi, Safari hii awamu ya JK ikiisha kuna Dini ya Mzee wetu Kingunge naye apewe Nafasi, Baada ya Hapo kuna dini ya Freemasons nayo ipewe nafasi nafikri malamiko yataisha.
 
1. Mwizi unapo mkemea wewe ni mwizi acha Wizi sidhani kama atafurahi mwanangu.

2. Ukisikia kelele vueni majoho ujue hapo fisadi limebanwa kiukweli

siasa haina unifomu eti joho kanga au suti pia haina ubaguzi wa aina yeyote

Tumeanza kukua sasa mwanangu
!

Kwenye RED : Nakubaliana jizi likibanwa hakika litaanza kurusha mateke mpaka liwekwe kona likose pa kupenyezea hayo ndo tunayashuhudia majizi yameamua kutumia ICC ili yaweze kuchukua mchana kweupe kwa maelezo ya uungwana etc.

Kwenye Blue : Chatanda Mary is better placed to describe the uniforms for the Politicians .
 
Kawni mwenzangu una kiwango gani cha elimu?
Tz tunatumia sheria za muingereza amabzo mtu yeyote hana hatia mpaka apatikani na kosa na mahakama (Every body is innocent until proved guilty). Ktk nchi inayofuata utawala wa sheria kama tz ni makosa kuwahukumu akina Mramba na wenzake kuwa ni mafisadi wakati mahakama haijathibitisha hilo.

Jk alichokifanya ni kuwapeleka mahakamani,tambua kuwa katika utawala wa sheria Rais hatakiwi kuingilia mahakama kwani ni mihimili tofauti.Kazi ya mahakama ni kuwahukumu. Lakini wengine wenu kwa ufinyu wa uelewa mnataka jk awaweke ndani tu kwa tuhuma,huo si utawala wa sheria.
Suala la maaskofu kumpiga vita jk hilo sio siri kwani hatuishi mbinguni tunaishi hapahapa tz tunapata habari yanayoongelewa makanisani,kumbuka tuna mchanganyiko wa familia moja kukuta waumini wa dini mbalimbali hivyo kuna mambo ambayo ni vigumu ndugu yako wa damu kukuficha hata kama mko dini tofauti.Mbona sijawahi sikia maaskofu wakisimama na kusema kuwa Mkapa ashitakiwe kwa makosa aliyofanya akiwa Rais?

Mwanangu waswahili wanasema 'Mbaazi ukikosa maua husingizi jua'!

Tatizo hapa sio una au nina elimu gani tatizo kubwa tulilo nalo watg ni KUJITAMBUA Vilevile kwa viongozi wetu hawana mawazo mapya wala maono hasa kwa nyakati hizi za vita ya uchumi duniani

Kuhusu sheria nadhani rais wa tz akisha apishwa ana mamlaka kuu na uwezo wa yeye kuwa juu ya sheria upo bila shaka. Hata spika Sita bila kuuma maneno aliwahi kumueleza mh kwamba kama kuna sheria ambayo ni kikwazo kwako kiutekelezaji ilete tuiweke sawa!

Kwa hiyo kujificha kwenye sheria bado hakukidhi haja na sababu au utetezi wa kutowashughulikia Mafisadi

Uwezo na sababu zipo nyingi!

Ima dhamira na kauli thabiti tu ndio tatizo.

Kumbukumbu zangu zinanikumbusha kwamba ktk awamu zilizo pita sikusikia Kina Basalehe au shehe kumkemea mkapa labda unikumbushe. ila nimemkumbuka rev Mtikila aliwahi kumkemea Mkapa kwamba hana uchungu na nchi hii kwa sababu ni Mmetu toka Msumbiji. jee mashehe walikuwa likizo?

MMUNGU Anatufahamisha kuwa
'ISEME HAKI HATA KAMA INAUMA'
 
Mwanangu waswahili wanasema 'Mbaazi ukikosa maua husingizi jua'!

Tatizo hapa sio una au nina elimu gani tatizo kubwa tulilo nalo watg ni KUJITAMBUA Vilevile kwa viongozi wetu hawana mawazo mapya wala maono hasa kwa nyakati hizi za vita ya uchumi duniani

Kuhusu sheria nadhani rais wa tz akisha apishwa ana mamlaka kuu na uwezo wa yeye kuwa juu ya sheria upo bila shaka. Hata spika Sita bila kuuma maneno aliwahi kumueleza mh kwamba kama kuna sheria ambayo ni kikwazo kwako kiutekelezaji ilete tuiweke sawa!

Kwa hiyo kujificha kwenye sheria bado hakukidhi haja na sababu au utetezi wa kutowashughulikia Mafisadi

Uwezo na sababu zipo nyingi!

Ima dhamira na kauli thabiti tu ndio tatizo.

Kumbukumbu zangu zinanikumbusha kwamba ktk awamu zilizo pita sikusikia Kina Basalehe au shehe kumkemea mkapa labda unikumbushe. ila nimemkumbuka rev Mtikila aliwahi kumkemea Mkapa kwamba hana uchungu na nchi hii kwa sababu ni Mmetu toka Msumbiji. jee mashehe walikuwa likizo?

MMUNGU Anatufahamisha kuwa
'ISEME HAKI HATA KAMA INAUMA'

Then, hujawahi kumsikiliza..
 
umekuja vizuriii mwishoni umejchanganya

Huyu askofu au shehe katiba ya nchi inamruhusu kushiriki siasa
Pia ni kiungo kati ya binadamu na Mungu.

Utamkwepea wapi mtu wa dini
Hata siku moja Huwezi kumkwepa!
Mwizi unapo mkemea wewe ni mwizi acha Wizi sidhani kama atafurahi mwanangu.

Ukisikia kelele vueni majoho ujue hapo fisadi limebanwa kiukweli

siasa haina unifomu eti joho kanga au suti pia haina ubaguzi wa aina yeyote

Tumeanza kukua sasa mwanangu!

Siasa ni uwongo unofanana na ukweli, ndio maana ni rahisi kwa wanasiasa kutoa sababu kila wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao na wananchi siku zote tunakubaliana na uwongo wao, unakumbuka ahadi za meli Kigoma, uwanja wa ndege Mara, vibajaji kwa wajawazito zile zote ni kamba sio kwamba hajui kama alikuwa anawalaghai wapiga kura bali ni moja mbinu za kisiasa kwenye kutafuta kura. Dini ni imani ya kiroho wote tunaamini mafundisho ya dini ni ukweli mtupu. Siasa na Dini havijichanganyi ndio maana Quran na Bible havitumiki kama katiba .
 
Naona wana JF sasa tunaelekea kubaya kujadili issue za udini, mtu anapohesabu mapungufu ya upande mmoja na kuweka kama ndiyo agenda ya kitaifa ni kupoteza maana na uhalisia wa mjadala, leo tunaweza kusema kipindi cha uongozi wa mwl nyerere waislamu walionewa, kwa vile Nyerere mkristo, je kipindi cha Mwinyi, naye alikuwa mkristo, kwanini waislamu wapate dahama hiyo, Je unaliongeleaje waislamu walivyo choma moto mabutcher ya kiti moto dar, yalikuwa yamejengwa kwenye maeneo ya misikiti! walivyokuwa wanachoma shule za sekondary za mission unaliongeleaje hili, wakati wakristo wanawekeza kwenye elimu waislamu wanawekeza kwenye madrasa kwenye kusoma elimu ya dini zaidi na hata wengi wao wamesoma shule za kikristo mfano Rais wako Jk Amesomeshwa na kanisa je ni mkristo!, leo bila aibu mtu anaibuka na hisia zake na kufanya topic za kujadili, huku ni kutugawa wana Jf, Mimi na shauri dini kila mtu anayakwake, issue ya imani ni nzito. tuiache.
 
Naona wana JF sasa tunaelekea kubaya kujadili issue za udini, mtu anapohesabu mapungufu ya upande mmoja na kuweka kama ndiyo agenda ya kitaifa ni kupoteza maana na uhalisia wa mjadala, leo tunaweza kusema kipindi cha uongozi wa mwl nyerere waislamu walionewa, kwa vile Nyerere mkristo, je kipindi cha Mwinyi, naye alikuwa mkristo, kwanini waislamu wapate dahama hiyo, Je unaliongeleaje waislamu walivyo choma moto mabutcher ya kiti moto dar, yalikuwa yamejengwa kwenye maeneo ya misikiti! walivyokuwa wanachoma shule za sekondary za mission unaliongeleaje hili, wakati wakristo wanawekeza kwenye elimu waislamu wanawekeza kwenye madrasa kwenye kusoma elimu ya dini zaidi na hata wengi wao wamesoma shule za kikristo mfano Rais wako Jk Amesomeshwa na kanisa je ni mkristo!, leo bila aibu mtu anaibuka na hisia zake na kufanya topic za kujadili, huku ni kutugawa wana Jf, Mimi na shauri dini kila mtu anayakwake, issue ya imani ni nzito. tuiache.

Una ushahidi gani kuwa Waislamu walichoma moto Shule za Mission? kuhusu ushauri wako kuwa Issue ya imani ni nzito, tuiache! nadhani ni kutaka kufichaficha maradhi lakini kumbuka kila chenye kufunikwa funikwa au kufichwa fichwa basi kuna uozo ndani yake na matokeo ni kilio?

Mimi nadhani kila mtu atoe hoja zake na wananchi waachwe watoe uamuzi kwani kila mtu ana kichwa chake na namna ya kuchambua na kutafakari kwa kutumia akili yake! hivyo naomba tuache siasa za kizamani za kuogopa kuchanganya Dini na Siasa!! zama hizo zimeshapitwa na wakati! hata huko Ulaya kuna vyama vya kidini vinavyoongoza Serikali hasa huko Ujerumani nk. sasa kwanini tunataka kuwazuia waumini wasishiriki Siasa?

Mimi ningefurahi sana kama Katiba yetu mpya itaruhusu vyama vyenye mrengo wa kidini kushiriki siasa! maana ni miaka 50 sasa tangu tumepata Uhuru, bado Umaskini, ujinga na maradhi yametugubika na chanzo mimi nadhani ni utawala wa chama kisicho na dini! hata vyama vya upinzani vingine vinafuata mrengo wa kulia, kushoto au wa kati! hivyo umefika wakati sasa siasa ibinafsishwe na soko huria litandae ili tupate na vyama kama Cristian Demokratic Movenment, Islamic Progressive Party, Hindus Tanzanians Party, nk.
 
Kuna mtu anaweza kunisaidia kwenye hili suala la mitihani. Nijuavyo mimi watahiniwa wote walipewa namba, sasa wakati wakisahihisha hiyo mitihani walijuaje kama hizi ni namba za waislamu?
 
unajua tatizo la hawa wenzetu wakianza kufundishana madudu, wanasahau hata mafundisho ya mtume wao. Angalia Algeria, walifundishana madudu mwisho wakauana wenyewe. Kwote Nigeria, sudan etc ni hivi hivi kupandikizana chuki ati kuna machawi anafaidi wakati kila mtanzania anakatiwa umeme.

Hal;afu sijawahi kuona wakizungumzia mambo ya msingi ya kitaiffa zaidi ya kadhi, kuonewa, etc. Mimi nafikiri wakati wac wao kubailika ni sasa.
 
Kuna mtu anaweza kunisaidia kwenye hili suala la mitihani. Nijuavyo mimi watahiniwa wote walipewa namba, sasa wakati wakisahihisha hiyo mitihani walijuaje kama hizi ni namba za waislamu?

Unajua huu uwongo mtupu, toka lini wasahihishaji toka mikoa yote ya tanzania wawe na muda wa kusahihisha kwa kujali dini, wakati mtu amefuata mshikomwake. Tatizo lilikuwqa ni kiwangio cha elimu , madrasa imewachklewesha sana.
 
Makala hii kuhusu Masheikh na Maaskofu imeandikwa na Mzee Mwanakijiji inatia moyo kuonyesha angalau mwana JF mmoja amejitokeza waziwazi kwa kuwakosoa Viongozi wetu wa dini 2 kubwa hapa nchini! soma makala yenyewe:

Nisikilizeni enyi masheikh na maaskofu!

Mimi nakubaliana na yote uliyotaja Mzee ila ushauri wangu kwa viongozi wa dini kama wataungana kwa lengo la kupinga dhulma basi muungano huo usiwe wa kibubusa bali uwe na masharti na kama masharti hayo yatavunjwa basi muungano huo uvunjike na kila mtu achukue jembe akalime!

Baadhi ya masharti hayo ya kuungana viongozi wa dini nashauri yafuatayo:

1) Kanisa liombe radhi kwa Watanzania kwa kufurahia madhambi yote yaliyofanywa na Serikali tangu ya awamu ya kwanza, ya pili, na ya 3! baadhi ya madhambi hayo ni Utawala wa Julius kuwakamata na kuwatia jela viongozi wa dini ya Kiislamu bila ya kuwafikisha mahakamani!

Mfano ni Mufti mkuu wa kwanza Tanzania Sheikh Mohamed Bin Ameir, Rais wa Jumuiya ya EAMWA Tanzania Sheikh Tewa Saidi tewa, Katibu Mkuu wa EAMWA Bibi Titi Mohamed na Julius kuivunja jumuiya hiyo tukufu iliyowaletea maendeleo makubwa Waislamu wa Tanzania na kuwaletea BAKWATA iliyoasisiwa kwa kutumia katiba inayofanana na katiba ya TANU! ndio maana mpaka leo tuna Shehe wa Mkoa, wilaya, kata na kijiji kama ilivyo kwa CCM mwenyekiti wa CCM mkoa, wilaya nk.

2) Kanisa liombe radhi kwa kushirikiana na Serikali ya Nyerere kumpachika Padre ktk Wizara ya Elimu ili asimamie uchakachuaji wa mitihani ya Secondary, high school na hata Chuo kikuu cha Dar, ili kuwachuja wanafunzi walio waislamu na kuwapendelea wakristo!

Mfano mimi mwenyewe nikiwa darasa la 7 jumla ya wanafunzi tulikuwa 30, waislamu walikuwa 17, wakristo 8, na Hindus 5 na kila mtihani kuanzia darasa la 4-7 mitihani yote walikuwa waislamu wakiongoza kuanzia namba 1,2,3,4,5,mpaka 7 lakini cha kusikitisha matokeo ya kuingia Secondary walifaulu wakristo 7, waislamu 2 na baniani 1 kwanini? ina maana hawa waislamu hawakudurusu?

Ukifuatilia ya Secondary mpaka chuo kikuu utakuta mapungufu kama hayo!

3) Kanisa liombe radhi kwa kunyamaza wakati Serikali ya Mwinyi ilipowauwa Waislamu wa zanzibar walipoandamana mwaka 1988 wakipinga kauli ya Mama Sofia kauwawa ya kutaka Qurani ifanyiwe mabadiliko!

4) Kanisa liombe radhi kwa kuishinikiza serikali ya Mkapa kuwakamata Waislamu na kisha kuwauwa ndani ya msikiti wa Mwembechai na kusababisha wengine kuwa walemavu wa maisha mfano ni Mtoto Chiku alimiminiwa risasi kama maji! Rejea kauli ya Paroko Camilius Lwambano An-nuur Na. 201

4) Kanisa liombe radhi kwa kubariki mauaji ya Wafuasi wa CUF huko Unguja na Pemba mwaka 2001!

5) Kanisa lisijiingize ktk madai ya Waislamu kwa Serikali kuhusu Mahakama ya Kadhi na OIC!

6) Makanisa hasa ya Kilokole yawache tabia ya kutembelea nyumba wanazoishi waislamu na kugawa Biblia bure kwani Waislamu wakijibu mapigo sidhani kama Kanisa litafurahi!

7) Makanisa ya Kisabato na Kilokole waache tabia ya kuja na magari ya tarumbeta na kuimba kwa sauti kubwa karibu na Misikiti wakati Waislamu wako ktk sala hivyo kusababisha usumbufu na kukosa utulivu ndani ya ibada zao! huo ni uchokozi!!

8) Mwisho na muhimu- Kanisa liwe na tabia ya uvumilivu pale Waislamu wanapohubiri kuwa Yesu si Mungu kwani wao nao huvumilia wakisikia Wakristo wakimuita Yesu kuwa ni Mungu!

Kama Kanisa liko tayari kufuata masharti haya basi Waislamu wako tayari kushirikiana na Kanisa kukemea maovu ktk msimamo wa pamoja kinyume chake kila mbwa afoke kivyake!

Nakushukuru Mzee Mwanakijiji kwa makala yako safi lakini...............

Kwa hiyo wewe ni msemaji wa waislam?
 
Kuna mtu anaweza kunisaidia kwenye hili suala la mitihani. Nijuavyo mimi watahiniwa wote walipewa namba, sasa wakati wakisahihisha hiyo mitihani walijuaje kama hizi ni namba za waislamu?

Matumizi ya namba yalianza kutumika kipindi cha Aliekuwa Waziri wa Elimu wa kwanza Muislamu tangu tupate Uhuru Marehemu Profesa Kighoma Ali Malima mwaka 1988 kabla ya hapo wizara hii haijawahi kuongozwa na Muislamu na matumizi ya majina ndio yalitumika na kushtukiwa na Waziri Malima!!
 
Siasa ni uwongo unofanana na ukweli, ndio maana ni rahisi kwa wanasiasa kutoa sababu kila wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao na wananchi siku zote tunakubaliana na uwongo wao, unakumbuka ahadi za meli Kigoma, uwanja wa ndege Mara, vibajaji kwa wajawazito zile zote ni kamba sio kwamba hajui kama alikuwa anawalaghai wapiga kura bali ni moja mbinu za kisiasa kwenye kutafuta kura. Dini ni imani ya kiroho wote tunaamini mafundisho ya dini ni ukweli mtupu. Siasa na Dini havijichanganyi ndio maana Quran na Bible havitumiki kama katiba .

Mwanangu Chama siasa si uongo kama wanavo tuaminisha wanasiasa tuamini, ili pale wanaposhindwa kuwajibika tusiwawajibishe mwana!
kwa wenzetu wanaojua maana halisi ya siasa basi atakaye ahidi bila kutekeleza lazima awajibike au awajibishwe na uma!

Tatizo la wanasiasa hasa hapa kwetu hawana dhamana kwa kile waahidicho mf; ninapo kuja unikopeshe 10000 itabidi uombe dhamana toka kwangu kama tv ili nikishindwa kulipa wewe utachukua tv yangu.
Leo msiasa anakuahidi meli kama kisiwa, kukuondolea ujinga brbr za juu nk nk nk. Dhamana yake ni nini ili asipotekeleza nimfanye nini?mf,msiasa mmoja anasema nisipo tekeleza mnifukuze kazi, mwingine anasema mimi nisipo tekeleza MNIUE Kumbe basi mwenye dhamana kubwa ni yule aliyeweka uhai wake dhamana mnamchagua mnampa muda wa utekelezaji akishindwa kutekeleza mnampeleka Jangwani shaba tu!
Hapo hatajitokeza kiongozi/msiasa MSANII!
Kuhusu dini na siasa vinasaidiana. Hasa ndipo pale mwanasiasa anashika kitabu cha dini kuapa kwamba atailinda katiba asipoilinda katiba kitabu cha dini KIMZURU Ndipo wanasiasa wengi wanapodhurika.
 
M.M. Mwanakijiji​
KAMA kuna wakati nimetamani kunyofoa nywele zangu kwa hasira na kushangazwa ni wakati kama huu. Hakuna watu ambao wamenishangaza juu ya misimamo yao kuhusu maslahi ya taifa kama hawa ndugu zetu masheikh na maaskofu.

Kuna kitu hakiko sawa katika kundi hili na kuna wakati mtu ajitokeze na kuwaambia ukweli. Nadhani wanatumia majoho na kanzu zao za ibada kuanza kulichanganya taifa na kutugawanya wananchi kwa misingi ya kidini huku wao wenyewe wakijiaminisha kuwa wanafanya mapenzi ya Mungu. Nisikizeni enzi maaskofu na masheikh!

Sasa hivi kuna mgongano wa wazi kati ya viongozi hawa wa dini huku kundi moja likionekana kuwa kali dhidi ya serikali na kundi jingine likionekana kutafuta udhuru na kuitetea serikali.

Yote mawili yanajaribu kuaminisha watu kuwa yanafanya hivyo kwa masilahi ya taifa au masilahi ya watu wa kundi lao. Lakini kinachonishangaza zaidi ni kuwa mgongano huu wa viongozi wa dini haumsaidii Mtanzania wa kawaida bali unawaimarisha watawala madarakani; kwani wanajua kuwa nguvu ya kuwakemea haiko katika umoja.

Niliandika makala mwaka 2009 mwezi Oktoba nikielezea kile nilichokiita kuwa ni uenzetu huu yaani kama nilivyofafanua kuwa ni hisia ya kuona mtu mnayefanana kwa namna fulani anaonewa, kunyanyaswa au kulengwa na wengine kwa sababu ya vitu mnavyofanana na si sababu halisi. Nilielezea kwa kirefu katika makala ile kuwa mojawapo ya mambo ya hatari yanayotokea katika Tanzania ni kuwa tunauangalia ufisadi, uongozi na vitendo vya kukiuka maadili ya uongozi kwa rangi ya uenzetu.

Nakumbuka nilihoji (kama masheikh walivyohoji hivi majuzi) kuwa kuna mambo ambayo ni ya kifisadi yalifanyika chini ya utawala wa Rais Mkapa (Mkatoliki) ambayo yamelisababishia taifa hasara kubwa na aibu ya kutosha tu.

Nikauliza kuwa: Hakuna kiongozi yeyote wa Kikatoliki aliyekuwa na ujasiri wa kupiga kelele na kutaka Mkapa arudishe mali hizo za Watanzania alizojipatia kinyemela kinyume na Sheria ya Maadili ya Viongozi ya mwaka 1998 (ambayo yeye mwenyewe aliisaini).

Na hata leo hii ambapo serikali imekiri kuwa Mkapa alijipatia vitu hivyo kinyemela na kuamua kuvirudisha serikalini na kuwabambikizia Watanzania gharama ya kulipa madeni ya Kiwira hakuna kiongozi yeyote wa Kanisa aliyemtaka Mkapa kuwaomba radhi Watanzania na kutengeneza alichoharibu (reparation)?

Nisikilizeni enyi masheikh na maaskofu!

Na nikasema kuwa: Lakini leo hii (maaskofu) wamepata ujasiri mkubwa wa kusema ukweli mbele ya wenye madaraka (speaking truth to power) hasa pale wanayemsemea ni Mwislamu! Hapa, mtu mwingine anaona kuwa kama wangekuwa na ujasiri huo wa kukemea uovu mbele ya Mkapa labda mengine yasingefika huku. Kauli yangu hiyo imerudiwa hivi juzi na uongozi wa Kiislamu kwenye tamko lao la Karimjee. Ukweli ni kuwa uongozi wa Uislamu una hoja katika hilo.

Ni kweli wanahoja kwa sababu wakati leo hii kina Kardinali Pengo wanashangazwa na wananchi kuuawa mikononi mwa vyombo vya dola wengine tunauliza mbona walikufa watu Mwembechai na Pemba mikononi mwa polisi na hakuna maaskofu waliokuja juu?

Je, yawezekana ni kweli kuwa hawakuweza kufanya hivyo kwa sababu serikali ilikuwa inaongozwa na Rais Mkristu mwenzao? Hii hoja inaweza kuwa na nguvu zaidi kwa sababu miaka zaidi ya mitano tangu Mkapa atoke madarakani uongozi wa Wakristu nchini bado hawajathubutu kunyoshea mkono utawala wake kuwa ulichochea ufisadi huku sote tunajua kuwa wizi wa EPA, Meremeta na uvurugaji wa Katiba ulifanyika chini ya utawala wa Mkapa?

Sasa leo maaskofu wanaposimama na kuinyoshea vidole serikali ya Kikwete (Mwislamu) kwanini baadhi ya Waislamu wasione kuwa linatokea kwa sababu za tofauti ya kidini? Nisikizeni enyi maaskofu!

Ili maaskofu wapate mahali pa kusimamia wanapoikosoa serikali ya Kikwete ni lazima kwanza waombe msamaha kwa ukimya wao wakati Watanzania wameuawa Pemba na Mwembechai; si kwa sababu Waislamu waliuawa bali kwa sababu wananchi wameuawa.

Msimamo huo ungetakiwa uwe hivyo hata kama waliouawa wangekuwa ni Wapagani! Kwa kadiri maaskofu hawatoi tamko la kuchukua msimamo wa ufisadi na kutaja kwa majina utawala wa Mkapa, hawana ujasiri wa kumkemea Kikwete; si kwamba hawana hoja au hawana sababu lakini bila ya kusahihisha kosa lao la awali, Waislamu ni lazima na wana haki ya kushuku sababu ya maaskofu kufanya hivyo.

Lakini katika makala ile ile niliandika kitu kingine ambacho nacho kinatokea tena sasa hivi. Nisikilizeni enyi masheikh!

Niliandika hivi: Upande wa pili tunauona leo hii mahusiano kati ya baadhi ya makundi ya Waislamu na utawala wa Rais Kikwete ambaye naye ni Mwislamu. Licha ya madudu ambayo yanafanywa mbele yetu na mengine yenye kuwaathiri Waislamu bado hakujatokea kiongozi au uongozi wa Waislamu ambao wamethubutu kumuambia Kikwete na serikali yake maneno yenye ukweli.

Jambo hili nililiandika 2009 na sasa mwaka 2011 bado linasimama kama ushahidi wa usahihi wake. Hakuna kiongozi wa Kiislamu au chombo cha Waislamu ambao wamethubutu kunyoshea kidole serikali ya Kikwete kwenye masuala ya kitaifa.

Nilifafanua hili kwa sababu naam, wamekuwepo viongozi wa Kiislamu ambao wameilalamikia serikali kwenye masuala yenye kuwahusu Waislamu na tumeliona hili tena siku ya Jumamosi ambapo hoja zao za utetezi zinahusu kile wanachokiita kuwa ni masilahi ya Waislamu. Kama mtu amefuatilia mjadala wao na tamko walilolitoa ni wazi kuwa wamekerwa zaidi na maaskofu waliozungumzia suala la mauaji ya wananchi Arusha si kwa sababu maaskofu wamesema kitu kibaya bali zaidi kwa sababu maaskofu hawakuonyesha kujali hivyo wakati Waislamu walivyouawa huko nyuma. Kwao suala hili ni suala la kidini zaidi.

Niliandika hivi kwa kuhoji katika makala ile kama unabii wa kule tulikokuwa tunaelekea na hatimaye sasa tumefika: Hapa sizungumzii katika masuala yenye kuwagusa Waislamu tu (kama Kadhi, OIC, Hija n.k) bali nazungumzia yale ambayo yanawagusa wao pia kama Watanzania na wananchi. Masuala ya nishati, madini, nafasi za ajira n.k
Leo tunashuhudia mabilioni ya fedha zetu yanatumika kama hayana mwenyewe wakati watoto wetu bado wanahangaika na majengo mabovu ya shule, huduma na miundombinu mibovu katika maeneo mbalimbali licha ya mafanikio ya hapa na pale.

Masuala ya Richmond, Dowans, Loliondo n.k ambayo yanawahusisha baadhi ya watu wenye kufungamana na nchi za Kiislamu hakujavutia hasira ya Waislamu wa Tanzania. Kwanini? Kwa sababu ni wenzao? Kwamba kwa vile watu hawa wanajulikana kuwa ni Waislamu au wanatoka nchi za Kiislamu basi wasipingwe sana kwani wote hawa ni sehemu ya umma wa Waislamu?

Matokeo yake ni kuwa uongozi wa Waislamu Jumamosi hawajatoa tamko lolote kuhusu malipo ya Dowans kwa sabababu wanazozijua wao. Shura ya Maimamu hawajasimama kuhoji uhalali wa wananchi kuuawa huko Mbarali na Arusha kwa sababu mbona huko nyuma wananchi wengine walikufa mikononi mwa serikali?

Marafiki zangu kama kina Prof. Njozi (aliyeandika kitabu cha Mwembechai) mbona hajatoa tamko lolote la kuonyesha kukerwa na mauaji haya? Yawezekana uongozi wa Waislamu hawataki kuonekana na wenyewe wamesimama dhidi ya Rais Mwislamu mwenzao?

Nisikizeni enyi maaskofu na masheikh!

Tanzania ni Tanzania na ni kubwa kuliko makundi yenu ya kidini. Watanzania ni Watanzania zaidi ya Wachagga, Wandengereko, Wamatumbi na Wanyiha! Utanzania wetu uko juu zaidi kuliko dini zetu.

Wale ambao wanataka kutugawa kwa sababu ya dini zetu wanafanya makosa ambayo gharama yake ni kuua Utanzania wetu.

Tunataka viongozi wa kidini ambao wanaposimama kutetea haki basi watetee haki bila kujali anayedhulumiwa ni nani! Hatutaki viongozi wa kidini ambao wanauliza kwanza ni dini gani badala ya kusimama na kupinga dhulma.

Jumatatu hii iliyopita huko Marekani wameadhimisha siku ya mwanaharakati za haki za kiraia na za kibinadamu Mchng. Martin Luther King Jr. Mchg. MLKJr. alitambua kuwa kutetea haki za watu weusi nchini mle haikuwa kwa sababu ya Ukristo wake kwani wengi walikuwa si Wakristu.

Hata Malcom X baadaye alikuja kuelewa kuwa ni haki za watu weusi wote zilizokuwa zinadhulumiwa. Uovu hauna dini na unatakiwa kupingwa na wenye dini na wasio na dini.

Nisikilizeni enyi masheikh na maaskofu; pataneni dhidi ya uovu ili muweze kuukabili. Msipopatana tutawaacha kwenye mataa na kama nilivyowahi kusema huko nyuma mtakuwa hamna mpango (you will become irrelevant)! Kwani wananchi watawashtukia kuwa na nyie mnaongozwa na majoho na kanzu zenu na hivyo Watanzania wasiwategemee kuwa ni watetezi wao.

Kwani hata hao maaskofu ambao leo hii wanaonyesha kuwa wanakerwa mbona hakuna hata aliyesimama kuandamana kupinga vitendo hivi vya kifisadi na dhuluma? Ni lini tutawaona walioshtushwa kina Pengo na Laizer wakisimama na kuongoza maandamano ya kuipinga serikali au uongozi wa dhulma? Je, Masheikh hawataweza kusimama dhidi ya ufisadi hata kama aneyehusishwa ni mtu wa msikiti wao? Au yanakuwa ni maslahi hadi pale yanpogusa maslahi ya Waislamu tu?

Ndugu zangu, kila zama zina mashujaa wake na kila shujaa ana ujumbe wake. Hizi ni zama zetu na ni katika zama hizi tutangeneza mashujaa wetu sisi wenyewe au historia itawanyanyua kati yetu. Haijalishi kama mashujaa hao watakuwa ni Wakristu, Waislamu, wasioamini, wenye kuamini kijadi au vinginevyo.

Hawa maaskofu na masheikh ambao wanafikiri wanaukiritimba wa mbinguni nina ujumbe mmoja kwao; sikilizeni enyi maaskofu na masheikh kwani nanyi zama zenu zinapita na Watanzania watasimama hata kama ni peke yao; kama watawala wetu walioshindwa nanyi msipoangalia mtaingia katika shimo la kusahauliwa kwa kushindwa kuukemea uovu na kumaanisha hivyo.

Ujumbe wangu uko wazi. Pataneni dhidi ya dhuluma na uovu kwani ni katika hilo tu mtahukumiwa. Kwani kama alivyosema Luther dhuluma mahali popote, ni dhuluma mahali pote.

Nisikilizeni enyi masheikh na maaskofu!

Source: Tanzania Daima
Tar. 19 January 2011,
By M.M. Mwanakijiji
Marudio tu
 
Back
Top Bottom