Mchango Huu nimeudaka kwenye forum ya wanabidii, nadhani unatoa picha ya masuala mengi kuhusiana na mada hii:
Kwa mujibu wa baadhi ya Magazeti, halikuwa Tamko la BAKWATA, ingawa katika Kongamano kulikuwa na baadhi ya Viongozi wa BAKWATA waliotajwa ambao yasemekana walililiunga mkono na kusema kwamba Tamko hili "ni la maana sana na likifanikiwa litaleta faraja kwa Waislamu na wananchi wote" (taz. Tanzania Daima ya jana).
Kimsingi Tamko hilo lilikuwa na mambo mengi ambayo mengi mengine tumeyazoea kuyasikia kutoka kwa Shehe Issa Ponda na Bassaleh. Nisingependa kuyarudia yote yaiyosemwa na viongozi hao lakini ningeomba kuongelea yale yaliyowatofautisha na maaskofu mintarafu vurugu za Arusha. Kwa ufupi wao walitofautiana na Maaskofu kwa kusema kwamba "yaliyotokea Arusha ni mgogoro wa kisiasa kwa hio si busara kwa Maaskofu kusimama mbele ya Chadema" na kuongeza kwamba: "kwa nini Maaskofu walikaa kimya wakati wa mauaji ya Zanzibar na sasa wanapiga kelele juu ya mauaji ya Arusha".
Kwanza sina uhakika kwamba ni kwa kiwango gani tunaweza kusema vurugu za Aurusha ni mgogoro wa kisiasa tu na hivyo Maaskofu hawapaswi kuingilia... Lakini zaidi ya hayo ni kwamba, Tamko hilo lilikuwa na mapungufu ya ukweli wa kihistoria, ama lilitaka kupotosha kwa makusudi umma kwa kusema kwamba Maaskofu walikaa kimya wakati wa mauaji ya Zanzibar.
Ukweli ni kwamba, baada ya mauaji ya raia 23 wasio na hatia yaliyotokea Zanzibar tarehe 26 na 27 Januari mwaka 2001, Maaskofu wakatoliki walitoa Tamko lao tarehe 23 Februari 2001 la kuelezea masikitiko yao juu ya ukatili uliofanywa na jeshi la polisi dhidi ya raia hao, na kuitaka Serikali ya Rais Mkapa wakati ule kufanya uchunguzi na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wote waliohusika.
Baada ya hapo, Maaskofu wa Kanisa katoliki hawakuishia hapo, wakawa mstari wa mbele ili kuhakikisha kwamba matukio ya kusikitisha kama hayo, hayajirudii tena katika nchi hii. Wakashawishi kuundwa kwa jukwaa la Viongozi wa dini mbali mbali kwa ajili ya kushughulikia amani na mazungumzano linalohirikisha wajumbe kutoka
BAKWATA, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Jumuiya ya Kikristo Tanzania na Ofisi ya Mufti Zanzaibar. Tangu wakati huo mpaka sasa, Maaskofu Katoliki wamekuwa wakibeba gharama zote za uendeshaji wa Jukwaa hilo ikiwemo mikutano n.k.
Wakati wa uchaguzi uliopita, Jukwaa hilo liliwatembelea viongozi wa vyama mbali mbali na kuwasihi wawaelekeze wafuasi wao kuwa na uvumilivu wa kisiasa wakati w kampeni, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi; na lilifaulu kuwatembelea, Maalim Seif Shariff Hamad, Dr. Slaa, Prof. Lipumba na Mhe. Kikwete. Baada ya kuyasema hayo, naomba niseme kwamba,
mshangao wangu ulikuwa mkubwa zaidi niliposoma katika gazeti hilo kwamba kiongozi huyo wa BAKWATA ambaye ni mjumbe wa Jukwaa hilo aliunga mkono Tamko hilo wakati yeye mwenyewe anajua mchango wa viongozi wenzake (Maaskofu) katika ujenzi wa amani na mazungumzano miongoni mwa wanajamii hapa Tanzania.
Amekuwa akishiriki vikao vingi tu na kuonyesha angalau
apparently, nia yake ya kutaka kupigania amani na maelewano miongoni mwa Watanzania. Sina uhakika kama aliyasema maneno hayo ambayo magazeti yalimnukuu ama kama alikuwa anaunga mkono yote yaliyokuwemo katika Tamko hilo.
Kama kweli aliyatamka hayo, na anaunga mkono yote yaliyo katika Tamko hilo, naanza kupata mashaka mengi juu ya baadhi ya viongozi wa dini kama wana nia ya kutusaidia kujenga na kulinda amani katika nchi hii.
Na moja kwa moja naelekea kupata mawazo kwamba
pengine viongozi wengine wa dini wanatumika kwa maslahi ya kisiasa. Na jambo hili, licha ya kuwashushia heshima, ushawishi na mvuto baadhi ya viongozi wa dini mbele ya jamii,
ni hatari kwa amani ya nchi yetu!
Source:
from
Edgar Mbegu <embegu@hotmail.com>reply-towanabidii@googlegroups.com
toWanabidii Mawazo <wanabidii@googlegroups.com>
date18 January 2011 17:11subjectRE: [wanabidii] TAMKO LA BAKWATA DSM KUHUSU ARUSHAmailing list<wanabidii.googlegroups.com>