Sikiri Mimi Maskini

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,994
156,296
Sikili mimi maskini,
Uvivu wangu nyumbani,
Ukiwa huu njiani,
Nakufa hapa kwa nini?
Sadiki sasa ashiba,
Chakula kingi kwa baba,
Nirudi tena kwa baba,
Nakufa hapa kwa nini?
.............................................
.................
Naomba radhi nimekosa,
Nitakuwa mtoto mwema sasa,
Shambani tena sitakosa,
Baba na mama nisameheni.
Nitalima kama Sadiki,
Nitalima wala sichoki,
Na nyumbani tena sitoki
Baba na mama nisameheni.
Kama umekumbuka jambo hapa bila
shaka wewe si wale waandikao 'x'
badala ya 's'
 
Fikiri mimi maskini,
Uvivu wangu nyumbani,
Ukiwa huu njiani,
Nakufa hapa kwa nini?
Sadiki sasa ashiba,
Chakula kingi kwa baba,
Nirudi tena kwa baba,
Nakufa hapa kwa nini?
.............................................
.................
Naomba radhi nimekosa,
Nitakuwa mtoto mwema sasa,
Shambani tena sitakosa,
Baba na mama nisameheni.
Nitalima kama Sadiki,
Nitalima wala sichoki,
Na nyumbani tena sitoki
Baba na mama nisameheni.
Kama umekumbuka jambo hapa bila
shaka wewe si wale waandikao 'x'
badala ya 's'

mkuu mie nikafikiri baada ya hapo ungeendelea na.... karudi baba mmoja toka safari ya mbali, kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili...watoto wake wakaja ili kumtaka hali, wakataka na kauli iwafae maishani!
 
Fikiri mimi maskini,
Uvivu wangu nyumbani,
Ukiwa huu njiani,
Nakufa hapa kwa nini?
Sadiki sasa ashiba,
Chakula kingi kwa baba,
Nirudi tena kwa baba,
Nakufa hapa kwa nini?
.............................................
.................
Naomba radhi nimekosa,
Nitakuwa mtoto mwema sasa,
Shambani tena sitakosa,
Baba na mama nisameheni.
Nitalima kama Sadiki,
Nitalima wala sichoki,
Na nyumbani tena sitoki
Baba na mama nisameheni.
Kama umekumbuka jambo hapa bila
shaka wewe si wale waandikao 'x'
badala ya 's'
Asante, umenikumbusha mbali!, nadhani hiki ni kitabu cha "Someni Bila Shida-3" Someni kwa Furaha" ndio vilikuwa vile vya darasa la kwanza na la pili, vya "JUMA NA ROZA".
Not sure anymore!.
Pasco
 
mkuu mie nikafikiri baada ya hapo ungeendelea na....
karudi baba mmoja toka safari ya mbali,
kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili...
watoto wake wakaja ili kumtaka hali,
wakataka na kauli iwafae maishani!

Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
roho naona yachinjwa, kifo kina nikabili,
kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
kama tunataka mali, tutapataje shambani?

Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
kama mnataka mali mtayapata shambani.

Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
kama mnataka mali, tutayapata shambani.

Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
wote wakashangilia, usemi wakakubali,
"KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".

Pasco
 
Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
roho naona yachinjwa, kifo kina nikabili,
kama mnataka mali, mtayapata shambani.

Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
kama tunataka mali, tutapataje shambani?

Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
kama mnataka mali mtayapata shambani.

Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
kama mnataka mali, tutayapata shambani.

Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
wote wakashangilia, usemi wakakubali,
"KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI".

Pasco

hahaAaaa asante sana bwana pasko! hakika umeifanya siku yangu ianze vyema...... naomba nisiwe mchoyo wa fadhila kwa kukutakia asubuhi njema
 
Asante, umenikumbusha mbali!, nadhani hiki ni kitabu cha "Someni Bila Shida-3" Someni kwa Furaha" ndio vilikuwa vile vya darasa la kwanza na la pili, vya "JUMA NA ROZA".
Not sure anymore!.
Pasco

Pasco nafikiri umechanganya hapa. Huo ushairi kweli ni toka kitabu cha darasa la tatu. Katika kitabu hicho kuna shairi jingine la sizitaki mbichi hizi.
Hicho kitabu cha Someni kwa furaha unachosema kilikuwa na hadithi za Bulicheka na Lizabeti. Hadidhi za Juma na Roza zilikuwa kwenye vitabu vya darasa la kwanza na la pili.
 
Kuna mwanafunz alkuwa darasan mawazo yake yalkuwa nyumban mwalmu kumuulza swal, akajbu kwa hofu " SKULAMBA SUKAR "
nafkr h n ya darasa la nne.
 
Pasco umenikumbusha Enzi zile nna maakili ile mbaya. Nikisoma kitu sisahau. Nikisoma kitabu all interesting quotes zinakaa kichwani day!

come to think of this sshairi la sikiri/fikiri, hayo maneno yalikuwa yanasaidia kuwakatisha tamaa vijana kukimbilia mjini ili kukwepa majukumu. Wknd moja najivinjari kuelekea kwenye mitkasi na shida zisizoisha, kwenye mataa akanigongea kioo binti omba omba. Hapo najilia spring rolls na goat chop na chai. Nikamuashiria sina fedha. Akaniambia nipe chakula. Nikamjibu automatikale nenda ukale nyumbani. Na huku najishawishi kabisa nisijusikie guilty.

mamangu alikuwa anasema kabisa. Usiuze utu Wako kwa ajili ya chakula, nguo AMA gari sijui na hereni. Soma! Komaa! Work hard! Hayo yote yatakufuata, it is just a matter of time unless you give up. Kuna watu wamelala njaa, wametembea peku, wamelala kwenye corridor na hatimae wametoka. Shairi la sikiri/fikiri linatukumbusha kutokuwa na tamaa. Ukiona zinduna....
 
Last edited by a moderator:
Pasco umenikumbusha Enzi zile nna maakili ile mbaya. Nikisoma kitu sisahau. Nikisoma kitabu all interesting quotes zinakaa kichwani day!

Hapo najilia spring rolls na goat chop na chai. ....
King'aa, ni goat chop ya wapi?, isije kuwa njia ya Kawe!, isije kuwa pale na Mlalakuwa JKT?.
Pasco
 
Wakazidi kumuuliza,wale watoto wawili,
Baba yetu ya thamani,sisi tunataka Mali.
Urithi tunatamani,Mali yetu ya halali.
Kama ipo mali,tutapataje shambani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom